Kitengo 14: Siku 4
Alma 1–4
Utangulizi
Muda mfupi baada ya Alma kuwa mwamuzi mkuu, mtu aitwaye Nehori alianza kufundisha mafundisho ya uongo na kuleta ukuhani wa uongo miongoni mwa Wanefi. Alimwua mtu mwenye haki na akauliwa kwa uhalifu wake. Miaka kadha baadaye, Amlisi alijaribu bila mafanikio kuwa mfalme juu ya Wanefi. Wakati watu walipopiga kura ya kumkataa kama mfalme, aliwakusanya wafuasi wake —waitwao waamlisi — ili kwenda vitani dhidi ya Wanefi. Wanefi walishinda, lakini makumi ya maelfu ya watu waliuawa. Kunyenyekezwa kwa ajili ya vita, Wanefi wengi walikumbuka wajibu wao, na maelfu wakajiunga na Kanisa. Hata hivyo, katika mwaka mmoja, washiriki wengi wa Kanisa walikuwa tayari na kiburi na walikuwa wakiwatesa wengine. Alma aliamua kuachana na majukumu yake kama mwamuzi mkuu na kulenga kutoa ushuhuda wa injili ya Yesu Kristo.
Alma 1
Waumini wa Kanisa wanafanikiwa licha ya kuenea kwa ukuhani wa uongo na mateso
Watu wakati mwingine hutafuta kuwa maarufu Chukua muda kidogo kufikiri juu ya hatari za wazi za tamaa hii. Ni nini hutokea iwapo utajali zaidi kuhusu yale marafiki zako wanafikiria juu yako kuliko yale Mungu anafikiria juu yako?
Kama ilivyoandikwa katika Alma 1, mtu aitwaye Nehori akawa maarufu sana miongoni mwa baadhi ya watu. Soma Alma 1:2–6, na utambue kile Nehori alifundisha na jinsi watu walivyoitikia hilo.
Tafuta mistari ya kwanza ya Alma 1:12 kwa neno Alma iliotumika kuelezea kile Nehori aliwaletea Wanefi. Kisha angalia tanbihi 12a. Soma 2 Nefi 26:29, marejeo ya kwanza kilichotajwa katika tanbihi, na utambue kile wale wanaotenda ukuhani wa uongo hufanya na wasichofanya.
Ukuhani wa uongo ni wakati watu wanahubiri “mafundisho ya uwongo… ili wapate utajiri na heshima” na “kujiinua wawe nuru ya ulimwengu” (Alma 1:16; 2 Nefi 26:29). Hawataki kujenga ufalme wa Mungu kwa mahubiri yao. Badala yake, wao wanataka kupokea faida (kama vile mali, faida ya kijamii, au nguvu juu ya wengine) na sifa ya watu wengine. Wanataka kuweka mtazamo kwao wenyewe, si kwa Mungu na injili Yake. Ukuhani wa uongo ni dhambi kubwa katika macho ya Mungu, kama vile Alma alivyoweka wazi alipomwambia Nehori, “Na kama ukuhani wa uongo utalazimshwa miongoni mwa watu hawa utathibitisha maangamizo yao kabisa” (Alma 1:12).
Nehori alipojaribu “kuwapotosha watu wa kanisa,” mtu mwenye haki aitwaye Gideoni “alimpinga na kumwonya kwa maneno ya Mungu” (Alma 1:7). Kujibu, Nehori akauchomoa upanga wake, akamuua Gideoni. Nehori alihukumiwa kwa makosa yake na akauawa. Soma Alma 1:16 ili kugundua ikiwa kifo cha Nehori kilimaliza ukuhani wa uongo miongoni mwa Wanefi.
Soma Alma 1:26–27, na utambue njia ambazo kwazo makuhani Wanefi wa Mungu walitenda tofauti na Nehori na wengine waliofanya ukuhani wa uongo.
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi makuhani Wanefi walivyotenda. Jinsi gani matendo ya makuhani Wanefi yalikuwa tofauti na matendo ya wale waliotenda ukuhani wa uongo?
Ukuhani wa uongo ulipoenea kote katika nchi, watu wengi walianza kuwatesa waumini waaminifu wa Kanisa. Ili kujiandaa kusoma sehemu yote ya Alma 1, fikiria jinsi umeona watu wengine wakiwaudhi, kudhihaki, au kuwatesa wale wanaozishika amri za Mungu.
Soma Alma 1:19–20, na uangalie ni kwa nini baadhi ya watu waliwatesa washiriki wa Kanisa. Alma 1:21–31 inaeleza jinsi washiriki wa Kanisa walivyofanya juu ya mateso hayo. Soma vifungu vya maandiko hapa chini na ujaze chati:
Washiriki wengine walijibu vipi kwa mateso hayo? |
Waumini wengine wa Kanisa waliishi vipi licha ya mateso hayo? |
Matokeo ya matendo yao ilikuwa nini? |
Ni baraka gani walizopokea? |
Andika kanuni uliojifunza kutokana na kusoma chati hii:
Mojawapo ya kanuni ungeweza kutambua ni:Tunapoishi injili, tunaweza kuwa na amani katika maisha yetu, hata kama tunateswa
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea jinsi kuelewa kanuni hiyo ya injili inaweza kukusaidia unapokabiliwa na mateso au shinikizo la kutotii amri. Kisha jibu mojawapo ya maswali yafuatayo:
-
Ni lini uliwahi kutii amri licha ya mateso au shinikizo la kutofanya hivyo, na ni baraka gani ulipokea?
-
Utakabiliana vipi na adui zako?
-
Alma 2
Waamlisi na Walamani waliungana katika vita dhidi ya Wanefi
Alma 2 inaelezea kuhusu majaribio zaidi kwa Wanefi. Soma utangulizi wa sura ili kujua jinsi mtu mmoja aitwaye Amlisi na wafuasi wake walivyowapinga Wanefi. Amlisi alitaka kuwa mfalme juu ya Wanefi, lakini Wanefi walipiga kura na kuchagua kumkataa na kuendelea na mfumo wao wa waamuzi. Wafuasi wa Amlisi walikusanyika pamoja na kumfanya mfalme wao. Amlisi aliwaamuru wafuasi wake kwenda vitani na Wanefi, na mara baadaye Walamani walijiunga na Waamlisi ili kuwapigaWanefi.
Kwa sababu Wanefi walikuwa waaminifu kwa Bwana, Bwana aliwasaidia katika vita vyao na Waamlisi na Walamani. Soma Alma 2:18, 28–31, 36, na uweke alama manenoimarishana kuimarisha kila wakati yanapoonekana. Angalia jinsi Bwana aliwaimarisha Wanefi.
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu wakati ulipohisi kuwa Bwana alikutia nguvu ulipojaribu kufanya kile ambacho ni sahihi.
Alma 3
Waamlisi walijitenga kutoka kwa Mungu
Fikiria kuhusu jumbe ambazo baadhi ya watu wanaweza kujaribu kutuma kuhusu wao wenyewe kupitia uchaguzi wao wa mavazi, mtindo wa nywele, hereni na mapambo ya vito, michoro, na kuchoma mwili.
Soma Alma 3:4, na utambue jinsi Waamlisi walivyobadilisha sura zao
Waamlisi walikuwa “wanatofautishwa” na nani?
Walitaka kufanana na nani?
Mabadiliko ya sura ya Waamlisi’ ilikuwa ni dhihirisho ya uasi wao. Kama ilivyandikwa katika Alma 3, Mormoni alitukumbusha juu ya laana na alama ambayo ilikuwa juu ya Walamani mamia ya miaka ya awali kwa sababu ya uasi wao dhidi ya Mungu (ona Alma 3:6–10; ona pia 2 Nefi 5:20–24). Waamlisi waliweka alama kwa hiari katika vipaji vyao, lakini hizi alama zilikuwa na kusudi ambalo lilifanana na alama ambayo Bwana aliweka kwa Walamani.
Weka alama kishazi katika Alma 3:18 ambacho kinaelezea tabia ya Waamlisi mbele ya Mungu. Pia weka alama katika Alma 3:19 kile ambacho Waamlisi walijiletea juu yao kwa sababu ya uasi wao.
Ni nini unajifunza kutoka Alma 3:18–19 kuhusu wale ambao wamelaaniwa na Bwana? (Wale ambao wanamwasi Mungu waziwazi hujiletea laana juu yao wenyewe.) Ni muhimu kuelewa kwamba laana ilikuwa hali ya “kutolewa kwenye uwepo wa Bwana” (2 Nephi 5:20). Kupitia kwa matendo yao, Waamlisi walikuwa wamejitenga kutoka kwa Mungu.
Kutokana na mfano wa Waamlisi, tunajifunza kwamba ni uchaguzi wetu kujitenga wenyewe kutoka kwa Mungu. Wale ambao “wamemwasi Mungu waziwazi” (Alma 3:18) wanajitoa kwenye uwepo wa Mungu, au kwa maneno mengine, wanajiteremshia laana kwao wenyewe.
-
Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Tofauti na Waamlisi, unaweza kufanya nini katika maisha yako sasa ili kuhakikisha kwamba hujajitoa kwenye uwepo wa Mungu?
Alma 3:20–25 inaeleza jinsi Wanefi waliwashinda Walamani katika vita vingine, lakini watu wengi kutoka pande zote mbili waliuawa. Soma Alma 3:26–27, ukitafuta somo kuu ambalo Mormoni alitaka tujifunze kutoka kwa maisha ya Waamlisi na vita kati ya Wanefi na Walamani.
Kamilisha kanuni ifuatayo kulingana na kile umesoma katika Alma 3:26–27: Tunapokea furaha au huzuni kulingana na
Chukua muda ili kufikiria juu ya yule ambaye umechagua kufuata katika maisha yako. Tafakari juu ya maswali yafuatayo: Ni aina gani ya malipo, au mishahara, ambayo Shetani huwatolea wale wanaomfuata? (Mara nyingi inavutia kwa mara ya kwanza, lakini hatimaye itasababisha huzuni na ulevi.) Kwa kulinganisha, ni mishahara gani uliopokea kutoka kwa Bwana kwa kuchagua kumfuata?
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu wakati ambapo kumfuata Bwana kulikuletea furaha.
Alma 4
Baada ya kipindi cha ukuaji wa Kanisa, waumini wa Kanisa wakawa na kiburi naye Alma akajiuzulu kama mwamuzi mkuu ili kuwaita wao kwenye toba.
Kufuatia vita na Walamani na Waamlisi, Wanefi “walikumbushwa jukumu lao,” na “wakaanza kuimarisha kanisa sana” (Alma 4:3–4). Kama matokeo, karibu watu 3,500 walijiunga na Kanisa (ona Alma 4:5). Kwa bahati mbaya, katika muda mfupi wa mwaka, wengi wa watu katika Kanisa walianza kuwa na kiburi. Soma Alma 4:8–12, na utambue matendo maovu ambayo yalitokea kwa sababu ya kiburi miongoni mwa washiriki wa Kanisa. Kanuni tunayoweza kujifunza kutoka katika kifungu hiki cha maandiko ni: Tukiweka mfano mbaya, matendo yetu yanaweza kuzuia wengine kukubali injili.(Ona Alma 4:10.)
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika mfano mmoja wa kitendo kiovu au tabia iliyoonyeshwa na Wanefi katikaAlma 4:8–12. Elezea ni kwa nini ni muhimu kuepuka kitendo hicho au tabia hio kama mshiriki wa Kanisa leo.
Kama matokeo ya uovu katika Kanisa, Alma alimteua mtu mwingine ili kuchukua nafasi yake kama mwamuzi mkuu ili aweze kujitolea wakati wake wote kwa wito wake kama kuhani mkuu wa Kanisa na kusaidia washiriki kushinda kiburi chao na dhambi zao kwa “kuwashawishi ushuhuda halisi” (Alma 4:19). Soma Alma 4:19, na uweke mstari chini ya kile Alma alitamani kufanya ili kuwasaidia watu wake.
Alma 4:19 inaonyesha kanuni hizi: Kutimiza wajibu wetu wa kiroho kunaweza kuhitaji dhabihu. Watumishi wa Bwana wanatoa ushuhuda na kuwaita wenye dhambi kutubu. Kutoa ushahidi msafi huwasaidia wengine kumkaribia Mungu.
Unaweza kufikiria mtu anayekataa cheo muhimu cha kisiasa, kama vile kuwa rais wa nchi, ili kutumikia misheni? Alma alifanya hivyo!
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile unafikiri kishazi “kuwashawishi ushuhuda halisi” (Alma 4:19) kinashawishi kuhusu jinsi Alma angefundisha. Pia andika jinsi umevutiwa kubadili au kuboresha kwa kusikia mtu mwingine akitoa ushuhuda wa injili.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza Alma 1–4 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: