Seminari
Kitengo cha 21: Siku ya 1, Alma 45–49


Kitengo cha 21: Siku ya 1

Alma 45–49

Utangulizi

Baada ya Alma kutoa maelekezo yake ya mwisho kwa mwanawe Helamani, aliondoka kutoka kwa watu wa Nefi na hakuwahi kamwe kusikia tena. Wakati wa nyakati ngumu zilizofuatia kwa Wanefi, Helamani na Kapteni Moroni walikuwa ndio viongozi wa kiroho na wa kijeshi wao. Amalikia kiongozi wa Walamani alifuatilia kwa uchoyo matamanio yake dhalimu, akitumia mbinu inayofanana na yale ya ibilisi. Kapteni Moroni alitayarisha watu wake kuwa waaminifu kwa Mungu nyakati hizo za hatari.

Alma 45

Helamani anaamini maneno ya baba yake, Alma, na kuanza huduma yake

Kumbuka mahojiano umeshakuwa na mzazi au kiongozi wa ukuhani. Fikiria aina ya maswali uliyoulizwa. Kabla ya Alma kuondoka nje ya nchi, aliuliza Helamani maswali matatu muhimu. Soma Alma 45:2–7, na utambue na uyawekee alama maswali haya. (“maneno” ambayo Alma alimaanisha katika mstari 2 yanaweza kupatikana katika Alma 37:1.) Fikiria jinsi utakavyojibu maswali ya Alma: Je, unaamini katika maandiko? Je, unaamini katika Yesu Kristo? Je, utashika amri?

mtu na kijana

Baada Helamani kutangaza ushuhuda wake, Alma alizungumza naye juu ya hatma ya Wanefi. Alitoa unabii juu ya maangamizo yao na maangamizo ya watu wengine wowote ambao wangeiva katika uovu juu ya nchi hii teule. Soma Alma 45:16, na ufikirie ukweli ufuatao katika mstari huu: Bwana hawezi kuangalia dhambi na kuivumilia hata kidogo.

Ili kukusaidia kuelewa kanuni hii, kumbuka kwamba kupitia kwa Upatanisho Wake, Mwokozi alilipia dhambi zetu zote kama tutatubu na kutafuta msamaha Wake. Mungu hawezi kuvumilia dhambi katika kiwango chochote. Hata hivyo, kwa sababu Mwokozi alikuwa tayari kuteseka kwa ajili yetu, hatupaswi kuteseka kwa ajili ya dhambi zetu tukitubu.

Soma Mafundisho na Maagano 1:31–33. Unaweza kutaka kuandika mistari hii kama marejeo mtambuko karibu na Alma 45:16.

  1. ikoni ya shajaraJibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Hisia zako kuhusu Mwokozi ni gani, unapofikiri kuhusu upendeleo wake wa kulipia dhambi zenu?

Kama ilivyoandikwa katika Alma 45:20–24, Helamani alianza huduma yake kama nabii wa Bwana na kiongozi wa Kanisa. Yeye na viongozi wengine wa Kanisa waliwateua makuhani na walimu katika mikusanyiko yote, lakini kwa sababu ya ubishi na kiburi kingi watu walikataa kusikiliza viongozi wao.

Alma 46

Kapteni Moroni anawahimiza wenye haki kulinda haki zao na dini yao

Toke Mbele

Kama ilivyoandikwa katika Alma 46:1–7, baadhi ya watu ambao walikuwa na hasira dhidi ya Helamani na ndugu zake waliamua kuacha Kanisa na kufuata mtu mbaya aitwaye Amalikia, ambaye alitaka kuwa mfalme. Soma Alma 46:8–10, na uangalie masomo ambayo Mormoni alitaka tujifunze kutoka kwa hali hii hatari.

Ili kusaidia kulinda uhuru wa watu, Moroni, ambaye alikuwa kapteni mkuu wa majeshi ya Wanefi, alirarua koti lake na kutumia kipande chake kutengeneza “bendera ya uhuru” ili kuhimiza watu katika ulinzi wa uhuru.

Soma Alma 46:12–13, na uweke alama kile ambacho Moroni aliandika juu ya bendera ya uhuru. Tambua jinsi alivyotayarisha kuwasilisha bendera ya uhuru kwa watu. Tafakari kile mistari hii inakufundisha juu ya tabia ya Moroni. Pia soma Alma 48:11–13, 17–18 ili kupata ufahamu zaidi katika tabia ya Kapteni Moroni. Unaweza kutaka kuweka alama sifa za Moroni ambazo ungependa kuendeleza kikamilifu zaidi katika maisha yako mwenyewe.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu moja au zaidi ya sifa za Moroni kutokaAlma 46:12–13 and Alma 48:11–13, 17–18. Eleza ni kwa nini ungependa kuwa na sifa hizi na jinsi unaweza kujitahidi kuziendeleza.

Soma Alma 46:18–22, na uangalie jinsi watu walivyoitikia mwaliko wa Moroni wa kupigania uhuru. Agano lililoelezwa katika mstari 20 ni ahadi maalum ambayo kundi hili la Wanefi lilifanya na Mungu.

Kulingana na Alma 46:20, ni kwa nini Moroni alitaka Wanefi kufanya agano na Mungu kwamba watatetea haki zao na dini yao?

Kama ilivyoandikwa katika Alma 46:28–37, Wanefi waliojiunga na Kapteni Moroni wakaliteka jeshi la Amalikia. Hata hivyo, Amalikia na wengine wachache walitoroka na kujiunga na Walamani. Wengi wa wafuasi wa Amalikia ambao walikamatwa waliingia katika agano ili kuhifadhi uhuru. Wale ambao hawangefanya hivyo waliuawa. Kutokana na matukio ya Wanefi, tunaweza kujifunza kanuni hii:. Tunapokuwa hodari katika kushika amri kama vile Kapteni Moroni alivyofanya, Mungu atatuimarisha na kutubariki.

Kufuatia vita, Kapteni Moroni aliweka bendera ya uhuru kwenye kila mnara wa Wanefi kama “ishara” au ukumbusho wa yale walioagana kupigania na kulinda (angaliaAlma 46:36).

Katika kijitabu cha Kwa Nguvu ya Vijana , Urais wa Kwanza ulisema: “Wapendwa wavulana na wasichana wetu, tuna imani kubwa kwenu. Nyinyi ni wana na mabinti wapendwa wa Mungu na Yeye anawajali. Mmekuja duniani wakati wa fursa kubwa na pia wa changamoto kubwa. Viwango katika kijitabu hiki vitakusaidia na chaguo muhimu unazofanya sasa na ambazo bado utafanya katika siku zijazo. Tunaahidi kwamba mnaweka maagano mliyoweka na viwango hivi, mtabarikiwa na ushirika wa Roho Mtakatifu, imani na ushuhuda wenu utakuwa na nguvu, na mtafurahia wingi wa furaha” ([2011], ii).

  1. ikoni ya shajaraKutokana na kile umejifunza katika ujumbe huo kutoka kwa Urais Kwanza, jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Je, ni ahadi gani zilizotolewa kwako ukitii maagano ya injili uliyofanya na viwango katika kijitabu cha Kwa Nguvu ya Vijana?

    2. Angalia katika ukurasa wa yaliyomo ya kijitabu cha Kwa Nguvu ya Vijana , na uchagua moja ya viwango katika kijitabu hiki. Jinsi gani kutunza kiwango hiki kumebariki maisha yako, au kunawezaje kubariki maisha yako katika siku za baadaye?

Alma 47

Amalikia anakuwa mfalme wa Walamani kupitia usaliti na udanganyifu

Ungefanya nini kama ungekuwa katika vita na mtu akupatie kitabu kinachoelezea kile ambacho adui yako anapanga kufanya ili kukuangamiza wewe na familia yako? Alma 47 inaweza kupatiana ufahamu wa mipango ya adui yetu, ibilisi.

Alma 47 umeandikwa udanganyifu mwingi ambao Amalakia alitumia ili kuwa mfalme wa Walamani ili aweze kuongoza jeshi la Walamani kwa vita dhidi ya Wanefi. Hamu yake ya mwisho ilikuwa ni kuwaleta Wanefi wote chini ya utumwa, na yeye kama mfalme wao.

Amalakia na wafuasi wake walitangulia kwenye nchi ya Nefi, ambapo Walamani waliishi. Mfalme wa Walamani alitamani kuenda vitani dhidi ya Wanefi, lakini wengi wa watu wake walikuwa na hofu. Basi mfalme aliuliza Amalakia kuwalazimisha Walamani waoga kujiunga na vita. Amalikia aliandamana hadi kimbilio mlimani ambapo watu hawa walikimbilia, lakini hakutaka kumsaidia mfalme. Alitaka kuwa kiongozi wa Walamani waoga kwa kumdanganya kiongozi wao, Lehonti, kushuka chini ya mlima pa kimbilio lake. Amalikia alinuia kumuua Lehonti kutumia sumu baada ya yeye kushuka chini.

Soma Alma 47:10–12. Ni mara ngapi Amalikia alimjaribu Lehonti kuacha mahali pake pa usalama? Pia soma Alma 47:17–19. Ni kwa jinsi gani Amalikia alimuua Lehonti baada ya kuteremka chini ya mlima?

Mzee Robert D. Hales

Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alifundisha kuwa watu leo wanaweza kujaribu kuharibu imani yetu na ushuhuda kwa kutujaribu sisi kuacha maeneo yetu ya usalama wa kiroho na kuja katika maeneo ya ibilisi: “Katika Kitabu cha Mormoni, tunasoma kuhusu Lehonti na watu wake walipiga kambi juu ya mlima. Msaliti Amalikia alimhimiza Lehonti ‘kuteremka chini’ na kukutana naye katika bonde. Lakini wakati Lehonti alipoondoka kwa uwanda wa juu, alipewa sumu ‘kidogo kidogo’ mpaka akafa, na jeshi lake likabakia mikononi mwa Amalikia (ona Alma 47). Kwa mabishano na shutuma, baadhi ya watu hutujaribu kuacha uwanda wa juu. Uwanda wa juu ndipo ambapo mwanga ulipo. Ndio sehemu salama. Ni kweli na ndipo ambapo elimu ipo” (“Christian Courage: The Price of Discipleship,” Ensign or Liahona, Nov. 2008, 74).

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa njia gani chache ambazo Shetani analenga kutufanya “kuteremka chini” kutoka uwanda wa juu kiroho?

    2. Je, unafikiri kwamba Shetani anajaribu kuwavutia vijana kushusha viwango vyao “kidogo kidogo”? Je, kuna mfano gani wa jinsi anavyojaribu kufanya hili?

    3. Ni kitu gani mahususi unaweza kufanya ili kukaa katika uwanda wa juu kiroho? Ni kiwango gani cha injili unachohitaji kushughulikia ili kwamba usipunguze kiwango hiki kwa “digrii?”

Kama alivyofanya na Amalikia, Shetani hutaka kutuharibu na kutuvutia kwa kiwango kidogo ili tushushe viwango vyetu.

Alma 48–49

Kapteni Moroni anawahamasisha Wanefi kujiimarisha wenyewe kimwili na kiroho

Wakati Amalikia alipokuwa akijaribu kupata uwezo kwa “udanganyifu na hila” (Alma 48:7) juu ya Walamani na Wanefi, Moroni alikuwa akitenda katika njia tofauti. Soma Alma 48:7–10, na uangalie kile ambacho Moroni alifanya alipojua kuwa Amalikia hivi karibuni angeongoza majeshi ya Walamani dhidi ya Wanefi. Unaweza kutaka kuweka alama mawazo haya: (1) Aliwatayarisha watu kuwa waaminifu kwa Mungu nyakati za shida (ona mstari wa 7). (2) Aliwasaidia watu kuimarisha maeneo ambayo walikuwa na udhaifu (ona mstari wa 8–9). (3) Aliwatayarisha watu kushika na kutetea “imani ya Wakristo,” au Kanisa (ona mstari wa 10).

Kama vile Moroni alivyowasaidia watu wake kujiandaa kwa ajili na kuvumilia nyakati ngumu, viongozi wa Kanisa katika siku zetu hutupa ushauri ili kutusaidia kujiandaa kwa nyakati za shida. Fikiria kuandika ukweli ufuatao katika shajara yako ya kujifunza maandiko karibu na Alma 48:7–10:Tunapofuata ushauri wa watumishi wa Bwana, tutajianda kwa matatizo ya maisha.

Walamani awali walipanga kushambulia mji wa Amoniha na kisha mji wa Nuhu, ambayo ilikuwa miji dhaifu ya Wanefi. Soma Alma 49:4–5 ili kuona majibu ya Walamani walipoona maandalizi ya Wanefi katika mji wa Amoniha. Walamani waliamua kutoshambulia mji kwa sababu ulikuwa umejiandaa vyema dhidi ya mashambulizi. Soma Alma 49:12–14 ili kuona majibu ya Walamani walipojaribu kushambulia mji wa Nuhu.

  1. ikoni ya shajaraChukua dakika chache ili kukagua mazungumzo kadhaa kutoka katika mkutano mkuu wa hivi majuzi (katika Ensign au Liahona). Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, fanya muhtasari ushauri uliyotolewa na moja au zaidi ya wasemaji. Ni kwa jinsi gani ushauri huu unakusaidia kujitayarisha kwa nyakati za shida katika maisha yako? Unawezaje kutumia ushauri huu katika maisha yako?

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 45–49 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: