Seminari
Kitengo cha 18: Siku ya 3, Alma 31


Kitengo cha 18: Siku ya 3

Alma 31

Utangulizi

Alma alijifunza kwamba kundi la wapinzani Wanefi wanaoitwa Wazoramu walikuwa wamepotea kutoka katika ukweli wa injili. Kusikitishwa na taarifa hizi za uovu, Alma alichukua wengine pamoja naye ili kufundisha Wazoramu neno la Mungu. Walishuhudia ibada za uasi na kiburi cha Wazoramu. Alma alisali kwa dhati kwamba yeye na wafuasi wake watapata faraja na mafanikio katika kuwaleta Wazoramu kwa Bwana.

Alma 31:1–7

Alma na wenzake wahubiri neno la Mungu kwa Wazoramu walioasi

Fikiria kwamba una rafiki au mwanafamilia ambaye anaanza kupotea kutoka kwa injili au ambaye haiishi injili kikamilifu kama vile anavyofaa. Fikiria kuhusu majibu ya kwa maswali yafuatayo:

  • Unaweza kufanya nini ili kusaidia mtu huyu kurudi Kanisani na kutamani kushika amri?

  • Ni nani ambaye utamwendea kwa msaada katika kukabiliana na matatizo na kutokuelewana kwa mtu huyu?

Somo hili linaonyesha jinsi Alma na wengine walijaribu kusaidia kundi la watu ambao walikuwa wamepotea kutoka kwa ukweli wa injili. Soma Alma 31:1–2. Ni kwa jinsi gani Alma alihisi aliposikia kuhusu yale Wazoramu walikuwa wakifanya?

Soma Alma 31:3–4, na ugundue ni kwa nini Wanefi walianza kuogopa kwa sababu ya vitendo vya Wazoramu.

Unapofikiri juu ya yale uliyojifunza wakati wa mafunzo yako ya Kitabu cha Mormoni, ni nini unafikiri kingeweza kusaidia kuhamasisha Wazoramu kutubu na kurudi katika ukweli wa injili? Soma Alma 31:5, na utambue kile Alma alijua ingekuwa njia bora zaidi ya kuwakomboa Wazoramu.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini unafikiri neno la Mungu lina nguvu zaidi katika kuwasaidia watu kubadilika kuliko kutumia nguvu au kitu kingine chochote.

Tafakari kauli ifuatayo kutoka kwa Rais Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, kuhusu nguvu ya neno la Mungu:

“Mafundisho kamili, yakieleweka, hubadilisha mtazamo na tabia.

Rais Boyd K. Packer

“Mafunzo ya mafundisho ya injili yataweza kuboresha tabia kwa upesi kuliko mafunzo ya tabia yanavyoweza kuboresha tabia. Mshughuliko na tabia isiyostahili inaweza kusababisha tabia isiyostahili. Hii ndio maana tunasisitiza kwa nguvu sana mafunzo ya mafundisho ya injili” (“Little Children,” Ensign, Nov. 1986, 17).

Kulingana na Alma 31:5 na kauli ya Rais Packer, kamilisha kanuni ifuatayo: Ninapojifunza neno la Mungu, litanielekeza kwenye .

Miongoni mwa uwezekano mwingine, unaweza kukamilisha kanuni hapo juu kwa njia hii: Ninapojifunza neno la Mungu, litanielekeza kufanya yaliyo sahihi.

  1. ikoni ya shajaraTafakari uzoefu wako kwa maandiko na kusikiliza neno la Mungu. Andika kuhusu wakati ambapo neno la Mungu lilipokuongoza wewe, familia, au marafiki zako kufanya yaliyo sahihi.

Alma 31:8–23

Wazoramu wanaomba na kuabudu kwa njia ya uongo.

Alma na wengine saba walikwenda kuhubiri neno la Mungu kwa Wazoramu. Walipofika, waliwaona Wazoramu wakiabudu Mungu katika njia ya kushangaza. Ni nini kinakuja akilini unapofikiri juu ya neno kuabudu?

Kuabudu kunalenga jinsi tunaonyesha upendo, uchaji, na kujitolea kwa Mungu. Kuabudu mara nyingi hujumuisha vitendo kama vile kusali, kufunga, na kuhudhuria ibada za kanisa. Hata hivyo, ibada ya kweli daima zinahusisha moyo. Soma Alma 31:8–11, na utambue na uwekee alama maneno na vishazi vinavyoelezea ibada ya Wazoramu.

Inaweza kusaidia kujua kwamba “heshima za kanisa” (Alma 31:10) zinahusiana na “ibada,” kama vile sadaka inayohitajika wakati huo kama sehemu ya sheria ya Musa au sakramenti katika siku zetu. Unaweza kutaka kuweka alama katika Alma 31:10 mojawapo ya sababu tunapaswa kuabudu na kusali kila siku.

familia ikisali

Fikiria kuandika kanuni hii katika pambizo ya maandiko yako karibu na Alma 31:9 {–11: Juhudi zetu za kila siku za kusali na kushika amri hutuimarisha dhidi ya majaribu.

Mzee Rulon G. Craven, wakati akihudumu kama mshiriki wa Sabini, alisisitiza umuhimu wa ibada ya binafsi ya kila siku kama kinga dhidi ya majaribu na makosa: “Katika miaka iliyopita nimeombwa mara kadha na Ndugu kukutana na waumini wanaotubu wa Kanisa na kuwahoji kwa ajili ya urejesho wa baraka zao za hekaluni. Hii daima imekuwa tukio la kiroho la kuvutia katika kurejesha baraka za watu wale wa ajabu ambao walitubu. Nimeliuliza baadhi yao swali, ‘Ni nini kilichotokea katika maisha yako kilichofanya upoteze ushiriki wako katika Kanisa?’ Kwa macho yaliyojawa na majonzi walijibu: ‘Sikutii kanuni za msingi za injili: sala, kuhudhuria kanisa mara kwa mara, kuhudumu katika kanisa na kujifunza Injili. Kisha nikajiingiza katika majaribu na kupoteza uongozi wa Roho Mtakatifu (“Temptation,” Ensign, May 1996, 76).

Ni kwa jinsi gani kauli ya Mzee Craven inaunga mkono ukweli unaopatikana katika Alma 31:9–11?

Soma Alma 31:12–23, na ufikirie jinsi ingekuwaje kuwasikia Wazoramu wakiomba kutoka kwa mnara wao. Fikiria kuhusu majibu ya maswali yafuatayo:

  • Ni wasiwasi gani ungekuwa nayo ukisikia mtu akiomba kwa njia hii?

  • Ni mafundisho gani ya uongo Wazoramu walikariri katika maombi yao?

  • Mtazamo wao ulikuwa upi dhidi ya watu wengine? (Tambua ni mara ngapi maneno sisi na sisi inaonekana katika sala za Wazoramu’.)

Baada ya kila mtu kurudia sala sawa, “walirejea kwao, bila kuzungumza maneno ya Mungu wao tena hadi wakati wa kukusanyika tena kwenye kituo kitakatifu” (Alma 31:23).

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni baadhi ya hatari gani za kuabudu, kuomba, na kuongea na Mungu mara moja tu kwa wiki?

    2. Ni kwa njia gani tunaweza kumwabudu Mungu wiki yote?

Mtazamo wetu ni muhimu pia tunapoabudu. Soma maelezo yafuatayo kutoka kwa Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili juu ya jinsi tabia yetu huathiri ibada yetu:

“Ibada mara nyingi hujumuisha vitendo, lakini ibada ya kweli daima inahusisha tabia fulani ya akili.

Mzee Dallin H. Oaks

“Mtazamo wa kuabudu huhamasisha hisia ya ndani ya utii, kuabudu, na uchaji. Kuabudu kunachanganya upendo na uchaji katika hali ya ibada inayovuta roho zetu karibu na Mungu” (Pure in Heart [1988], 125).

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu jinsi unavyoamini unaendelea katika ibada yako, ikiwa ni pamoja na mtazamo wako, katika makundi yafuatayo: (a) sala ya binafsi ya kila siku, (b) mafunzo ya binafsi ya kila siku, (c) utii kwa amri, na (d) kuhudhuria mikutano ya kanisa na kushiriki sakramenti ya kila wiki. Weka lengo kuboresha ibada yako ya binafsi ya kila siku. Pia unaweza kutaka kumwambia mzazi, kiongozi, au rafiki kuhusu lengo lako ili aweze kukutia moyo katika wiki zijazo.

Alma 31:24–38

Alma anaomba kwa nguvu na mafanikio kwa wamisionari katika kuwaleta Wazoramu kwa Bwana.

Baada ya kushuhudia ibada ya uasi ya Wazoramu, Alma aliomba kwa Bwana. Soma Alma 31:30–35, na uangalie jinsi sala ya Alma ilitofautiana na sala za Wazoramu.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika yale umejifunza kuhusu jinsi ya kuomba kwa kulinganisha sala ya Alma pamoja na sala za Wazoramu. Pia andika jinsi mfano wa Alma wa sala ya haki unaweza kushawishi maombi yako binafsi.

Soma Alma 31:36–38, na uangalie baraka ambao zilimjia Alma na wenzake walipopokea baraka ya ukuhani na kuhubiri injili. Kumbuka kwamba kishazi “aliwapigia makofi wote waliokuwa pamoja naye” (Alma 30:36) inahusu kuwekea mikono.

Alma na uzoefu wa wenzake unatufundisha kanuni: Kama tutaomba na kutenda kwa imani, basi tutapokea msaada wa Mungu katika majaribu yetu.

Alma na wengine wanasali

Kufuatia maombi yake, Alma na wenzake walionyesha imani yao kwa kwenda kufanya kazi na kumtegemea Bwana kuwapa mahitaji yao walipomtumikia Yeye na watoto Wake. Angalia njia unayoweza kufuata mfano wa Alma wa kuomba kwa imani.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 31 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: