Seminari
Kitengo cha 18: Siku ya 1, Alma 25–29


Kitengo cha 18: Siku ya 1

Alma 25–29

Utangulizi

Baada ya miaka ya kuhubiri injili, Amoni alimsifu Bwana na kuonyesha shukrani kwa baraka ya kuwa chombo katika mikono Yake ya kuleta injili kwa Walamani. Walamani wengi walianza kuamini katika Bwana, kutubu, na kujiita Waanti-Nefi Lehi. Baada ya Waanti-Nefi-Lehi kufanya agano na Mungu ili kamwe kutochukua tena silaha za vita, Waamaleki na Walamani walianza kufanya maandalizi ya kwenda vitani dhidi yao. Ili kuwasaidia wao kuweka agano lao na Bwana,Waanti-Nefi-Lehi walikubali toleo la ulinzi kutoka kwa Wanefi. Alma nabii wa Wanefi alionyesha furaha aliyohisi kwa kuhubiri injili na kuwaalika wengine waje kwa Yesu Kristo.

Alma 25

Unabii wa Abinadi umetimia, na Walamani wengi wanaongoka.

Fikiria juu ya mabadiliko yoyote uliyofanya vile ulivyoongoka zaidi kwa injili ya Yesu Kristo. Alma 25 inaelezea juu ya utimiaji wa unabii wa Abinadi ya kwamba wazao wa makuhani wa Nuhu watawindwa na kuuawa na inaonyesha kuwa Bwana huwathibitisha manabii Wake na kutimiza unabii wao wenye maongozi (ona Alma 25:9). Pia inaelezea ni Walamani wangapi walitubu na kujiunga na Waanti-Nefi-Lehi. SomaAlma 25:14, na ubainishe yale hawa Walamani walifanya walivyoongoka kwa injili. Katika Alma 25:15 tunajifunza sababu mbili za kwa nini walishika sheria za Musa.

Alma 26

Amoni anafurahia katika rehema ya Bwana kwa Walamani na wana wa Mosia.

mfanyakazi  wa ujenzi akitumia chombo.

Inahitajika nini ili kujenga nyumba au kanisa? Ni aina gani ya kanisa ambayo fundi mwenye ujuzi anaweza kujenga akitumia zana au vyombo sahihi? Katika Alma 26, Amoni alijieleza na ndugu zake kama kuwa vyombo katika mikono ya Mungu vya kufanya kazi kubwa. Soma Alma 26:1–5, 12–13, na ubaini kile Bwana alikamilisha kwa kutumia Amoni na ndugu zake kama vyombo katika mikono Yake. (Unaweza kutaka kuweka alama majibu unayopata katika maandiko yako.) Katika mstari wa 5 kishazi “kusukuma pepeto” ina maana ya kufanya kazi kwa bidii, “miganda” yanawakilisha waongofu, “maghala” yanawakilisha Kanisa, na kishazi kwamba wale ambao wamekusanyika “hawajapotea” inahusu Mungu kuhifadhi waongofu na kuwapa uzima wa milele.

Tambua au weka alama kishazi kimoja au zaidi katika Alma 26:12 ambacho kinaonyesha kwamba Amoni alielewa kuwa alikuwa tu chombo katika mikono ya Bwana na ya kuwa ni Bwana ndiye aliyetimiza miujiza wakati wa utume wake.

Kutoka mistari hii tunajifunza kanuni hii: Tunapojiandaa na kujinyenyekeza, Bwana anatutia nguvu na kututumia kama chombo katika mikono Yake. Kanuni la kirafiki ambayo pia tunajifunza katika Alma 26 ni: Tunapata furaha tunapomtumikia Bwana na watoto Wake kwa uaminifu. Soma Alma 26:11, 13, 16, na uweke alama kila wakati unapoona neno furaha au kufurahi.

Soma Alma 26:13–16, na utambue sababu ambazo Amoni alitoa kwa kufurahi kwake.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini unafikiri tunapata furaha tunapokuwa katika huduma ya Bwana. Pia unaweza kutaka kuandika kuhusu wakati ulipohisi furaha kama matokeo ya huduma yako katika Kanisa.

Soma mistari ifuatayo, na ufikirie juu ya majibu kwa maswali yake yanayoandamana:

Alma 26:22–23, 26–29. Andika mahitaji yaliyotajwa ili kujua siri za Mungu. Ni ahadi gani iliyopeanwa kwa wamisionari ambao wana sifa hizi? Nini vikwazo gani ambavyo Amoni na ndugu zake walipitia katika huduma yao kwa Bwana na Walamani? Ni gani kati ya vikwazo hivi vinafafana na vikwazo vinavyowakabili wale wanaomtumikia Bwana leo? Wamisionari wa kisasa wanaweza kujifunza nini kutoka Alma 26:29 kuhusu mahali ambapo wanapaswa kufundisha injili?

Alma 26:30. Ni nini kilichowahimiza wana wa Mosia kuendelea kuhudumu hata wakati wa kipindi kigumu?

  1. ikoni ya shajaraSoma Alma 26:35–37, na ujibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kweli gani zilizofundishwa katika mistari hii ambazo zinaweza kukupatia sababu za kufurahi katika wema wa Mungu? (Unaweza kutaka kuweka alama vishazi vinavyoonyesha kweli hizi.)

    2. Kuna tofauti gani kwa kujua kwamba Mungu anakujali wewe?

Alma 27

Amoni anawaongoza watu wa Waanti-Nefi-Lehi kwa usalama miongoni mwa Wanefi.

Unapojiandaa kujifunza Alma 27, fikiria juu ya majibu kwa maswali yafuatayo:

  • Umewahi kupewa ahadi na mtu na kisha akaivunja ahadi ile?

  • Unamfahamu mtu yeyote aliyeendelea kuweka ahadi yake kwako?

  • Unahisi vipi kuhusu watu wanaotimiza ahadi zao? Kwa nini?

Kufuatia juhudi zao zisizozaa matunda za kuwaangamiza Wanefi, Walamani walijaribu kuwaangamiza wale Walamani (Waanti-Nefi-Lehi) ambao waligeuzwa na Amoni na ndugu zake. Kumbuka kwamba Waanti-Nefi-Lehi walizika silaha zao za vita ili kuonyesha kwamba wangeshika agano lao ili kamwe wasiue tena. Ili kujua jinsi Waanti-Nefi-Lehi walikuwa katika kuweka agano hilo, soma Alma 27:2–3.

Vita vya Walamani

Fikiria uwezo wa ahadi ya Waanti-Nefi-Lehi wa kuheshimu agano lao la kutochukua silaha walipokuwa wakishambuliwa. Fikiria jinsi unavyoweza kuimarisha ahadi yako kutii maagano yako na Baba wa Mbinguni wakati inapoonekana vigumu kufanya hivyo.

Kwa sababu ya mateso na mashambulizi kutoka Walamani waovu, Amoni aliwaongoza Waanti-Nefi Lehi kwenda Zarahemla —mji wa Wanefi —ambapo Wanefi waliahidi kuwalinda kutokana na maadui zao. Fikiria kile unaweza kufanya ili kuwasaidia wale walio karibu nawe kutii maagano walioweka na Bwana.

Wakati walipokuwa Zarahemla, Waanti-Nefi Lehi waliitwa watu wa Amoni na Wanefi. Soma Alma 27:27–30, ukiangalia yale watu wa Amoni walijulikana kwayo. Weka alama kwenye maneno yo yote au vishazi vinavyofundisha kanuni ifuatayo: Wakati tumeongoka kikamilifu kwa Bwana, tunaweka maagano tuliofanya Naye.

  1. ikoni ya shajaraJibu moja au yote ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni matukio gani uliyopata ilipokuwa vigumu kwako kutii maagano yako na Bwana, lakini bado uliendelea kuyatii?

    2. Ni nani ambaye amekuwa mfano kwako wa mtu ambaye ni mwaminifu na wa kweli kwa maagano yake kwa Bwana? Ni kwa jinsi gani mtu huyo ameonyesha uaminifu kwa ahadi hizo?

Alma 28

Wanefi wawashinda Walamani katika vita vikuu.

  1. ikoni ya shajaraFikiria kuwa wewe ni mwandishi wa habari aliyetumwa kufuatailia matukio yanayopatikana katikaAlma 28. Soma Alma 28:1–6, 11–14, na uandike aya fupi katika shajara yako ya kujifunza maandiko ukifanya muhtasari kile kilichotokea. Hakikisha unajibu maswali yafuatayo katika aya yako.

    1. Nini thamani gani Wanefi walilipa kwa ajili ya kuwasaidia watu wa Amoni kuweka maagano yao? (Ona Alma 28:1–3.)

    2. Ni kiasi gani vifo hivi viliwaathiri Wanefi? (Ona Alma 28:4–6.)

    3. Kwa nini baadhi ya watu walikuwa na hofu wakati wapendwa wao walikufa wakati wengine walifurahia na kuwa na matumaini? (Ona Alma 28:11–12.)

Andika maelezo muhimu kufupisha yale uliyojifunza kutoka Alma 28:11–12:

Mojawapo ya kanuni iliyofundishwa katika Alma 28 ni: Tunapokuwa na imani katika Yesu Kristo na ahadi Zake, tunaweza kuwa na matumaini na furaha licha ya kifo.

  1. ikoni ya shajaraJibu moja au yote ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni lini uliwahi kushuhudia mtu akipitia kifo chake mwenyewe au kifo cha mpendwa kwa matumaini kwa sababu ya imani katika Yesu Kristo?

    2. Ni kwa jinsi gani unaweza kuelezea kifo kwa mtu ili kumsaidia mtu huyo kuwa na matumaini baada ya kifo cha mpendwa?

Tambua maneno matatu ya Mormoni “na hivyo tunaona” katikaAlma 28:13–14. Unaweza kutaka kuweka alama katika maandiko yako. Ni mambo gani ambayo Mormoni anasisitiza anapohitimisha historia ya utume wa wana wa Mosia kwa Walamani? Tafakari ni kwa nini kweli hizi ni muhimu kwako kuzijua.

Alma 29

Alma anafurahia katika kuleta nafsi kwa Mungu

Je! Umewahi kutamani kuwa ungekuwa na uwezo wa kuleta peke yako baadhi ya mazuri makubwa au kusitisha baadhi ya maovu ya kutisha katika ulimwengu? Alma 29 kina maelezo ya Alma ya hamu yake ya kuwa chombo katika mikono ya Bwana. Pekua Alma 29:1–3, na uangalie hamu ya moyo wa Alma.

Alma Inuka

Kukumbuka kilichomfanyikia Alma kama kijana, fikiria ni kwa nini Alma alikuwa na hamu aliyoonyesha. Angalia katika Alma 29:3 kwa nini alijisikia kwamba alikuwa akikosa katika hamu yake. Soma Alma 29:4–5, na utambue kile Bwana huwapa wale ambao wana hamu ya haki.

Pekua Alma 29:10, 14–16, na uweke alama zawadi ambayo Alma alipata kwa kuleta nafsi kwa Kristo. Unaweza kutaka kuweka alama kila wakati Alma anapotumia nenoshangwe katika aya hizi.

Kanuni moja iliyofundishwa katika Alma 29 ni: Tutapata shangwe tunapowasaidia wengine kutubu na kuja kwa Yesu Kristo. Ni matukio gani umewahi kupata ambayo yalikusaidia kuhisi shangwe katika kuwasaidia wengine kuja kwa Kristo?

Tafakari kwa muda njia ambazo kwazo unaweza kuwasaidia watu binafsi katika makundi yafuatayo ya watu kufanya mabadiliko muhimu katika maisha yao na kuja kwa Yesu Kristo: (a) marafiki zako, (b) washiriki wa familia yako, na (c) wale ambao bado usiowajua vizuri. Tafuta uongozi wa Roho unapotafuta fursa ya kuleta wengine kwa Yesu Kristo.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 25–29 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: