Seminari
Kitengo cha 21: Siku ya 4, Alma 59–63


Kitengo cha 21: Siku ya 4

Alma 59–63

Utangulizi

Helamani aliandika barua kwa Kapteni Moroni, akimwambia kuhusu jitihada za jeshi na kuomba msaada kutoka kwa serikali ya Wanefi. Kapteni Moroni alifurahi kujua kuhusu mafanikio ya Helamani, lakini alikuwa na hasira kwa serikali kwa kupuuza kutuma askari zaidi. Kapteni Moroni aliandika barua ya ukemevu kwa mwamuzi mkuu, Pahorani. Katika jibu lake, Pahorani alieleza juu ya uasi dhidi ya serikali. Moroni alienda kumsaidia na kushinda waasi. Wakati huo majeshi ya Wanefi waliweza kwa umoja kuwashinda Walamani. Baada ya miaka 14 ya vita, Wanefi tena walikuwa na amani katika nchi, kuruhusu Helamani na ndugu zake kuzingatia kujenga Kanisa.

Alma 59

Wanefi walipoteza ngome, na Kapteni Moroni anahuzunika kwa sababu ya uovu wa watu.

Wakati Kapteni Moroni alipopokea barua kutoka kwa Helamani ikielezea mafanikio ya jeshi lake, Moroni na watu wake walifurahia. Moroni kisha akatuma barua kwa Pahorani, kiongozi wa Wanefi katika Zarahemla, akimtaka kutuma askari zaidi na vifaa kwa Helamani. Lakini hakuna askari zaidi waliotumwa. Kwa hiyo, wakati Walamani waliposhambulia mji wa Nefiha, watu wa Nefiha walilazimishwa kukimbia na Walamani wakateka mji.

Soma Alma 59:9–12 ili kujifunza majibu ya Moroni kwa ushindi wa Walamani. Fikiria kuweka alama katika maandiko yako kishazi hiki katika Alma 59:9: “Ilikuwa ni rahisi kulinda mji usianguke kwenye mikono ya Walamani kuliko kuuteka kutoka kwao.” Kutoka kwa kishazi hiki, tunaweza kujifunza kanuni hii:Ni rahisi na bora kubakia mwaminifu kuliko kurudi nyuma katika imani baada ya kupotea

  1. Jifunze kishazi ulichoweka alama katika Alma 59:9 na kanuni katika aya ya awali. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini ni rahisi kuepuka ulevi wa vitu vyenye madhara kuliko kushinda ulevya?

    2. Kwa nini ni rahisi kudumisha ushuhuda kuliko kuupata tena baada ya kuupoteza?

    3. Kwa nini inaweza kuwa rahisi kwa mtu kubaki hai katika Kanisa kuliko kurejea Kanisani baada ya kutoshiriki kikamilifu?

Picha
mvulana anaegemea kabati

Alma 60–62

Moroni anamuuliza Pahorani kuhusu sababu ya kupuuzwa na serikali

Baada ya mji wa Nefiha kutekwa na Walamani, Kapteni Moroni aliamua kuandika rufaa kwa Pahorani, mwamuzi mkuu katika Zarahemla. Soma Alma 60:17–24, na uangalie madai yaliyofanywa na Moroni kuhusu Pahorani na watu katika Zarahemla.

Soma Alma 60:23 tena, na utambue maelezo ya Kapteni Moroni wa usafishaji wa “chombo cha ndani” kwanza. Alikuwa akimaanisha haja ya kuondoa ufisadi katika serikali ya Wanefi na watu wake. Hata hivyo, mstari huu unaweza kutumika kwa maisha yetu pia. Fikiria kuweka uchafu au tope ndani ya kikombe. Hata kama uliosha nje ya kikombe, je, utajisikia sawa kunywa kutoka kwa kikombe hicho?

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Tukijiona wenyewe kama “vyombo,” unafikiri inamaanisha nini kusafisha ndani ya chombo?

    2. Kwa nini kutakasa chombo chetu cha ndani kunatusaidia kuwa na huduma kubwa zaidi katika ufalme wa Bwana?

Kama ilivyoandikwa katika Alma 60:33–36, Kapteni Moroni alimwambia Pahorani kutuma wanaume kwa haraka na vifaa kwa jeshi lake na kwa jeshi la Helamani. Ikiwa Pahorani hangefanya, Moroni alisema angeongoza kikosi cha kijeshi huko Zarahemla na kumlazimisha kufanya mambo haya. Pahorani alipokea barua ya Moroni na kumjibu kwa haraka. Soma Alma 61:1–5 ili kugundua kile kilichokuwa kinatendeka katika Zarahemla.

Soma Alma 61:9–14, na ufikirie kuhusu jinsi Pahorani alijibu shutuma za Moroni. Fikiria kuwekea alama kauli hizo zinazoelezea ukuu wa tabia ya Pahorani. Badala ya kukasirika, Pahorani alimwalika Moroni kuungana pamoja naye kwa nguvu za Bwana kupigana na adui. Soma Alma 62:1 ili kugundua jinsi Moroni alivyohisi alipopokea majibu ya Pahorani.

Fikiria kuandika kweli zifuatazo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Tunaweza kuchagua kutokasirishwa na maneno au matendo ya wengine. Tunapoungana katika haki na wengine, tunaimarika zaidi katika vita vyetu dhidi ya uovu.

Mzee David A. Bednar wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili alielezea:

Picha
Mzee David A. Bednar

‘Kupitia kwa nguvu ya kuimarisha ya Upatanisho wa Yesu Kristo, wewe na mimi tunaweza kubarikiwa ili kuepuka na kushinda kukasirika. ‘Wana amani nyingi waipendao sheria yako:Wala hawana la kuwakwaza’ (Zaburi 119:165). …

“… Moroni … alimwandikia Pahorani ‘kwa njia ya lawama’ (Alma 60:2) na kumkashifu kwa ukali kuhusu ukaidi, uvivu, na upuuzaji. Pahorani pengine angeudhika na Moroni na ujumbe wake, lakini alichagua kutokasirika. …

“Mojawapo wa viashiria vikubwa vya ukomavu wetu wa kiroho imefunuliwa kwa jinsi tunavyofanya kuhusu udhaifu, upungufu wa ujuzi, na vitendo vya kukera vya wengine. Kitu, tukio, au maelezo yanaweza kukera, lakini wewe na mimi tunaweza kuchagua kutokerwa — na kusema pamoja na Pahorani, ‘haijalishi’ [Alma 61:9]” (“And Nothing Shall Offend Them,” Ensign or Liahona, Nov. 2006, 90–91).

  1. Fikiria juu ya wakati ulipochagua kutokereka na maneno au matendo ya wengine. Andika aya fupi kuhusu umuhimu wa kuchagua kutokukereka .

Kama ilivyoandikwa katika Alma 62, Kapteni Moroni alileta jeshi lake Zarahemla ili kusaidia Pahorani kuwapindua watu wa mfalme — wapinzani wa Nefi waliotaka kuweka mfalme na kuingia katika muungano pamoja na Walamani. Watu wa mfalme walikuwa wamezuia Pahorani kutuma watu na vifaa kwa usaidizi wa Moroni na Helamani. Moroni na Pahorani kisha wakaunganisha nguvu zao na kupata msaada kutoka kwa majeshi mengine ya Wanefi ili kuondosha Walamani nje ya nchi. Wakati huu Walamani wengi walitubu na kuungana na watu wa Amoni.

Fikiria baadhi ya changamoto ambazo pengine zilikuwepo kwa ajili ya familia na watu binafsi mwishoni mwa vita hivyo. Soma Alma 62:39–41 ili kuona jinsi Wanefi walivyoathirika na majaribio ya vita. Unaposoma, angalia kweli unazoweza kubaini katika mistari hii.

Andika kanuni au ukweli ufuatayo katika maandiko yako karibu naAlma 62: 39–41 au katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Tunaweza kuwa karibu na Bwana wakati wa majaribio yetu

  1. Andika majibu kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini unafikiri watu wengine hukua karibu na Bwana wanapokabiliwa na majaribio ilihali wengine hujiondoa mbali kutoka Kwake?

    2. Umejifunza nini kutoka kwa sura juu ya vita kuhusu kuwa mwanafunzi wa Yesu Kristo katika nyakati za shida au majaribio?

Alma 63

Wanefi wengi wanasafiri nchini upande wa kaskazini

Baada Helamani kufariki (onaAlma 62:52), ndugu yake Shibloni alichukua usimamizi wa kumbukumbu takatifu. Soma Alma 63:1–2 ili kuona Shibloni alikuwa mtu aina gani. Kama ilivyoandikwa katika Alma 63, Moroni na Shibloni walikufa, na Moroniha mwana wa Moroni, akachukua mamlaka ya majeshi ya Wanefi.

Soma Alma 63:10–13. Kabla ya kufa, Shibloni alimpa Helamani, ambaye alikuwa mwana wa Helamani, usimamizi wa kumbukumbu takatifu. Helamani alihifadhi kumbukumbu ambazo tayari zilikuwa zimeandikwa na kuanza kuandika kumbukumbu ambayo ingekuwa kitabu cha Helamani.

Alma 63:5–8 imeandikwa kwamba Wanefi wengi walisafiri kwa meli kwa nchi upande wa kaskazini na hawakuwahi kusikika tena. Pia, mwisho wa Alma 63 inafunua kwamba mara nyingine tena kulianza kuwa na ubishi kati ya Walamani na Wanefi, hivyo kukamilisha kitabu kirefu na chenye maongozi cha Alma.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 59–63 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha