Seminari
Kitengo cha19: Siku ya 4, Alma 38


Kitengo cha 19: Siku ya 4

Alma 38

Utangulizi

Shibloni Mwanawe Alma alihudumu pamoja naye kama mmisionari kwa Wazoramu. Kufuatia utume huu, Alma alionyesha shangwe kwa bidii na uaminifu ulionyeshwa na Shibloni wakati akipitia mateso miongoni mwa Wazoramu. Alma alimshuhudia Shibloni juu ya uwezo wa Yesu Kristo wa ukombozi na kumshauri kuendelea kufundisha injili.

Alma 38:1–3

Alma anaonyesha shangwe kwa uaminifu wa Shibloni

Chukua dakika moja kufikiri juu ya wakati ambapo wazazi wako walihisi shangwe kwa sababu ya uamuzi mwema ambao wewe au mshiriki mwengine wa familia alifanya au kwa sababu ya jinsi unavyoishi maisha yako.

familia katika meza ya chakula

SomaAlma 38:1–3, na uangalie vishazi vinavyoelezea jinsi Alma alivyohisi kuhusu Shibloni na kwa nini. Andika baadhi ya vishazi ulipata:

Kutoka kwa mistari hii tunajifunza kanuni hii: Tunapoanza katika ujana wetu kuwa na uthabiti na uaminifu katika kushika amri, tunaweza kuleta shangwe kuu kwa wazazi wetu

  1. ikoni ya shajaraChukua muda mchache kuuliza mmoja wa wazazi wako, walezi, au viongozi wa Kanisa jinsi maamuzi yako mazuri yanamuathiri. Andika majibu yao katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

Alma 38:4–9

Alma anashuhudia juu ya uwezo wa Mwokozi wa kukomboa

Alma alimkumbusha Shibloni kwamba wote walikuwa wameona uwezo wa Mwokozi wa ukombozi, ingawa kwa njia tofauti. Soma Alma 38:4–8, na ukamilishe chati ilioko chini. Pia tumia kile unajua kuhusu Shibloni kutoka Alma 38:2–3 na yale uliyojifunza kuhusu Alma kutoka sura ingine katika Kitabu cha Mormoni ili kukusaidia kukamilisha chati.

Shibloni (Alma 38:2–5)

Alma (Alma 38:6–8)

Alikombolewa kutoka kwa nini?

Alipokea baraka ya ukombozi kwa jinsi gani?

Kutokana na matukio ya Shibloni, tunaweza kujifunza: Tukistahimili mambo yote kwa uvumilivu na imani katika Mungu, Atatuokoa kutokana na majaribio, matatizo, na mateso na kutuinua juu siku ya mwisho. Kutokana na matukio ya Alma pia tunajifunza: Ili kupokea ondoleo la dhambi zetu na kupata amani kwa nafsi zetu, ni lazima tutumie imani katika Yesu Kristo na kutafuta rehema Yake.

Sanamu ya Kristo
  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Unajifunza nini kutoka kwa maelezo ya Shibloni na Alma juu ya uwezo wa Mwokozi wakukuponya?

    2. Chagua mojawapo wa kanuni ulioonyeshwa kwa msisitizo katika aya iliyotangulia, na uandike sentensi chache juu ya jinsi unaweza kutumia kanuni hiyo katika maisha yako.

SomaAlma 38:9, na uangalie kile ambacho Alma alitaka Shibloni kujifunza. Unaweza kutaka kukiweka alama kishazi katika mstari huu ambacho unahisi kinaelezea kile Alma alitaka mtoto wake kuelewa.

Fikiria juu ya wakati ambapo uwezo wa Mwokozi ulikukomboa kutokana na majaribu, taabu, au fedheha. Ulifanya nini kutafuta ukombozi huo? Je! Una majaribio au dhambi katika maisha yako sasa? Unawezaje kumgeukia Mwokozi kwa ajili ya ukombozi?

  1. ikoni ya shajaraJibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni kwa nini unafikiri ni muhimu kwako kujua kuwa “njia au mbinu” pekee kwa ambayo unaweza kuokolewa ni kupitia kwa Mwokozi? (ona Alma 38:9).

Alma 38:10–15

Alma anamshauri Shibloni kuendelea kukuza sifa za haki

Fikiria juu ya mwalimu au kiongozi wa Kanisa ambaye amekuwa na ushawishi bayana juu ya maisha yako. Fikiria sifa katika mtu huyo ambazo unatamani.

Kama ilivyoandikwa katika Alma 38:10–15, Alma alihimiza Shibloni kuendelea kukuza sifa ambazo zingemsaidia alipoendelea kufundisha injili na kuwatumikia wengine. Ushauri ambao Alma alimpa Shibloni unaweza kutumika kwa mtu yeyote ambaye anataka kuwashawishi wengine kwa wema kupitia kwa huduma, mafundisho, na kwa njia nyingine. Jifunze Alma 38:10–15, na utambue ushauri wowote ambao unahisi unaweza kusaidia hasa kwako. Unaweza kutaka kuweka alama yale unayopata.

  1. ikoni ya shajaraHapo chini ni mwongozo wa masomo ili kukusaidia kuelewa zaidi na kutumia ushauri wa Alma kwa mwanawe Shibloni (ona Alma 38:10–15). Kutoka safu ya kushoto chagua sehemu mbili au tatu za ushauri wa Alma ambazo unahisi zitakuwa ya thamani zaidi kwako. Kamilisha shughuli zinazohusiana za kujifunza katika safu ya kulia. Andika majibu yako katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

    Alma 38:10–12 Mwongozo wa Masomo

    Ushauri wa Alma

    Shughuli za Kujifunza

    “Uwe na bidii na kiasi kwa vitu vyote” (Alma 38:10).

    Mtu mwenye bidii huweka nguvu thabiti na juhudi katika shughuli za maisha. Mtu ambaye ni wastani hutumia kiasi katika vitu vyote na hutumia kujitawala. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini sifa hizi mbili zinahitajika unapowahudumia wengine. Andika jinsi unaweza kuwa na bidii au wastani katika eneo moja au zaidi la maisha yako na jinsi kufanya hivyo kunaweza kukusaidia kuwatumikia wengine kwa ufanisi zaidi.

    “Hakikisha kwamba hujuinui kwa kiburi; ndio, angalia kwamba hujisifu kwa hekima” (Alma 38:11).

    Kiburi, katika maandiko, ni wakati mtu anapoweka uaminifu mkuu kwake mwenyewe kuliko Mungu. Pia ina maana kwamba mtu anadhani yeye ni bora kuliko wengine. Kinyume cha kiburi hiki kisichokuwa cha haki ni unyenyekevu. Wale walio wanyenyekevu hujitahidi kufikiria juu ya wengine kwa njia ile wanavyojifikiria wenyewe, na wanampenda Mungu na kumweka wa kwanza katika maisha yao. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile kinaweza kutokea ikiwa muumini wa Kanisa alikuwa na kiburi na majivuno katika wito wake. Fikiria juu ya wito wako wa Kanisa au nafasi nyingine uliyonayo ili kuhudumu. Andika njia moja au mbili utakazotafuta ili kuwa mnyenyekevu na kuepukana na kiburi au majivuno unapohudumu.

    “Tumia ujasiri, lakini usiwe mjeuri” (Alma 38:12).

    Kuwa mjasiri inamaanisha kuwa na imani kwamba Mungu yu pamoja nasi na anaweza kutusaidia kutenda bila hofu katika huduma Yake. Kuwa mjeuri inaweza kumaanisha kushinikiza imani yetu au mitazamo kwa wengine bila ya kuwa msikivu kwa mahitaji na hisia zao. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini unafikiri Bwana angetaka tuwe na ujasiri. Pia andika njia mahususi ambayo unaweza kutumia ushauri wa kutumia ujasiri lakini sio ujeuri unapotafuta kuwatumikia wengine.

    “Zuia tamaa zako zote” (Alma 38:12).

    Kuzuia inamaanisha kuongoza au kutawala. tamaa ni hisia kali. Tafakari maswali yafuatayo na uandike majibu yako katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni kwa nini unafikiri ni muhimu kwetu kuzuia tamaa zetu —kwa maneno mengine, kuongoza au kutawala hisia zetu kali? Ni kwa jinsi gani unafikiri kuzuia tamaa zako kunaweza kukusaidia kujazwa na upendo? Utafanya nini ili kufuata ushauri wa Alma wa kuzuia tamaa zako zote?

    “Uepuke kutokana na uvivu” (Alma 38:12).

    Tafuta “Vivu, Uvivu” ” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.lds.org) au “Uvivu, Vivu, mvivu” katika Mwongozo wa Mada ili ujifunze zaidi kuhusu kinachomaanisha kuwa mvivu. Chagua mistari miwili iliyoorodheshwa chini ya mada hiyo, na uisome. Andika kile ulichojifunza kutoka kwa mistari hizi katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Andika jinsi ushauri wa kuepukana na uvivu utakusaidia kuwatumikia wengine kwa ufanisi zaidi. Hatimaye, andika njia mahususi ambayo kwayo utatafuta kuepukana na uvivu.

Ushauri wa Alma kwake Shibloni katika Alma 38:10–15 unafundisha kanuni hii: Kukuza sifa za haki hutuandaa kufundisha na kuwatumikia wengine. Tafakari jinsi kukuza sifa za haki unazosoma katikaAlma 38 kunaweza kubariki maisha yako na maisha ya wale walio karibu nawe.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 38 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: