Seminari
Kitengo cha15: Siku ya 4, Alma 8–10


Kitengo cha 15: Siku ya 4

Alma 8–10

Utangulizi

Baada ya Alma kufundisha katika Zarahemla, Gideoni, na Meleki na alipata watu wengi kukubali ujumbe wake, watu katika Amoniha walikataa ujumbe wake na kumtupa nje ya mji wao. Hata hivyo, akiwa mtiifu kwa amri ya Bwana, Alma alirudi Amoniha Bwana alimtayarisha Amuleki kumpokea Alma katika Amoniha na kujiunga naye katika kuwashuhudia watu. Alma na Amuleki aliwaonya watu wa Amoniha kwamba kama hawatatubu, wataangamizwa. Amuleki kwa uaminifu alimtii Mungu na kutumia sifa yake, jina zuri, na ushawishi kusaidia nabii Alma na kushuhudia juu ya Yesu Kristo.

Alma 8

Alma kwa utiifu anarudi Amoniha, ambapo anamuandaa Amuleki kuhubiri

Baada ya Alma kufundisha injili katika Zarahemla na Gideoni (ona Alma 5–7), alisafiri kwenda Meleki. Soma Alma 8:4–5, na utambue jinsi watu wa Meleki walipokea mafundisho ya Alma. (Kishazi “mpango mtakatifu wa Mungu” katika Alma 8:4 kinahusu ukuhani, kama vile utaona katika Alma 13.)

Baada ya Alma kumaliza kufundisha huko Meleki, alisafiri hadi Amoniha ili kuhubiri. Alikuwa na uzoefu tofauti sana na watu ambao waliishi huko. Jifunzeni picha zifuatazo na vifungu vya maandiko, na kisha uandike maelezo kwa kila moja, ukiandika kwa muhtasari kile kilichotokea kwa Alma alipokuwa huko Amoniha:

Picha
Alma akikaa chini ardhini

Alma 8:8–13.

Picha
Alma na malaika

Alma 8:14–16.

Picha
Alma na Amuleki

Alma 8:18–26.

Fikiria maswali yafuatayo (hauhitajiki kuandika majibu yako):

  • Malaika alimtokea Alma alikuwa malaika yule yule aliyemtokea na wana wa Mosia awali. Jinsi gani maneno ya malaika yamekuwa ya faraja kwa Alma (ona Alma 8:15)?

  • Kwa nini ilikuwa vigumu kwa Alma kurudi Amoniha (ona Alma 8:16)?

Licha ya ugumu wa amri, Alma “alirudi kwa haraka katika nchi ya Amoniha” (Alma 8:18). Rais Howard W. Hunter alifundisha kwamba Bwana anapenda kutii vile: “Hakika Bwana anapenda, zaidi ya kitu kingine, uamuzi usio yumba yumba wa kutii ushauri Wake” (“Commitment to God,” Ensign, Nov. 1982, 58).

  1. Chagua moja au zaidi ya hali zifuatazo. Kisha uandike katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi mtu anaweza kubarikiwa ikiwa yeye ni mtiifu:

    1. Wakati msichana anapoondoka kwenda shule, mama yake anamuliza kuvaa shati inayostahili zaidi.

    2. Kuhani mpya anapewa changamoto na Askofu wake au rais wa tawi kupata tuzo la Wajibu kwa Mungu.

    3. Wamisionari wawili wanahisi kuvutiwa kuitembelea familia isiyohudhuria, ambayo mama si mshiriki wa Kanisa.

Unaweza kutaka kuandika kanuni zifuatazo katika maandiko yako kandoni mwa Alma 8:18–20: Kama tutaitika haraka kwa neno la Bwana, atatusaidia kutimiza amri Zake.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu wakati ambapo ulihisi kuwa Bwana alikusaidia kuwa mwema na mtiifu licha ya mazingira magumu.

Soma Alma 8:27–32, ukitafuta njia zaidi ambazo Bwana alimsaidia Alma kufanya kile alichoagizwa kufanya.

Alma 9

Alma anawaonya watu wa Amoniha kutubu na kujiandaa kwa ujio wa Yesu Kristo

Alma 9 unaandika jitihada za Alma za kufundisha watu wa Amoniha kuhusu haja yao ya kutubu na kukombolewa kupitia kwa Mwokozi, Yesu Kristo. Ili kujaribu kusaidia watu hawa waovu kutambua haja yao ya kutubu, Alma aliwaomba kukumbuka kile Mungu aliwatendea na baba zao.

Angalia katika Alma 9:8–10, 13 kwa marudio ya maneno kumbuka na kusahaulika. Je! Unafikiri vipi wenyeji wa Amoniha wangekuwa tofauti kama wangekumbuka mambo ambayo Alma alizungumzia?

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Kwa nini unafikiri ni muhimu kukumbuka uzoefu wa kiroho uliokuwa nao zamani? Kisha uandike kuhusu uzoefu moja wa kiroho ambao hautaki kusahau.

Baada ya kuwaita watu katika Amoniha kutubu, Alma aliwafundisha kwamba wanapaswa kujiandaa kwa wakati Mwokozi atakapokuja duniani. Soma Alma 9:26–27, na uweke alama kwa vishazi vinavyokusaidia kuelewa vyema sifa za Mwokozi. (Neno usawa ina maana ya haki na uadilifu.) Maneno na vishazi hivi vinakufundisha nini juu ya Mwokozi? Katika wiki ijayo, chukua muda ili kufikiri juu yake.

Alma 10

Amuleki anaelezea uzoefu wake na malaika na anawahimiza watu kutubu

Tia alama ya mviringo kwenye taarifa inayoelezea vilivyo jinsi ulivyoamka asubuhi ya leo:

  • Mimi niliamka mwenyewe, bila ya kutumia kengele au kuitwa na mtu.

  • Mimi niliamka vile tu kengele yangu ilipolia au mara ya kwanza nilipoitwa.

  • Kengele yangu ililia mara kadhaa, au ilibidi niitwe mara kadhaa kabla ya kuamka.

Soma Alma 10:6, na uangalie ni “miito migapi ya kiroho ya kuamka” ambayo Amuleki alipokea alipokuwa akiendelea kumwasi Bwana Kwenye mistari iliyotolewa, andika jibu lako kwa swali hili: Je, unafikiri vishazi “Sikusikia” na “nisingeweza kuvifahamu” vinaonyesha kuhusu hali ya kiroho ya Amuleki kabla ya malaika kumjia?

Kama ilivyoandikwa katika Alma 10:2–11, Amuleki alielezea maisha yake kabla ya kutembelewa na malaika na uongofu wake kwa Injili. Tafuta Alma 10:1–6 kwa maelezo ambayo yatakusaidia kujua zaidi kuhusu Amuleki.

Picha
Amuleki anafundisha

Amuleki alielezea jinsi Malaika alimwamuru kumpeleka Alma ndani ya nyumba yake na kumhudumia. Soma Alma 10:7–11, na uangalie jinsi Amuleki na wengine walibarikiwa kwa sababu Amuleki alimtii malaika.

Andika kanuni hii karibu naAlma 10:11–12: Tunaposikia na kutii wito wa Bwana, baraka huja kwetu na kwa wengine. Kuna njia nyingi ambazo Bwana anaweza “kutuita” —kupitia kwa uvuvio wa Roho; kupitia kwa hisia; kupitia ndoto; kupitia maneno ya kiongozi wa Kanisa, mwalimu, au mzazi; kwa kuitwa kwa nafasi Kanisani; kupitia shida, au kwa njia nyingine.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu swali lifuatalo: Ni lini ulihisi kuwa ulibarikiwa kwa sababu ulitii “wito” kutoka kwa Bwana?

Kama ilivyoelezwa katika salio la Alma 10, wengi wa watu katika Amoniha hawangesikiliza maneno ya Amuleki. Amuleki aliwaonya kwamba ikiwa hawangetubu, siku itakuja ambapo wataangamizwa. Soma Alma 10:22–23, na utambue ni kwa nini watu walikuwa wakiokolewa kutokana na maangamizo ya wakati huo. Mistari hii inakufundisha nini juu ya umuhimu wa kuwa mwenye haki hata kama wale walio karibu nawe sio?

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 8–10 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha