Seminari
Kitengo cha 19: Siku ya 2, Alma 36


Kitengo cha 19: Siku ya 2

Alma 36

Utangulizi

Baada ya Alma kurudi kutoka misheni yake miongoni mwa Wazoramu, aliwakusanya wanawe watatu na kuwapa ushauri wa kibinafsi kwa kila mmoja (ona Alma 35:16). Ushauri wake kwa Helaman umeandikwa katika Alma 36–37, ushauri wake kwa Shibloni umeandikwa katikaAlma 38, na ushauri wake kwa Koriantoni umeandikwa katikaAlma 39–42. Alma alishuhudia kwa Helamani kwamba Mungu atawaokoa wale walioweka tumaini lao Kwake. Ili kuonyesha ukweli huu, Alma alielezea jinsi alivyokombolewa kutokana na maumivu ya dhambi zake nyingi miaka ya awali. Baada ya kuliitia jina la Yesu Kristo, alizaliwa kwa Mungu na kujazwa na furaha. Kisha alifanya kazi ili kuleta wengine kwa Yesu Kristo.

Alma 36:1–5

Alma anafundisha mwanawe Helamani kuhusu nguvu za Mungu ili kutusaidia katika majaribu yetu.

Tafakari jinsi ushuhuda au mafundisho fulani ya mwanafamilia, rafiki, au kiongozi wa Kanisa yamebariki maisha yako.

SomaAlma 36:1–5, na ujione mwenyewe katika mahali pa Helamani alipokuwa akisikiliza ushuhuda wa baba yake. Ni nini ambacho Alma alitaka Helamani kukumbuka? (Ona mstari 2.) Ni nini ambacho Alma alitaka Helamani kujifunza kutoka kwake? (Ona mstari 3.)

Andika kanuni ifuatayo katika shaajara yako ya kujifunza maandiko karibu na Alma 36:3: Tunapoweka matumaini yetu kwa Mungu, Yeye hutusaidia katika majaribio na mateso yetu yote. Fikiria wakati ulipokuwa na majaribu katika maisha yako. Katika nafasi zilizotolewa, andika njia chache ambazo Mungu alikusaidia na kukukimu wakati huo.

Alma 36:6–22

Alma anaeleza uasi wake na anaelezea jinsi alivyopokea msamaha.

Picha
Uongofu wa Alma

Alma alimwelezea mwanawe Helamani jinsi Mungu alivyomkomboa kutokana na maumivu ya dhambi zake. Soma Alma 36:6–10, na uchambue kile kilichomtokea Alma katika ujana wake alipokwenda pamoja na wana wa Mosia wakitafuta kuangamiza Kanisa.

Katika Kitabu cha Mormoni kuna maelezo matatu ya malaika kumtembelea Alma na wana wa Mosia. Alma 36 ina maelezo ya kina zaidi ya kile Alma alipitia wakati wa siku tatu za mchana na usiku wakati hangeweza kutembea au kuzungumza. (Ili kusoma maelezo mengine, onaMosia 27 na Alma 38.) Soma Alma 36:11–16, na uweke alama maneno au vishazi ambavyo Alma alitumia ili kuelezea hofu au maumivu aliyopitia baada ya malaika kutokea.

Rais Boyd K. Packer wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ametusaidia kuelewa maana ya niliteseka na nilipoteseka:

Picha
Rais Boyd K. Packer

Niliteseka ina maana ‘kuteswa.’ Zamani kitanda cha kutesea kilikuwa mfumo ambapo mwathirika aliwekwa na kila kifundo cha miguuni na mkono kilifungwa kwenye mironjo ambacho kingeweza kugeuzwa na kusababisha maumivu makali.

“Uma ni fremu yenye msumari pande zote. Linapovutwa juu ya ardhi, linapasua na kukata ndani ya udongo. Maandiko mara nyingi huzungumza juu ya nafsi na akili ‘kuteseka’ kwa hatia” (“The Touch of the Master’s Hand,” Ensign, May 2001, 23).

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini unafikiri Alma alitumia maneno ya nguvu katika kueleza jinsi alijisikia. Pia andika jinsi maneno haya yanaelezea hatia na maumivu ya mtu ambaye amefanya dhambi na hajatubu.

Unaweza kutaka kuandika ukweli ufuatao katika maandiko yako karibu Alma 36:11–16: Dhambi inaweza kusababisha maumivu na majuto.

Soma {Alma 36:17–18,na uangalie kile Alma alikumbuka baba yake akitoa unabii kuhusu. Tambua kile Alma alifanya alipokumbuka kile baba yake alikuwa amemfundisha.

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alitoa umaizi wa uzoefu wa Alma: :Alma alikuwa ameguswa na mafundisho ya baba yake, lakini ni muhimu hasa kwa unabii aliokumbuka ulikuwa ni mmoja kuhusu ‘kuja kwa mmoja aitwaye Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, kulipia dhambi za ulimwengu.’ Alma 36:17.) Hiyo ndilo jina na huu ndio ujumbe ambao kila mtu ni lazima asikie. Alma alisikia hayo, na akalia kutokana na uchungu wa kuzimu ambao uliendelea kuteketeza dhamiri ambayo haingepona. ‘Ee Yesu, wewe Mwana wa Mungu, nihurumie.’ Alma 36:18.) Maombi yoyote mengine tunayotoa, mahitaji yoyote mengine tunayo, yote kwa namna fulani yanategemea ombi hilo: ‘Ee Yesu, wewe Mwana wa Mungu, nihurumie.’ Yeye yu tayari kutupa huruma hiyo. Alilipa kwa maisha yake ili kuupeana” (However Long and Hard the Road [1985], 85).

  1. Fikiria kitambo wakati ulipoomba ili kupokea baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo, ikiwemo baraka ya msamaha wa dhambi. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini unafikiri ni muhimu kuomba Bwana baraka ya Upatanisho katika maisha yako.

  2. SomaAlma 36:19–22, na uweke alama maneno na vishazi vinavyoelezea jinsi Alma alivyobadilika baada ya kuomba ili kupokea huruma. Andika baadhi ya maneno na vishazi katika shajara yako ya kujifunza maandiko, na ueleze kile vinakufundisha juu ya uwezo wa Upatanisho wa Mwokozi.

Picha
Yesu Kristo

Kutoka kwa maandiko haya tunajifunza kanuni hii: Tukifanya imani katika Upatanisho wa Yesu Kristo, basi atatuokoa kutokana na maumivu ya dhambi zetu na kutujaza furaha. Tafakari kile unaweza kufanya imani zaidi katika Yesu Kristo ili kwamba, kama Alma, uweze kukombolewa kutokana na hisia za maumivu au huzuni kutoka kwa dhambi zako.

Soma hali ifuatayo, na ufikirie jinsi unavyoweza kujibu: rafiki ambaye amekuwa akisoma Kitabu cha Mormoni anakuomba usaidizi katika kuelewa maneno ya Alma katikaAlma 36:19. Rafiki yako anauliza, “Kama naweza kukumbuka dhambi zangu na bado kuhuzunika kwazo, je, ina maana mimi sijasamehewa?”

Soma maelezo yafuatayo kutoka kwa Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza, na uweke mstari chini ya vishazi vyovyote ambavyo unaamini vitakuwa na manufaa kwa rafiki yako:

“Shetani atajaribu kutufanya kuamini kwamba dhambi zetu hazisamehewi kwa sababu tunaweza kuzikumbuka. Shetani ni mwongo; yeye anajaribu kuziba macho yetu na kutupotosha mbali na njia ya toba na msamaha. Mungu hakuahidi kwamba hatutakumbuka dhambi zetu. Kukumbuka kutatusaidia kuepuka kufanya makosa sawa na hayo tena. Lakini tukibakia wakweli na waaminifu, kumbukumbu ya dhambi zetu italainishwa baada ya muda. Hii itakuwa ni sehemu ya uponyaji unaohitajika na mchakato wa utakaso. Alma alishuhudia kwamba baada ya ya kumlilia Yesu kwa huruma, bado aliweza kukumbuka dhambi zake, lakini ufahamu wa dhambi zake haukumhuzunisha tena na kumtesa, kwa sababu alijua alikuwa amesamehewa (ona Alma 36:17–19).

“Ni wajibu wetu kuepuka chochote kitakachorejesha kumbukumbu ya dhambi za zamani. Tunapoendelea kuwa na ‘moyo uliyopondeka na roho iliyovunjika’ (3 Nefi 12:19), tunaweza kuamini kwamba Mungu ‘hatazikumbuka[dhambi zetu] tena’[M&M 58:42]”(“Point of Safe Return,” Ensign or Liahona, May 2007, 101).

Pia ni muhimu kutambua kuwa Alma hakusema kwamba hakukumbuka dhambi zake tena bali kwamba hakukumbuka uchungu wa dhambi zake tena, na “hakuteseka” na ufahamu wake (Alma 36:19). Toba ya kweli itasababisha uchungu na hatia ya dhambi kuondolewa mbali (onaEnoshi 1:6–8).

  1. Katika shajara ya kujifunza maandiko, andika jibu kwa rafiki aliyetajwa hapo juu, na utumie ufahamu uliopata kutoka kwa maelezo ya Rais Uchtdorf . Jumuisha katika jibu lako la ni kwa nini unadhani ni baraka kwamba bado tuendelee kukumbuka dhambi zetu, hata kama “hatutateseka na ufahamu wa dhambi [zetu]” (Alma 36:19) baada ya toba yetu.

Alma 36:23–30

Alma anaelezea ni kwa nini anafanya kazi bila kukoma ili kuleta wengine kwa toba

Unahisi vipi unaposhiriki chakula kitamu na rafiki? Unapopokea kipande cha habari ya kusisimua, ni jambo gani la kwanza unataka kufanya? Kwa nini unafikiri watu wengi wana hamu ya haraka ya kushiriki kile walichokisikia na mtu mwingine? Soma Alma 36:23–24, na uangalie jinsi hisia ilivyoelezwa katika maswali haya inahusiana na tukio la Alma kufuatia uongofu wake. Ni nini Alma alitaka watu wengine kuona?

Soma Alma 36:25–26, na utambue jinsi jitihada za Alma za kufundisha injili zilimwathiri yeye na watu wengine. Kamilisha kanuni ifuatayo, kulingana na yale ambayo umejifunza kuhusu kushiriki injili kutoka kwa mistari hii: Tunaposhiriki injili na wengine, sisi tunapokea.

  1. Andika taarifa yako ya kanuni iliyokamilika katika shajara yako ya kujifunza maandiko, na ueleze ni kwa nini unaamini kanuni hii ni ya kweli. Kama sehemu ya maelezo yako, unaweza kutaka kujumuisha uzoefu uliyopata kwa kuhisi furaha kwa ajili ya kushiriki injili na watu wengine.

Fikiria juu ya mtu unayemjua —rafiki, mwanafamilia, muumini katika kata au tawi —ambaye anaweza kunufaika kutokana na ushuhuda wako wa Mwokozi na injili Yake ya urejesho. Tafakari jinsi unavyoweza kushiriki na mtu huyu ushuhuda wako wa jinsi Yesu Kristo anaweza kutuokoa kutokana na uchungu na kutujaza furaha. Unaweza kufikiria kuandika barua au barua pepe kwa mtu huyu, au unaweza kutaka kuandika maelezo machache ili kujiandaa kwa muda maalum utakapozungumza na mtu huyo.

Picha
msichana akiandika
  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 36 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha