Seminari
Kitengo cha 17: Siku ya 1, Alma 17–18


Kitengo cha 17: Siku ya 1

Alma 17–18

Utangulizi

Alma 17–18 ina kile Mormoni aliandika kuhusu ujumbe wa wana wa Mosia kwa Walamani. Matukio haya yanatoa mfano wa jinsi wamisionari leo wanapaswa kujiandaa na kuhudumu. Wana wa Mosia walitafuta uongozi wa Bwana walipokuwa wanajitayarisha kuhubiri injili kwa Walamani. Walivyoenda njia zao tofauti, Bwana aliwafariji na wakaahidi wataleta nafsi Kwake. Amoni alienda nchi ya Ishmaeli na kuaanza kufundisha kwa kuhudumia mfalme Mlamani aitwaye Lamoni. Mfalme Lamoni alistaajabia nguvu za Amoni alipotetea mifugo ya mfalme. Huduma hii ililainisha mioyo ya mfalme na watu wake ili kusikia mafundisho ya Amoni kuhusu Mungu na mpango wa wokovu. Mfalme Lamoni aliamini kile Amoni alifundisha, alitambua haja yake ya Mwokozi, akamlilia Bwana kwa ajili ya rehema, na akazidiwa na Roho.

Alma 17:1–18

Wana wa Mosia wanaandaa kuhubiri injili kwa Walamani

Fikiria kuhusu urefu wa muda ambao wazee na kina dada hutumikia katika misheni yao leo. Soma Alma 17:4, na uweke mstari chini ya idadi ya miaka wana wa Mosia walifundisha injili miongoni mwa Walamani.

Wakati Alma alipokuwa akisafiri kwenda nchi ya Manti, alikutana na wana wa Mosia walipokuwa wakirudi nyumbani kutoka kwa misheni yao ndefu, na wote wakafurahi. Soma Alma 17:2–4, na uweke alama kwa maneno na vishazi vinavyoelezea aina ya wamisionari ambayo wana wa Mosia walikuwa.

  1. Rejelea Alma 17:2–4. Katika shajara yako kujifunza maandiko, fanya yafuatayo:

    1. Orodhesha kile wana wa Mosia walifanya ili kujiandaa kuwa wamisionari watendaji, na ueleze matokeo ya maandalizi yao.

    2. Chagua kitu ambacho hawa wamisionari walifanya ambacho ungependa kufanya vizuri katika maisha yako, au tabia ungependa kuendeleza vizuri zaidi. Andika aya kuhusu jinsi unavyoweza kufanya hili.

Tafakari ni mara ngapi unaomba na unapekua maandiko kibinafsi na katika familia yako, na ufikirie juu ya fursa unazo za kufunga. Katika njia gani mazoea haya yamekusaidia kupata “nguvu kwa ufahamu wa kweli” (Alma 17:2)?

Kutoka kwa mfano wa wana wa Mosia, tunajifunza kanuni hii: Kwa kupekua maandiko, kuomba, na kufunga, tunaweza kupokea Roho Mtakatifu na kufundisha kwa nguvu. Kwa kupokea Roho Mtakatifu, tunaweza kujiandaa vilivyo kushiriki injili na wengine.

Soma taarifa ifuatayo kutoka kwa Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Wale Mitume kumi na Wawili, ambapo alifundisha vijana njia wanazoweza kujiandaa kuwa wamisionari. Angalia njia mahususi ambayokwayo unaweza kujiandaa kushiriki injili kama wana wa Mosia walivyofanya.

Picha
Mzee David A. Bednar

“Unaweza kuongezeka katika hamu yako ya kumtumikia Mungu (ona M&M 4:3), na unaweza kuanza kufikiri jinsi wamisionari hufikiri, kusoma kile wamisionari husoma, kuomba kama vile wamisionari huomba, na kuhisi kile wamisionari huhisi. Unaweza kuepuka mvuto wa kilimwengu unaosababisha Roho Mtakatifu kujiondoa, na unaweza kukua kwa uaminifu katika kutambua na kujibu ushawishi wa kiroho. Mstari juu ya mstari na amri juu ya amri, huku kidogo na huko kidogo, polepole unaweza kuwa mmisionari unayetamani kuwa na yule misionari Mwokozi anatarajia. …

“Kutangaza injili si tu shughuli ambayo tunashiriki kwa muda mdogo au zoezi ambalo lazima tukamilishe kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku Za Mwisho. Badala yake, kazi ya umisionari ni dhihirisho ya utambulisho wa kiroho na urithi wetu” (“Becoming a Missionary,” Ensign or Liahona, Nov. 2005, 46–47).

Picha
vijana wakisoma kijitabu cha Joseph Smith

SomaAlma 17:9, na uweke mstari chini ya kile ambacho wana wa Mosia waliombea walipokuwa wakijiandaa kuhudumu. Soma Alma 17:11, na utafakari juu ya kile Bwana aliwaambia kuhusu jinsi ya kuwa chombo katika mikono Yake. Mistari hii inafundisha kanuni: Kwa kuwa mfano mzuri, hasa wakati wa taabu, Bwana anaweza kutufanya chombo katika mikono Yake.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu hali ambayo unahisi ingekuwa mfano mzuri. Fikiria kuhusu mazingira ya shule, hali ya nyumbani na familia yako au na familia kubwa, na mazingira ya kijamii ambayo ni ya uso kwa uso au kwenye mtandao. Elezea jinsi utaonyesha mfano mzuri katika hali hiyo.

Ni vigumu kuwa mfano mzuri katika hali fulani kuliko zingine. Angalia jinsi Walamani wameelezwa katika Alma 17:12–16, na ufikirie ni kwa nini wana wa Mosia wangekuwa na wakati mgumu kufundisha katika hali hii.

Kwa nini unafikiri wana wa Mosia walikuwa tayari kupitia mateso ili kusaidia watu waliowachukia Wanefi? Ili kukusaidia kuelewa kile wana wa Mosia walitarajia kukamilisha, jaza pengo kwa neno kutoka Alma 17:16: Wana wa Mosia walitaka Walamani kuletwa , kwa sababu walitaka Walamani kujua juu ya mpango wa ukombozi.

Ili kukusaidia kuelewa jinsi ya kuwa mfano mzuri kwa wengine, kamilisha zoezi hili kati ya siku chache zijazo: Uliza mwanafamilia au rafiki kukuambia jinsi mfano wa mtu wa kama Kristo umeleta tofauti katika maisha yake.

Alma 17:19–39

Amoni anakuwa mtumishi wa Mfalme Lamoni na kulinda mifugo yake

Unaposoma Alma 17:19–39, angalia jinsi Amoni alitumikia Mfalme Lamoni na watumishi wa mfalme. Fikiria jinsi huduma ya Amoni ilisaidia kutayarisha Walamani ili kupokea injili. Panga kushiriki hadithi ya Amoni akihifadhi mifugo ya mfalme na mwanafamilia au rafiki. Fafanua ukweli ufuatao unaposhiriki hadithi: Kupitia huduma, tunaweza kusaidia kuandaa wengine kukubali injili. Jadili na mtu yule ambaye ungependa kusaidia kuwa imara kiroho. Fikiria jinsi unavyoweza kumtumikia mtu huyu, na uamue jinsi unaweza kutoa huduma.

Alma 18

Uaminifu wa Amoni unavutia Mfalme Lamoni, na Amoni anamfundisha mfalme injili

Watumishi wa Mfalme Lamoni walimweleza kile ambacho Amoni alifanya katika kulinda mifugo ya mfalme. Soma Alma 18:4–6, na uangalia majibu ya mfalme kwa kile Amoni alikuwa amefanya.

Wakati mfalme alipouliza watumishi wake mahali Amoni alikuwa, walimwambia kwamba Amoni alikuwa akitimiza ombi la mapema kutoka kwa mfalme la kutayarisha farasi zake kwa safari kwenda nchi ya Nefi, ambapo baba ya mfalme aliishi. Soma Alma 18:12–15, na uangalie athari ambayo huduma ya Amoni ilileta kwa Mfalme Lamoni.

Picha
Amoni Analinda Mifugo ya Mfalme Lamoni

Soma Alma 18:16–21, na uangalie ushahidi kwamba Bwana alikuwa akimwongoza Amoni alipofundisha Mfalme Lamoni. Katika nafasi iliyotolewa, andika jinsi Roho wa Mungu alimsaidia Amoni katika hali hii.

Unaposoma Alma 18:22–32, angalia kweli maalum za injili ambazo Amoni alimfundisha Lamoni. Unaweza kutaka kuziweka alama katika maandiko yako au kuziandika katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Amoni alipofundisha, alikuwa akijenga kwa imani ambayo yeye na Lamoni walishiriki. Lamoni aliamini katika Mungu —ambaye aliita Roho Mkuu —lakini hakuelewa asili ya kweli ya Mungu.

Soma Alma 18:33–35, na uangalie jinsi Amoni alivyojibu wakati mfalme alipomuuliza ikiwa alitumwa na Mungu.

  1. Kutoka kwa kujifunza kwako kwa Alma 17–18, andika aya fupi katika shajara yako ya kujifunza maandiko ambayo inafanya muhtasari yale Amoni aliweza kufanya miongoni mwa Walamani kwa usaidizi wa Mungu.

Unaweza kutaka kuandika kanuni ifuatayo katika maandiko yako karibu na Alma 18:35: Tunapomtumikia Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo, Wataongeza uwezo wetu wa kufanya kazi Yao.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu moja au yote ya maswali yafuatayo:

    1. Ni kwa jinsi gani kanuni ya kwanza itakusaidia katika majukumu yako ya sasa na ya baadaye katika Kanisa?

    2. Ni kwa jinsi gani unaweza kumtumikia Bwana kwa uaminifu zaidi ili aweze kuongeza uwezo wako wa kufanya kazi Yake?

Kwa sababu ya mfano wa uaminifu wa Amoni na huduma, aliweza kumfundisha Lamoni kuhusu mpango wa ukombozi wa Baba wa Mbinguni. Kumbuka kwamba Lamoni alikuwa akihisi kuwa na hatia kwa mauaji ambayo alikuwa ametenda (angaliaAlma 18:4–6). Soma Alma 18:36–43, na uangalie jinsi Amoni alifundisha mpango wa ukombozi kwa Lamoni na jinsi Lamoni aliitikia mafundisho haya.

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kwa nini unafikiri Upatanisho wa Yesu Kristo utakuwa muhimu hasa kwa ajili ya Mfalme Lamoni kuelewa?

Fikiria jinsi kujifunza mafundisho ya Uumbaji, Kuanguka, na Upatanisho kungeweza kumsaidia Lamoni kutambua haja yake ya Mwokozi. Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya Wale Mitume kumi na Wawili alifundisha juu ya umuhimu wa Uumbaji, Kuanguka, na Upatanisho:

Picha
Mzee Bruce R. McConkie

“Haya matukio matatu ya kiuungu —nguzo tatu za milele—zimesukwa pamoja katika kitambaa kimoja kikubwa kijulikanacho kama mpango wa milele wa wokovu. Tunatazama upatanisho wa Bwana Yesu Kristo kama kiini na msingi na moyo wa dini iliyofunuliwa. Inaleta kutokufa na uzima wa milele wa mwanadamu. Wokovu ni katika Kristo.

“Lakini kama hakungekuwa na kuanguka, hakungekuwa na upatanisho. Kuanguka kwa Adamu kulileta kifo cha kimwili na kifo cha kiroho ulimwenguni, na ni kutoka kwa vifo hivi ndipo mwanadamu na aina zote za maisha zanakombolewa kupitia kwa upatanisho uliotolewa na Bwana Yesu Kristo. Adamu alileta kifo; Kristo kuletwa kutokufa. Wokovu unakuja kwa sababu ya kuanguka na upatanisho.

“Lakini kama dunia na mwanadamu na viumbe vyote hai havikuwa vimeumbwa katika hali yao ya kimwili na furaha, katika hali ya milele, hakungekuwa na kuanguka. Hivyo wokovu uliletwa katika na kupitia na kwa sababu ya uumbaji wa mbingu na ardhi na vyote na vilivyo ndani na juu yake. Wokovu huja kwa sababu ya uumbaji, kuanguka, na upatanisho; kila moja ya hivi vitatu ni sehemu ya mpango mmoja wa uungu” (A New Witness for the Articles of Faith [1985], 81–82).

Kutokana na uzoefu wa Lamoni tunaweza kujifunza ukweli huu: Tunapoelewa haja yetu ya Mwokozi, tutatamani kutubu.

Hitimisha somo la leo kwa kutafakari kile unaweza kufanya kitachokukusaidia kukumbuka haja yako ya Mwokozi.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 17–18 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe)

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha