Seminari
Kitengo cha 20: Siku ya 4, Alma 43–44


Kitengo cha 20: Siku ya 4

Alma 43–44

Utangulizi

Katika Alma 43–44, Mormoni alianza kuandika kuhusu vita kati ya Walamani na Wanefi. Wakati Alma na wanawe walipoendelea kuhudumia watu, Wazoramu walijiunga na jeshi la Walamani ili kushambulia Wanefi. Kapteni Moroni alionyesha imani na hekima katika kuwatetea Wanefi dhidi ya jeshi la Walamani. Hata ingawa walizidiwa kwa wingi, maandalizi ya jeshi la Wanefi na imani yao katika Yesu Kristo iliwapa faida katika vita. Walipojua wangeshindwa, Walamani walifanya agano la amani na wakatoka nje ya nchi hiyo kwa msimu.

Alma 43

Maandalizi na mikakati ya Kapteni Moroni inasaidia kuvuruga miundo ya jeshi la Walamani

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika orodha ya baadhi ya mipango, malengo, na hamu yako kwa maisha yako ya baadaye. Unapoandika, fikiria kuzingatia malengo ya kiroho na hamu, kama vile utume, ndoa ya hekalu, na familia.

Picha
wachumba vijana hekaluni

Baada ya kumaliza kuandika orodha yako, tambua hamu na malengo unayojisikia Shetani akikutaka ukamilishe. Unapojifunza Alma 43–44, angalia kanuni ambayo itakusaidia kukamilisha malengo yako ya haki licha ya jitihada za adui za kuzuia mafanikio yako.

Katika Alma 43:1–4, licha ya jitihada za Alma za kuleta Wazoramu Kanisani, wengi wao walijiunga na Walamani katika maandalizi yao ya kuwashambulia Wanefi. Soma Alma 43:5–8, na utambue “miundo” (mipango) ya kiongozi wa Walamani Zerahemna. Unaweza kutaka kuweka alama dhamira za Zerahemna unapozigundua. Tafakari jinsi miundo au hamu ya Zerahemna kwa Wanefi inaweza kuwa kama miundo ambayo Shetani anaweza kuwa nayo kwako.

Ifuatayo soma Alma 43:9–11, na utambue miundo au tamaa ya Wanefi. Sasa tafakari jinsi tamaa hizi zinaweza kufana na tamaa ya haki ulizonazo.

Kapteni Moroni, kapteni mkuu wa majeshi ya Wanefi, alitayarisha watu wake ili kutetea nchi yao na familia kutokana na nia mbaya ya Zerahemna. Soma Alma 43:16–19, ukiangalia ni maandalizi gani Kapteni Moroni na Wanefi walifanya.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, chora mambo mawili ambayo Moroni alipeana kwa watu wake ili kuwaandaa kwa ajili ya vita.

Sasa soma Alma 43:20–22 ili kugundua jinsi Walamani walijibu kuhusu maandalizi ya Wanefi. Tafakari ni kwa nini Walamani waliondoa mashambulizi yao hata ingawa walikuwa wengi kuliko Wanefi.

Tunapojifunza maelezo ya mapambano ya kimwili katika Kitabu cha Mormoni, tunaweza kuyafananisha na vita vya kiroho tunayopitia.

  1. Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni nini unaweza kujifunza kutoka kwa maandalizi ya Moroni kwa ajili ya vita juu ya kujitetea mwenyewe dhidi ya mashambulizi ya Shetani na majaribu?

Baada ya Walamani kujiondoa, Moroni hakujua mahali ambapo maadui zake wangeshambulia tena. Kama ungekuwa Moroni, ungeweza kufanya nini ili kujaribu kujiandaa kwa mashambulizi mengine?

Soma Alma 43:23–24 ili kujua kile Moroni alifanya.

Kutoka kwa mfano wa Moroni tunajifunza: Tukitafuta na kufuata ushauri wa kinabii, tutaweza kujilinda vilivyo dhidi ya adui. Kama vile nabii Alma aliweza kumwaambia Moroni jinsi ya kuwalinda Wanefi dhidi ya maadui zao, manabii wa Bwana leo wanatufundisha jinsi ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya kiroho ya adui.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika sentensi chache juu ya aina ya ushauri wa kinabii iliopeanwa katika siku za mwisho ambao, kama ukiutii, unaweza kukusaidia kujikinga dhidi ya miundo na majaribu ya Shetani.

Kama ilivyoandikwa katika Alma 43:25–43, Moroni alitenda juu ya maarifa aliyopokea kutoka kwa nabii kwa kugawa jeshi lake na kuyaficha katika njia inayofuatwa naWalamani. Jinsi Walamani walivyokaribia, nusu moja ya jeshi la Wanefi lilishambulia na kuwafukuza Walamani hadi mto Sidoni. Baada ya Walamani kuvuka mto, nusu ingine ya jeshi la Wanefi ilishambulia. Wakati Walamani walipoona kuwa wamezungukwa, walipigana vikali mno hata Wanefi wakaanza kusita.

Unaweza kujifunza kanuni kuhusu jinsi ya kutekeleza malengo na hamu ya haki yako kwa kujifunza masalio yaAlma 43. Soma Alma 43:43–54, na ulinganishe vyanzo vya nguvu kwa wote Walamani na Wanefi.

Tafakari kile kilikuwa bora zaidi kuhusu sababu ya vita ya Wanefi kuliko sababu ya Walamani. Tunapolinganisha Moroni na jeshi lake aminifu kwa vita vyetu na adui, tunajifunza kwamba tunapoomba kwa usaidizi katika kutimiza mipango na hamu zetu za haki, Mungu atatusaidia kuyakamilisha..

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu wakati ulipoona usaidizi wa Bwana katika kutimiza malengo yako ya haki.

Alma 44

Baada ya ushindi ya Wanefi, Kapteni Moroni anaamuru Walamani kufanya maagano ya amani.

Kumbuka kwamba katika Alma 43 wakati Kapteni Moroni alipoona kwamba Walamani walizunguukwa na kutishika, aliaamuru watu wake kusitisha mapigano. Soma maneno ya Moroni katika Alma 44:1–6, na uangalie ni nani ambaye Moroni alimsifu kwa ushindi wa Wanefi.

  1. Kulingana na ushuhuda wa Moroni katika Alma 44:4–6, andika ukweli katika shajara yako ya kujifunza maandiko ambao unaweza kukusaidia kukabiliana na vita vyako vya kiroho.

Picha
kijana akiomba

Rais Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, aliahidi vijana kwamba Bwana atawalinda wanapobakia waaminifu. Unaposoma maneno yake, onyesha sehemu hizo zenye faraja kwako na ambazo unahisi zinakuhusu.

Picha
Rais Boyd K. Packer

“Vijana leo wanakuzwa katika maeneo ya adui kwa kiwango cha chini cha maadili. Lakini kama mtumishi wa Bwana, naahidi kwamba utakuwa salama na kulindwa kutokana na mashambulizi ya adui ikiwa utatii ushawishi unaotoka kwa Roho Mtakatifu.

“Vaa vizuri; zungumza kwa heshima; sikiliza muziki ya kuinua. Epuka uovu wote na mazoea binafsi ya udhalilishaji. Shikilia msimamo wa maisha yako na ujiweke kuwa jasiri. Kwa sababu tunakutegemea sana, utabarikiwa kiajabu sana. Kamwe hauko mbali na uwepo wa Baba yako wa Mbinguni mwenye upendo” (“Counsel to Youth,” Ensign or Liahona, Nov. 2011, 18).

Katika Alma 44:7–10, Zerahemna alitangaza kwamba hakuamini Mungu alikuwa ndiye chanzo cha nguvu ya Wanefi. Alijitolea kuwafanya Walamani kuacha silaha zao, lakini alikataa kufanya maagano ya amani. Soma majibu ya Moroni katika Alma 44:11. Fikiria ni kwa nini unafikiri ilikuwa muhimu kwa Moroni kuwafanya Walamani kufanya maagano ya amani.

Wakati wengi wa Walamani walifanya agano la amani, Zerahemna aliwarai salio la watu wake kukabiliana na jeshi la Moroni. Wakati Wanefi walipowaangukia Walamani na kuanza kuwaua, Zerahemna aliona kuwa maangamizo ja jeshi lake ilikuwa karibu na aliaahidi kuweka agano la amani (ona Alma 44:12–20).

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi utakavyotumia baadhi ya kanuni na kweli ulizojifunza katika somo hili ili kujilinda dhidi ya majaribu na mashambulizi ya adui na kukamilisha hamu zako zenye haki na malengo.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 43–44 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha