Seminari
Kitengo cha 15: Siku ya 1, Alma 5:1–36


Kitengo cha 15: Siku ya 1

Alma 5:1–36

Utangulizi

Wakati Kanisa likitishiwa kwa njia ya uovu na ubishi (ona Alma 4:9–11), Alma alijua kuwa mageuzi ya kweli yanaweza kuja tu kupitia mabadiliko makuu katika mioyo ya waumini wa Kanisa. Kama kuhani mkuu wa Kanisa, Alma alianza ujumbe wake wa kuwaokoa watu wa Zarahemla kwa kushuhudia juu ya Yesu Kristo na kuwaalika watu watubu. Aliwahimiza kujiandaa kwa hukumu ya Bwana kwa kuwa na imani katika neno la Mungu na kutathmini hali ya kiroho ya nyoyo zao. Unaposoma nusu ya kwanza yaAlma 5, fikiria jinsi unaweza kutumia kile umejifunza ili uweze kupata au kuendelea kupata mabadiliko makuu ya moyo yaliyojadiliwa katika sura.

Alma 5:1–13

Alma anakumbuka uongofu wa baba yake na wale waliomfuata

Umebadilika kiasi gani tangu ulipokuwa na umri wa miaka 8? Umebadilika kiasi gani tangu ulipokuwa na umri wa miaka 12? Fikiria juu ya njia mbalimbali ambazo watu wanaweza kubadilika, kama vile katika maumbile yao, tabia, au mtazamo. Tafakari kile kinaweza kusababisha au kuleta baadhi ya mabadiliko haya katika watu. Kisha usome Alma 5:12, na uangalie kilichobadilika katika Alma Mzee. Unaposoma Alma 5:1–13, fikiria jinsi moyo wa mtu unaweza kubadilika.

Mzee Gerald N. Lund, ambaye baadaye alihudumu kama mshiriki wa wale Sabini alifundisha kwamba wakati neno moyo linatumika katika maandiko, mara nyingi inahusu “mtu halisi wa ndani” (“Understanding Scriptural Symbols,” Ensign, Oct. 1986, 25). Fikiria kwa muda jinsi “mabadiliko makuu ya moyo” ni tofauti na njia nyingine ambayo watu wanaweza kubadilika —ikiwemo pamoja na njia ulizofikiria kuhusu ulipoanza somo hili.

Kumbuka kwamba watu wa Mfalme Benyamini waliona “mabadiliko makuu” ndani ya mioyo yao, ambayo yaliwafanya “wasiwe na tamaa ya kutenda maovu, lakini kutenda mema daima” (Mosia 5:2). Unaweza kutaka kuandika ufafanuzi kutoka kwa Mzee Lund na Mosia 5:2 marejeo ya maandiko katika pambizo la maandiko yako karibu na Alma 5:11–13.

Mzee D. Todd Christofferson

Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili alieleza: “Unaweza kuuliza, kwa nini mabadiliko haya makuu hayatokei haraka zaidi kwangu? Unapaswa kukumbuka kwamba mifano ya ajabu ya watu wa Mfalme Benyamini, Alma, na wengine kadha katika maandiko ni —ajabu na si kawaida. Kwa wengi wetu, mabadiliko ni taratibu zaidi na yanatokea kwa muda mrefu. Kuzaliwa tena, tofauti na kuzaliwa kwetu kimwili, ni mchakato badala ya tukio. Na kushiriki katika mchakato huo ni lengo kuu la maisha” (“Born Again,” Ensign or Liahona, May 2008, 78).

Soma Alma 5:3–7 na uangalie kile ambacho Alma aliwaambia watu wa Zarahemla ili kusaidia kuandaa mioyo yao kubadilika.

Jibu swali lifuatalo katika kitabu cha kiada hiki: Alma aliwaambia watu wa Zarahemla kuhusu uongofu wa baba yake na watu wengine, vile vile ukombozi wao kutoka utumwani. Je, unafikiri matokeo haya yaliwasaidiaje watu kujiandaa kwa mabadiliko ya moyo?

Soma Alma 5:10, na uweke mviringo kwenye maswali katika sehemu ya mwisho ya maswali matatu ambayo Alma aliuliza watu. Kisha tafuta Alma 5:11–13, ambapo Alma alianza kujibu maswali haya, ili kupata msaada kwa kauli hii: Tunapoamini katika neno la Mungu na kutekeleza imani katika Yesu Kristo, tutapata mabadiliko makuu ya moyo.

Imani katika neno la Mungu inaleta mabadiliko makuu ya moyo kwa sababu neno la Mungu linatufundisha kuhusu Mwokozi. Watu wa Alma waliamini katika neno la Mungu, walilopewa na manabii watakatifu. Walijifunza kuhusu nguvu za ukombozi wa Upatanisho wa Yesu Kristo, na nyoyo zao zikabadilishwa walipokuza imani katika Mwokozi.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea kwa maneno yako mwenyewe jinsi kuamini katika Upatanisho wa Yesu Kristo kunaleta mabadiliko makuu ya moyo.

  2. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi moyo wako umebadilishwa. Ukiwa umegundua mabadiliko ya moyo ulipojifunza Kitabu cha Mormoni mwaka huu katika seminari, unaweza kuelezea uzoefu wako kama sehemu ya jibu lako.

Alma 5:14–36

Alma anafundisha kuwa mabadiliko makuu ya moyo yanahitajika ili kuingia katika ufalme wa mbinguni.

Baada ya Alma kufundisha kwamba imani katika neno la Mungu inatusaidia kuanza mchakato wa kupokea mabadiliko makuu ya moyo, aliomba watu kufikiria maswali mengi. Maswali haya yanaweza kutusaidia kutathmini hali ya mioyo yetu ya kiroho —tamaa na hisia za mtu ndani.

Soma Alma 5:14, na uweke alama kwenye maswali matatu ambayo Alma aliwauliza watu kufikiria kuhusu wao wenyewe. Maswali haya matatu yanaelezea mabadiliko tunayoona tunapotekeleza imani katika ukombozi unaotolewa kwa njia ya Yesu Kristo. Kumbuka kutoka kwa masomo ya awali (ona Mosia 5 na Mosia 27) kwamba “kuzaliwa tena” inahusu mabadiliko ambayo mtu huona wakati anapokubali Yesu Kristo na kuanza maisha mapya si tu kama mfuasi wake lakini pia kama mwana au binti Wake kiroho (ona Mosia 27:25).

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu jinsi mabadiliko ya moyo yanaweza kujitokeza katika uso wa mtu. Katika muktadha huu, neno uso inamaanisha muonekano wa uso wa mtu, ambao huonyesha tabia ya mtu, hisia, au hali ya kiroho. Elezea mtu unayemjua ambaye alipokea sura ya Mwokozi katika uso wake.

Katika kazi ya matibabu kadiogramu ni chati ambayo madaktari hutumia ili kutathmini hali ya mioyo yetu ya kimwili. Inasaidia kutambua hali zinazohitaji matibabu. Jifunze mistari kutokaAlma 5 ambayo imeorodheshwa chini ya kadiogramu ya kiroho hapo chini. Unapojifunza kila mstari, weka alama kwenye sanduku katika chati ambacho kinafafanua jinsi wewe ungejibu swali au maswali katika kila mstari. (Kama ungependa kuweka siri majibu yako, unaweza kunakili chati hii kwenye kipande kingine cha karatasi au katika shajara yako ya binafsi na kisha kuikamilisha.)

Alma 5 Kadiogramu ya Kiroho

Daima

Karibu daima

Kawaida

Wakati mwingine

Nadra, kama inawezekana

Mistari kutokaAlma 5

15

16

19

26

27

28

29

30–31

Ukisha kamilisha kadiogramu yako ya kiroho, somaAlma 5:21–25. Angalia kile ambacho Alma alifundisha kuhusu ukweli huu: Kwa kupitia mabadiliko ya moyo, tunajiandaa kupokea mahali katika ufalme wa mbinguni (ufalme wa selestia)

  1. ikoni ya shajaraFanya yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Tengeneza orodha ya maneno na vishazi ambavyo Alma alitumia katika Alma 5:21−25 ili kuelezea hali ungependa kuwa nayo kwa sasa.

    2. Eleza jinsi unafikiri mabadiliko ya moyo hutuandaa sisi kupokea mahali katika ufalme wa mbinguni.

Soma Alma 5:33–36, na ufikirie jinsi unavyohisi kuhusu ujumbe wa Alma. Tafuta maneno na vishazi ambavyo vitakusaidia kujibu maswali yafuatayo:

  • Je, Bwana ananialika nifanye nini?

  • Ni zawadi gani za kukubali mwaliko huu?

  • Mistari hii inanifundisha nini kuhusu Mwokozi?

Soma maelezo yafuatayo ya Rais Ezra Taft Benson ambayo yanaonyesha jinsi watu ambao wamekuwa na mabadiliko ya moyo hutaka kuishi:

Rais Ezra Taft Benson

“Unapochagua kumfuata Kristo, unachagua kubadilishwa. …

“Bwana hufanya kazi kutoka ndani nje. Ulimwengu unafanya kazi kutoka nje ndani. Ulimwengu utawaondoa watu kutoka kwa makazi duni. Kristo huondoa makazi duni kutoka kwa watu, na kisha wanajiondoa kutoka kwa makazi duni. Ulimwengu utabadilisha watu kwa kubadilisha mazingira yao. Kristo hubadilisha watu, ambao kisha hubadilisha mazingira yao. Ulimwengu utajenga tabia ya binadamu, bali Kristo anaweza kubadili tabia ya binadamu …

“Wanaume [na wanawake] waliobadilishwa kwa ajili ya Kristo wataongozwa na Kristo. Kama Paulo watauliza, ‘Bwana, unataka nifanye nini?’ (Matendo ya Mitume 9:6.) …

“Mapenzi yao yamemezwa katika mapenzi Yake (Ona Yohana 5:30.)

“Wanafanya siku zote yale yampendezayo Bwana. (Ona Yohana 8:29.)

“Siyo tu kwamba watakufa kwa ajili ya Bwana, lakini muhimu zaidi wanataka kuishi kwa ajili Yake.

“Ingieni majumbani mwao, na picha kwenye kuta zao, vitabu juu ya rafu zao, muziki hewani, maneno na matendo yao yanawaonyesha kama Wakristo.

“Wanasimama kama mashahidi wa Mungu nyakati zote na katika vitu vyote, na katika mahali popote. (Ona Mosia 18:9.)

“Wana Kristo katika mawazo yao, wanapomtazamia Yeye katika kila wazo. (OnaM&M 6:36.)

“Wana Kristo katika mioyo yao kwa kuwa mapenzi yao yamewekwa Kwake milele. (Ona Alma 37:36.)

“Karibu kila wiki washiriki sakramenti na kushuhudia upya kwa Baba yao wa milele kwamba wao wako tayari kuchukua juu yao jina la Mwanawe, daima kumbuka Yeye, na kuweka amri Zake. (Ona Moro. 4:3.)” (“Born of God,” Ensign, Nov. 1985, 5–7).

Ili kukamilisha somo hili, weka mstari chini kwenye wazo moja kutoka kwa kauli ya Rais Benson ambayo inakusaidia kufikiria jinsi unataka kuishi kama mtu ambaye anapitia mabadiliko ya moyo. Weka lengo ambalo litakusaidia kuishi kile umehisi ulipojifunza mafundisho ya Alma kuhusu kupitia mabadiliko ya moyo (unaweza kutaka kukiandika katika shajara yako ya binafsi au kwenye kipande kingine cha karatasi). Unapoendelea kutafuta kuzaliwa kwa Mungu na kuona mabadiliko ya moyo, utajitayarisha kuingia katika ufalme wa Mungu.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 5:1–36 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: