Seminari
Kitengo cha 20: Siku ya 1, Alma 39


Kitengo cha 20: Siku ya 1

Alma 39

Utangulizi

Alma alimshtumu mwanawe mpotevu, Koriantoni, ambaye alikuwa amewacha huduma na kufanya dhambi mbaya ya ngono . Alma alimfundisha Koriantoni uzito wa matendo yake na kuonyesha maudhiko yake kwamba Koriantoni alikuwa na hatia ya makosa mazito vile. Alma aliaamuru Koriantoni kuacha kufuata “tamaa ya macho yake” na kutubu (Alma 39:9). Ujumbe wa Alma kwa Koriantoni unapatikana katika Alma 39–42.

Alma 39:1–6

Alma anaelezea uzito wa dhambi ya ngono kwa mwanawe Koriantoni

Fikiria maelezo yafuatayo: Dhambi zingine ni mbaya zaidi kuliko dhambi nyingine.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Je, unakubali kwamba dhambi zingine ni mbaya zaidi kuliko dhambi zingine? Kwa nini au kwa nini sivyo?

Kama ilivyoandikwa katika Alma 39, Alma alitoa ushauri kwa mwanawe Koriantoni ambao unaweza kukusaidia kuelewa hali nzito ya dhambi fulani. Koriantoni aliambatana na Alma na ndugu yake Shibloni katika ziara ya kuhubiri injili kwa Wazoramu. Akiwa huko, Koriantoni alifanya dhambi mbaya ya ngono.

SomaAlma 39:1–4, na uangalie kile Koriantoni alikosea. Ili kukusaidia kuelewa mistari hii, inaweza kuwa na manufaa kujua kwamba kahaba ni mwanamke msherati au malaya. Ni muhimu kuelewa kwamba “Bwana hawezi kuiangalia dhambi na kuivumilia hata kidogo” (M&M 1:31); dhambi za ngono hasa ni mbaya zaidi. Tambua pia kwamba Koriantoni aliacha kwa makusudi huduma yake na kwenda kumtafuta kahaba Isabeli, ambayo ilichangia kwa uzito wa dhambi zake.

Soma Alma 39:5, na uangalie jinsi Alma alivyoelezea uzito wa dhambi ya ngono ikilinganishwa na dhambi nyinginezo. Chukizo ni kitu ambacho ni cha dhambi, uovu, au ubovu. Kutoka kwa mistari hii tunajifunza kwamba dhambi ya ngono ni machukizo mbele za Bwana. Tafakari ni kwa nini unafikiri dhambi ya ngono imewekwa karibu na mauaji kwa uzito.

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitoa maelezo haya kuhusu ni kwa nini dhambi ya ngono ni machukizo mbele ya Bwana: “Kwa kuweka uzito kama huo kwa hamu ya kimwili inayotolewa kote ulimwenguni, ni nini ambacho Mungu anajaribu kutuambia kuhusu nafasi yake katika mpango Wake kwa wanaume na wanawake wote? Nawaambieni kuwa Anafanya hivyo —kuzungumza juu ya mpango huo wa maisha yenyewe. Wazi wazi miongoni mwa shauku Yake kubwa kuhusu maisha ni jinsi mtu anavyoingia katika dunia hii na jinsi mtu anavyotoka nje yake. Ameweka mipaka kali sana katika masuala haya” (“Personal Purity,” Ensign, Nov. 1998, 76).

Soma mistari ifuatayo, na uangalie na uweke alama majibu ya maswali yafuatayo: Ni baadhi baraka zipi zilizopo kwa kubakia wasafi kimaadili?

“Urafiki wa kimwili kati ya mume na mke ni mzuri na mtakatifu. Imetakaswa na Mungu kwa uumbaji wa watoto na kwa udhihirisho wa upendo kati ya mume na mke. Mungu ameamrisha kuwa urafiki wa kujamiiana uhifadhiwe kwa ajili ya ndoa.

“Unapokuwa msafi kimaadili, unajiandaa kufanya na kushika maagano matakatifu katika hekalu. Unajitayarisha kujenga ndoa imara na kuleta watoto ulimwenguni kama sehemu ya familia ya milele na familia ya upendo. Unajikinga kutokana na uharibifu wa kiroho na kihisia ambao huja kwa kushiriki urafiki wa kujamiiana nje ya ndoa. Unajikinga pia dhidi ya magonjwa hatari. Kubakia msafi kimaadili hukusaidia kuwa na ujasiri na furaha ya kweli na huboresha uwezo wako wa kufanya maamuzi mazuri kwa sasa na baadaye” (For the Strength of Youth [booklet, 2011], 35).

Sasa soma mistari ifuatayo, ukitafuta majibu ya maswali yafuatayo: Viwango vya Bwana ni vipi vya kubakia msafi kimaadili?

“Kiwango cha Bwana kuhusu usafi wa kimaadili ni wazi na hakibadiliki. Usiwe na uhusiano wowote wa ngono kabla ya ndoa, na uwe mwaminifu kabisa kwa mwenzi wako baada ya ndoa. Usiruhusu vyombo vya habari, rika lako, au watu wengine kukushawishi kuwa urafiki wa kujamiiana kabla ya ndoa unakubalika. Hairuhusiwi Mbele za Mungu, dhambi za ngono ni nzito mno. Zinachafua mamlaka takatifu ambayo Mungu ametupa ili kuumba uhai. Nabii Alma alifundisha kwamba dhambi za ngono ni mbaya zaidi kuliko dhambi zingine zozote isipokuwa mauaji au kumkana Roho Mtakatifu (ona Alma 39:5).

“Kamwe usifanye kitu chochote kinachoweza kusababisha uvunjaji wa kimaadili. Tendea wengine kwa heshima, si kama vitu vinavyotumika kutimiza tamaa mbaya na ubinafsi. Kabla ya ndoa, usishiriki katika busu la kimapenzi, kulala juu ya mtu mwingine, au kugusa sehemu za siri, sehemu takatifu za mwili wa mtu mwingine, ukiwa na au bila nguo. Usifanye kitu kitakachoamsha hisia za ashiki. Usiamshe hisia hizo katika mwili wako mwenyewe. Kuwa msikivu kwa maongozi ya Roho ili uweze kuwa msafi na mwema. Roho wa Bwana atajiondoa kwa yule ambaye yumo katika uvunjaji wa kimaadili.

“Epuka hali zinazoalika majaribu mengi, kama vile shughuli za usiku au usiku kucha mbali na nyumbani au shughuli zisizokuwa na usimamizi wa watu wazima. Usishiriki katika majadiliano au mawasiliano yoyote yanayoamsha hisia za kiashiki. Usishiriki katika aina yoyote ya picha za ngono. Roho anaweza kukusaidia kujua wakati upo katika hatari na kukupa nguvu ya kujiondoa kutoka kwa hali hiyo. Kuwa na imani katika na uwe mtiifu kwa ushauri wa haki wa wazazi na viongozi wako.

“Tabia ya ushoga na usagaji ni dhambi kubwa. Ukijipata ukikabiliwa na kivutio hicho cha jinsia au unashawishi wa kushiriki katika tabia zisizofaa, tafuta ushauri kutoka kwa wazazi na Askofu wako. Wao watakusaidia.

“Waathiriwa wa unyanyasaji wa kimapenzi hawana hatia ya dhambi na hawahitaji kutubu. Ikiwa umekuwa mwathiriwa wa unyanyasaji, jua kwamba hauna hatia na kwamba Mungu anakupenda. Zungumza na wazazi wako au mtu mwingine mzima anaye aminiwa, na utafute ushauri wa Askofu wako mara moja. Wanaweza kukusaidia kiroho na kukusaidia katika kupata ulinzi na msaada unaohitaji. Mchakato wa uponyaji unaweza kuchukua muda. Tumaini katika Mwokozi. Atakuponya na kukupa amani.

“Kama umejaribiwa kufanya aina yoyote ya dhambi ya kujamiiana, tafuta usaidizi kutoka kwa wazazi na Askofu wako. Omba kwa Baba yako wa Mbinguni, ambaye atakusaidia kukinza majaribu na kuyashinda mawazo na hisia zisiozofaa. Kama umetenda dhambi ya kujamiiana, zungumza na Askofu wako sasa na uanze mchakato wa toba ili uweze kupata amani na uwe na urafiki kamili wa Roho.

“Fanya uamuzi wa kibinafsi ili kuwa msafi kimaadili. Kwa maneno na matendo yako, wahimize wengine kufanya vivyo hivyo” (For the Strength of Youth, 35–37).

Tafakari ni ujumbe gani unahisi Bwana angetaka uzingatie kutokana na kile umesoma.

Alma 39:7–19

Alma anamhimiza Koriantoni kutubu

Fikiria kuwa na mazungumzo na wazazi wako, viongozi wa Wasichana au Vijana, au askofu wako au rais tawi juu ya umuhimu wa usafi wa kimaadili. Fikiria jinsi unavyoweza kuitikia wazazi wako au viongozi wa Kanisa wanapokushauri kuhusu umuhimu wa kubakia msafi kimaadili. Soma Alma 39:7–8 ili kujua madhumuni ya Alma yalikuwa nini katika kufundisha Koriantoni kuhusu uzito wa dhambi zake. Tafakari jinsi majibu yako kwa ushauri wa wazazi wako au viongozi wa Kanisa ungeathiriwa kwa kujua ulikuwa ni mwaliko wa upendo kubakia msafi au kutubu na kuepuka hukumu ya Mungu.

Picha
Mzee D. Todd Christofferson

Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi Mitume Kumi na Wawili alieleza ni kwa nini wazazi, kama Alma, hualika watoto wao kutubu “mwaliko wa kutubu ni onyesho la upendo. Kama hatuwezi kualika wengine kubadilika au kama hatuwezi kudai toba yetu wenyewe, tunaanguka katika wajibu wa kimsingi tunaowia mmoja kwa mwingine na kwetu sisi wenyewe. Mzazi mwenye uhuru, rafiki msahemevu, kiongozi wa Kanisa mwoga hakika wanajali kuhusu wao wenyewe kuliko ustawi na furaha ya wale ambao wangeweza kusaidia. Ndiyo, mwito wa toba nyakati nyingine huonekana kama haivumiliki au wa kukera na huweza hata kuchukiwa, lakini ikiongozwa na Roho, hakika ni kitendo cha uangalifu halisi” (“The Divine Gift of Repentance,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 39).

  1. Andika yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Toba inajumuisha … Kisha, unapojifunza Alma 39:9–14, tengeneza orodha katika shajara yako ya kujifunza maandiko juu ya kile Alma alimfundisha Koriantoni kuhusu toba ambacho kinaweza kusaidia kukamilisha taarifa hii.

Tumia maswali yafuatayo na ufafanuzi ili kukusaidia kuelewa na kutumia ushauri wa Alma. Jaribu kutambua na kuandika angalau ukweli mmoja kwa kila mstari uliyoorodheshwa hapa chini ambao unaweza kusaidia kukamilisha taarifa katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Hauna haja ya kujibu maswali katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

Soma Alma 39:9. (Alma 39:9 ni mstari wa umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kuweka alama katika njia tofauti ili uweze kuupata katika siku zijazo.) Ni nini vishazi “usiende tena kupendeza tamaa ya macho yako” na “ujikataze mwenyewe kwa vitu hivi vyote” vinahusiana nacho na kuacha dhambi?

Katika siku zetu, kishazi “tamaa ya macho yako” kina matumizi ya nguvu kwa uasherati na picha au burudani yenye ngono kwa njia yoyote. Kishazi “ujikataze mwenyewe,” kama inavyotumika katika Alma 39:9, ina maana ya kujinyima mwenyewe kitu fulani. Kishazi hiki haijulikani sana kwetu leo. Hata hivyo, katika siku za Joseph Smith, maana kadhaa ya kitenzi ujikataze ilikuwa ni “kufuta; kukatisha. … Kukabiliana … ; kuacha” (Noah Webster’s First Edition of an American Dictionary of the English Language, facsimile ed. [1967]). Tukitumia ufafanuzi huu kwa yale Alma alikuwa akifundisha mtoto wake, tunaweza kuelewa umuhimu wa kuondoa hali zote za kutokufa (ikiwemo vyanzo vya majaribu ya uasherati ambao unatudhibiti) katika maisha yetu, ili tuweze “kurithi ufalme wa Mungu”. Je! Ni njia gani vijana Watakatifu wa Siku za Mwisho wanaweza kujichorea mstari wenyewe katika masuala ya usafi wa kimaadili na kuepuka kwenda kupendeza tamaa ya macho yao?

Soma Alma 39:10. Ni kwa jinsi gani kutafuta chakula cha kiroho—kutoka kwa wazazi, viongozi wa Kanisa, ndugu, au marafiki wa kuaminika—kunaweza kusaidia mtu kutubu?

Soma Alma 39:11–12, na utafakari maswali yafuatayo:

  • Ni nini kinapaswa kubadilika katika moyo wa mtu wakati wa mchakato wa toba ili asiweze kupotoshwa tena na ibilisi kutenda dhambi?

  • Ni kwa jinsi gani kuepuka ufuataji wa vitu potovu na vya kijinga kunamsaidia mtu kutubu?

Soma Alma 39:13. } Kumbuka kwamba Alma alimwambia Koriantoni kwamba wakati Wazoramu walipoona mwenendo wa Koriantoni hawangeamini maneno ya Alma (ona Alma 39:11). Inaweza kusaidia kuelewa kwamba katika maandiko, kishazi “kumgeukia Bwana” kinaashiria toba. Toba ni “kugeuka kwa moyo na mapenzi kwa Mungu” (Bible Dictionary, “Repentance”).

  • Unafikiri inamaanisha nini kutubu kwa “akili , uwezo, na nguvu zako zote”?

  • Wakati dhambi zetu zinawaathiri wengine, tunapaswa kufanya nini kama sehemu ya toba yetu?

  • Wakati dhambi nzito inapofanywa, kwa nini ni muhimu kutafuta usaidizi wa askofu au rais wa tawi?

Kutoka Alma 39:9–13 tunajifunza: Toba inajumuisha kutambua na kuacha dhambi zetu na kugeukia Bwana kwa akili, uwezo, na nguvu zetu zote

Tafakari yale unahisi Bwana angetaka ufanye ili kugeuza kikamilifu zaidi moyo wako na mapenzi Kwake. Unaweza kufanya nini leo ili kuanza kufuata maongozi haya?

Bila Yesu Kristo na Upatanisho Wake, isingekuwa rahisi kwako kusamehewa dhambi zako. Soma Alma 39:15–16, 19, na uangalie jinsi Alma alivyoeleza juu ya maarifa kwamba Yesu Kristo atakuja kuchukua dhambi za ulimwengu.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini kuja kwa Yesu Kristo ni habari njema kwa Koriantoni na kwako.

Picha
alama ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko—Alma 39:9

Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema yafuatayo kuhusu kukariri maandiko:

“Kujifunza, kutafari, kutafuta, na kukariri maandiko ni kama kujaza kabati la faili na marafiki, maadili, na kweli ambazo zinaweza kutumika wakati wowote, mahali popote duniani.

“Uwezo mkubwa unaweza kutokana na kukariri maandiko. Kukariri maandiko ni kujenga urafiki mpya. Ni kama kugundua mtu mpya ambaye anaweza kusaidia wakati wa mahitaji, kutoa uongozi na faraja, na kuwa chanzo cha motisha ya mabadiliko unaohitajika” (“The Power of Scripture,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 6).

  1. Jaribu kukaririAlma 39:9. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika sentensi moja au mbili kuhusu jinsi kukariri mstari huu kunaweza kuwa kinga kwako wakati wa majaribu.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 39na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha