Seminari
Kitengo cha 15: Siku ya 2, Alma 5:37–62


Kitengo cha 15: Siku ya 2

Alma 5:37–42

Utangulizi

Alma alipokuwa akiendelea kuhubiri katika Zarahemla, aliwaonya watu kwamba uamuzi wao wa kuyasikia au kukataa maneno yake ulikuwa na baraka fulani au madhara. Aliwahimiza kusikia sauti ya Mchungaji Mwema, Bwana Yesu Kristo, aliyewaita na kutamani kuwarejesha tena katika zizi Lake. Unapojifunza somo hili, fikiria jinsi kufuata sauti ya Mchungaji Mwema kutakusaidia kuepuka mambo machafu ya ulimwengu na kurudi kuwa pamoja na Mungu.

Alma 5:37–42, 53–62

Alma anaalika wote kufuata Mchungaji Mwema, ambaye ni Mwokozi

Katika maandiko, Yesu Kristo wakati mwingine anajulikana kama “Mchungaji Mwema” (ona Yohana 10:11–15). Kwa nini unafikiri mchungaji ni ishara nzuri ya Mwokozi? Rais Ezra Taft Benson alitoa maelezo yafuatayo ya wachungaji wa kale:

“Katika nyakati za Yesu, mchungaji Mpalestina alijulikana kwa ulinzi wa kondoo wake. Tofauti na wachungaji wa kisasa, mchungaji daima alitembea mbele ya kundi lake. Aliwaongoza. Mchungaji alijua kila kondoo na kwa kawaida alikuwa na jina kwa kila mmoja. Kondoo alijua sauti yake na alimwamini na hangeweza kufuata mgeni. Hivyo, alipoitwa, kondoo angekuja kwake. (Ona Yohana 10:14, 16.)

“Wakati wa usiku wachungaji wangeleta kondoo wao kwenye boma liitwalo zizi la kondoo. Kuta ndefu zilizunguka zizi la kondoo, na miiba iliwekwa juu ya kuta hizi ili kuzuia wanyama mwitu na wezi kupanda juu.

Hakupoteza Tena

“Wakati mwingine, hata hivyo, mnyama pori aliyezidiwa na njaa angepanda juu ya kuta hadi ndani miongoni mwa kondoo, na kuwatisha. Hali kama hiyo ilitenganisha mchungaji wa kweli—yule aliyependa kondoo wake —na muajiriwa—yule aliyefanya kazi tu kwa ajili ya malipo na wajibu.

“Mchungaji wa kweli alikuwa tayari kutoa maisha yake kwa ajili ya kondoo. Angeingia miongoni mwa kondoo na kupigania maslahi yao. Muajiriwa, kwa upande mwingine, alithamini usalama wake binafsi zaidi ya kondoo na kila mara angekimbia wakati wa hatari.

“Yesu alitumia kielelezo hiki cha kawaida ya siku zake ili kutangaza kwamba Yeye alikuwa ndiye Mchungaji Mwema, Mchungaji wa Kweli. Kwa sababu ya upendo Wake kwa ndugu na dada Zake, Yeye angetoa maisha yake bure na kwa hiari kwa ajili yao. (Ona Yohana 10:17–18.)” (“A Call to the Priesthood: ‘Feed My Sheep,’” Ensign, Mei 1983, 43).

Andika majibu mafupi kwa maswali yafuatayo katika kitabu hiki cha kiada:

  • Ni nini kinaweza kutokea kwa kondoo ikiwa hawasikizi mchungaji?

  • Sisi ni kama kondoo kwa jinsi gani, na Mwokozi ni kama mchungaji wetu kwa jinsi gani?

  • Inamaanisha nini kuletwa katika zizi Lake? (ona Alma 5:60).

In Alma 5:37, Alma alielezea watu wa Zarahemla kama kondoo “waliopotea.” Soma Alma 5:37–42, na uangalie kile ambacho Alma alifundisha kuhusu kusikiliza sauti ya Mwokozi.

  1. ikoni ya shajaraAndika majibu kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Soma Alma 5:37–38, na ueleze kwa maneno yako mwenyewe kile ambacho Alma alifundisha kuhusu jitihada ya Mwokozi ya kutuita ili tumfuate.

    2. Katika Alma 5:41, Alma alifundisha nini kuhusu jinsi tunaweza kujua ikiwa tunasikiliza sauti ya Mchungaji Mwema? Ni “matendo gani mema” ambayo yanaweza kuonyesha kwamba kijana Mtakatifu wa Siku za Mwisho anafuata Mchungaji Mwema?

Kutambua na kufuata sauti ya Mwokozi daima si rahisi. Tafakari dondoo ifuatayo ya Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Wale Mitume kumi na Wawili: “Kutoka miongoni mwa sauti nyingi tunazosikia katika maisha, ni lazima tutambue sauti ya Mchungaji Mwema, ambaye anatuita tumfuate kuelekea nyumbani kwetu mbinguni” (“Alternate Voices,” Ensign, May 1989, 27).

Soma Alma 5:53–56, na uweke alama kwa tabia na vitendo vinavyofanya kuwa vigumu kwa mtu kuisikia sauti ya Mwokozi.

Fikiria kuhusu tabia au vitendo vingine ulimwenguni leo vinavyofanya kuwa vigumu kwa watu kuisikia sauti ya Mwokozi. Eleza kwa ufupi kwa nini unafikiri hizi tabia na vitendo vinafanya kuwa vigumu kwa mtu kusikia sauti ya Mwokozi:

Katika Alma 5:57, tia alama kwenye kishazi “nyote ambao mnatamani kufuata sauti ya mchungaji mwema.” Kisha tia alama kwenye vishazi vingine vitatu katika mstari wa 57 vinavyokuelezea kile unaweza kufanya ili kufuata sauti ya Mwokozi.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika mfano kwa kila mojawapo ya kauli tatu zifuatazo, zinazoonyesha kile ambacho kijana Mtakatifu wa Siku za Mwisho katika shule au jamii yako anaweza kufanya ili: (a) kujitenga na maovu, (b) kuwa tofauti, na (c) kutogusa vitu vichafu. Kisha fikiri juu ya shughuli mbili zenye haki au tabia ambazo zitawasaidia vijana vilivyo kuisikiliza sauti ya Mchungaji Mwema. Ikiwa moja ya shughuli hizi au tabia imekusaidia kusikia sauti ya Mwokozi, fikiria kuiandika katika shajara yako ya kujifunza maandiko ili kushiriki na mwalimu wako au darasa baadaye.

Kama ilivyoandikwa katika Alma 5:58–60, Alma alifundisha ukweli huu: Tukifuata sauti ya Bwana (Mchungaji Mwema), tutakusanywa katika ufalme Wake. Weka alama kwa ahadi au ya baraka katika Alma 5:58–60 ambazo wale ambao wamepokea urithi kwenye mkono wa kulia wa Mungu watapokea.

  1. ikoni ya shajaraFikiria kile kila moja ya ahadi au baraka hizi ulizoweka alama zinamaanisha kwako. Kisha andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu ni kwa nini unafikiri kujitenganisha na mambo maovu kunastahili baraka hizi.

Unapofuata sauti ya Mwokozi, utapokea baraka hizi na hatimaye kupata baraka ya kuinuliwa.

Alma 5:43–52

Alma anaeleza jinsi alipata ushuhuda na anafundisha kuhusu toba

Fikiria kuhusu kitu ulichojifunza kupitia kwa kila hisia zako tano: kuona, kusikia, kugusa, kunusa, na kuonja. Je, kuna njia ambayo unaweza kujua kitu bila kutumia moja ya hisia zako za kimwili? Soma Alma 5:45–48, na uangalie kile ambacho Alma alisema alijua na jinsi alikijua.

Weka alama katika Alma 5:48 kile Alma alifundisha kuhusu Yesu Kristo. Ujumbe wa Alma 5:45–48 unaweza kufupishwa kwa njia hii: Tunaweza kujua wenyewe, kwa njia ya Roho Mtakatifu, kwamba Yesu Kristo ni Mkombozi wa watu .

Kila mtu anakabiliwa na changamoto kwa imani na ushuhuda wake. Kuwa na ushuhuda wako mwenyewe wa ukweli wa injili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu kunaweza kukuimarisha nyakati zile za changamoto. Kukumbuka ushahidi wako mwenyewe wa Roho Mtakatifu, kama vile Alma, kunaweza kukusaidia kusimama imara katikati mwa changamoto. Kutoka kwa mfano wa Alma, tunaweza pia kujifunza kwamba kufunga na sala kunaweza kutusaidia kuhisi Roho akithibitisha ukweli na kuimarisha shuhuda zetu zinapohitajika kuimarishwa.

Mzee M. Russell Ballard

Tafakari ushuhuda wako mwenyewe unaposoma dondoo ifuatayo kutoka kwa Mzee M. Russell Ballard wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili ikituhimiza tutafute ushuhuda wetu wenyewe wa Yesu Kristo: “Ushuhuda binafsi, wa ukweli wa injili, hasa maisha matakatifu na utume wa Bwana Yesu Kristo, ni muhimu kwa uzima wa milele wetu. ‘Na uzima wa milele ndio huu,’asema Mwokozi, ‘Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma’[Yohana 17:3]. Kwa maneno mengine, uzima wa milele unatabiriwa juu ya maarifa yetu binafsi kuhusu Baba yetu wa Mbinguni na Mwanawe Mtakatifu. Kujua tu kuwahusu haitoshi. Lazima tuwe na uzoefu binafsi wa kiroho kututia nanga” (“Feasting at the Lord’s Table,” Ensign, Mei 1996, 80).

  1. ikoni ya shajaraKamilisha moja au zaidi ya shughuli zifuatazo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Andika kuhusu wakati uliposikia mtu akitoa ushuhuda wenye nguvu, na kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, kwamba Yesu Kristo ni Mkombozi wa mwanadamu. Andika jinsi ulivyohisi kusikiliza ushuhuda huu.

    2. Soma Alma 5:46, na kisha uandike kwa maneno yako mwenyewe jinsi Alma alivyopokea ushuhuda wake wa Yesu Kristo. Fikiria jinsi unaweza kufuata mfano wa Alma ili kusaidia kuimarisha ushuhuda wako wa Mwokozi, na uandike mawazo yako.

    3. Andika kuhusu wakati ulipohisi Roho Mtakatifu akikushuhudia kwamba Yesu Kristo ni Mkombozi wa ulimwengu. Andika lengo maalum ambalo litakusaidia kupata au kuimarisha ushuhuda wako wa Mwokozi, kama vile kufunga au kuomba kwa bidii zaidi au kusoma maandiko zaidi kwa makini. Fanya kazi ili kutimiza lengo hili, hata kama itachukua “siku nyingi” (Alma 5:46). (Kukamilisha shughuli hii inaweza pia kukusaidia kutimiza mahitaji ya Maendeleo ya Binafsi au Wajibu kwa Mungu.)

Soma Alma 5:49–52, na uangalie kile ambacho Alma alifundisha watu kuhusu toba. Juu ya mistari iliyotolewa, elezea ni kwa nini unafikiri watu wote ni lazima watubu ili kuishi milele na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo:

Mzee Dallin H. Oaks alitualika ili tufikirie maswali kadhaa ambayo yanaweza kutusaidia kuishi kile Alma alifundisha kuhusu toba na kujiandaa kuingia katika ufalme wa Mungu:

Mzee Dallin H. Oaks

“Je! Ikiwa siku ya kuja Kwake ni kesho? Ikiwa tunajua kwamba tungekutana na Bwana kesho —kupitia kwa kifo chetu cha mapema au kupitia kuja Kwake kusikotarajiwa —tungefanya nini leo? Ni maungamo gani tungefanya? Ni mazoea gani tungesitisha? Ni mambo gani tutasuluhisha? Ni msamaha gani tutatoa? Ni shuhuda gani tutatoa?

“Ikiwa tutafanya mambo hayo basi, kwa nini si sasa? Mbona tusitafute amani wakati amani inaweza kupatikana?” (“Preparation for the Second Coming,” Ensign au Liahona, Mei 2004, 9).

  1. ikoni ya shajaraFikiria kuhusu moja ya maswali za Mzee Oaks. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika ni kwa nini unafikiri ni muhimu kuishi kila siku kama kuwa unajiandaa kukutana na Bwana.

Fikiria kwa maombi jinsi unaweza kutenda kwa yale uliyojifunza leo ili uweza kuwa tayari kukutana na Mwokozi na kuingia katika ufalme Wake.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Alma 5:37–62 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: