Seminari
Kitengo cha 21: Siku ya 3, Alma 53, 56–58


Kitengo cha 21: Siku ya 3

Alma 53; 56–58

Utangulizi

Helamani na Kapteni Moroni alipigana na Walamani katika sehemu mbalimbali za nchi. Helamani alituma barua kwa Moroni akielezea vita vya majeshi yake na Walamani na kudhihirisha matumaini yake na maridhiko katika imani kubwa ya vijana askari 2060. Kwa sababu ya imani na ujasiri wa mashujaa hawa Wanefi, Bwana aliwasaidia kushinda vita na kuwabariki na uhakika na matumaini katika nyakati zao za taabu.

Alma 53; 56

Majeshi ya Antipo na Helamani yashinda jeshi lenye nguvu zaidi la Walamani.

Wakati Kapteni Moroni akipigana na Walamani katika sehemu moja ya nchi, Helamani aliongoza jeshi lake katika sehemu nyingine ya nchi. Pamoja katika jeshi lake walikuwa vijana 2,000 wana wa watu wa Amoni. Wazazi wa vijana hawa walikuwa wamefanya agano kamwe kutochukua silaha dhidi ya maadui zao tena, lakini wana wao hawakuwa wamefanya agano, ili kuweza kuwasaidia majeshi ya Wanefi (onaAlma 53:10–18).

  1. Chora mchoro ufuatao katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Soma Alma 53:18–21, na uangalie vishazi vinavyoelezea sifa walizokuza vijana hawa 2000 kabla ya huduma yao ya kijeshi. Orodhesha vishazi unavyogundua chini ya kichwa “Sifa zilizokuzwa kabla wa vita.” Unaweza kutaka kuweka alama vishazi hivi katika maandiko yako.

Picha
Stick Figure

Antipo, kiongozi wa kijeshi wa Wanefi, alikuwa amezidiwa kwa wingi na adui Walamani wakati yeye na jeshi lake lilipotetea sehemu zao za nchi. Antipo alifurahia wakati Helamani alipowaleta vijana askari 2000 ili kumsaidia (ona Alma 56:9–10).

Katika vita vyao vya kwanza dhidi ya adui, vijana askari 2000 waliwatorosha jeshi la nguvu la Walamani, na Antipo Kamanda wa Wanefi aliamrisha jeshi lake kulifuata jeshi ya Walamani kutoka nyuma. Jeshi la Antipo lililipata jeshi ya Walamani, ambalo lilisimama ili kupambana nao. Vijana askari, ambao walisonga mbele, waligundua kuwa Walamani waliacha kuwafuata. Hawakujua kama Walamani walikuwa wamesimama ili kuwadanganya kurudi ili waweze kuharibiwa au kama Walamani walikuwa wamesimama kwa sababu jeshi la Antipo lilikuwa limewapata kutoka nyuma. Kwa hiyo, Helamani hakujua ikiwa walipaswa kurejea nyuma na kushambulia Walamani. (Ona Alma 56:29–43.)

Soma Alma 56:43–48, na uangalie vishazi vinavyoelezea sifa ambazo vijana hawa walionyesha katika wakati muhimu wa vita. Orodhesha kile ulichopata katika shajara yako ya kujifunza maandiko chini ya kichwa “Sifa zilizodhihirishwa wakati wa vita” Unaweza pia kuchagua kuweka alama ya vishazi hivi katika maandiko yako.

Soma Alma 56:49, 54–56 ili uone kile kilichotokea wakati vijana askari 2000 waliporudi kupigana na Walamani. Angalia vishazi vinavyoelezea ukweli huu: Tunapotenda katika imani, tunaweza kupokea nguvu kutoka kwa Mungu.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa jinsi gani kuendeleza sifa za vijana askari kunakusaidia kutenda kwa imani unapokabiliana na hali za changamoto?

    2. Elezea wakati wewe (au mtu unayemjua) alipotenda kwa imani na kupokea nguvu kutoka kwa Mungu ili kwa mafanikio kushughulikia hali ngumu.

Alma 57

Jeshi la Helamani linaiteka tena miji ya Antipo na Kumeni

Picha
Vijana Askari Elfu Mbili

Helamani na jeshi lake walikuwa na uwezo wa kuiteka miji ya Antipo na Kumeni kutoka kwa Walamani. Wakati huu, Helamani alipokea askari zaidi kwa jeshi lake. Maelfu ya maaskari kutoka nchi ya Zarahemla walijiunga na jeshi, kama walivyofanya wana 60 zaidi wa watu wa Amoni (ona Alma 57:1–12).

Mara baada ya jeshi la Helamani kuuteka mji wa Kumeni, Walamani waliwashambulia tena. Jeshi la Helamani lilikabiliwa na mashindano makubwa, ambapo vijana askari 2060 walikuwa nguvu kubwa ya jeshi lote. Soma Alma 57:19–21 ili kugundua sifa kadha ambazo vijana askari walidhihirisha katika vita hivi. Unaweza kutaka kuongeza sifa hizi kwenye orodha ya “Sifa zilizodhihirishwa wakati wa vita” katika shajara yako ya kujifunza maandiko na kuziweka alama katika maandiko yako.

  1. Mojawapo wa sifa bainifu ya vijana askari ilikuwa kwamba walitii “kwa uhalisi” (Alma 57:21). Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Unafikiri inamaanisha nini kutii amri “kwa uhalisi”?

    2. Unadhani kutii maneno ya kamanda wao kwa uhalisi kuliwasaidiaje askari vijana kushinda vita vyao?

    3. Ni kwa jinsi gani kutii amri za Bwana kwa uhalisi kunakusaidia katika vita vya kiroho ulivyonavyo katika maisha?

Fikiria kuandika kanuni zifuatazo katika maandiko yako au katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Tunampotii Bwana kwa uhalisi, Yeye atatuimarisha katika vita tulivyonavyo katika maisha. Soma maelezo yafuatayo ya Mzee Russell M. Nelson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, aliyeelezea ni kwa nini kutii amri za Mungu “kwa uhalisi” ni muhimu sana:

“[Wewe] utakutana na watu ambao wanachagua ni amri gani watalishika na kupuuza zingine ambazo wanazochagua kuvunja. Mimi huita hii mbinu ya mghahawa ya utii. Tabia hii ya kuokota na kuchagua haitafanya kazi. Itatupelekea katika taabu. Ili kujiandaa kukutana na Mungu, mtu hutii amri Zake zote. Inahitaji imani kuzitii, na kutii amri Zake kutaimarisha imani hiyo.

“Utii unaruhusu Baraka za Mungu kutiririka bila kikwazo. Yeye atabariki watoto Wake watiifu na uhuru kutoka katika utumwa na taabu. Naye atawabariki na mwanga zaidi.

“… Utii kwa amri za Mungu utaleta ulinzi wa kimwili na kiroho” (“Face the Future with Faith,” Ensign au Liahona, May 2011, 34–35).

Soma Alma 57:25–27, ukiangalia baadhi ya sababu za kwa nini Bwana alionyesha uwezo Wake ili kulinda askari vijana. Ni nini kinachowavutia zaidi kuhusu askari vijana katika mistari hii?

Hata tunapokuwa wenye haki, Mungu hatatulinda kila mara kutokana na ugumu. Hata ingawa askari vijana walihifadhiwa kutokana na kifo, wote walijeruhiwa (ona Alma 57:25), na Wanefi wengine wengi wenye haki waliuawa (onaAlma 57:26). Hata hivyo, Mungu atatuimarisha kila mara wakati wa shida na kutubariki na mambo tunayohitaji. Hatimaye, atawapa baraka za milele kwa wale wote wanaotii maagizo Yake.

Alma 58

Majeshi ya Wanefi yanasubiri vifaa na kisha kuteka upya mji wa Manti

Picha
Wanaweka Matumaini yao katika Mungu

Mbali na vita walivyopigana na Walamani, jeshi la Helamani lilikabiliwa na aina nyingine ya dhiki. Vita vyao vilikuwa vikipiganwa umbali kiasi kutoka Zarahemla, ambayo ilikuwa kitovu cha serikali ya Wanefi. Jeshi la Helamani lilikuwa limeshinda vita vingine vigumu sana, lakini hawakupokea chakula, vifaa na askari wa ziada waliohitaji kutoka kwa serikali. Hawakujua ni kwa nini serikali haikuwa ikiwasaidia. (OnaAlma 58:7–9.)

  1. SomaAlma 58:10–12, na ujibu maswali yafuatayo:

    1. Ni nini Wanefi walifanya walipokabiliwa na hali hii ngumu?

    2. Ni kwa jinsi gani Bwana alijibu maombi yao ya kweli na sala?

    3. Kulingana na Alma 58:12, ni kwa jinsi gani hakikisho la Bwana liliwasaidia Helamani na jeshi lake?

Andika kanuni ifuatayo katika maandiko yako au shajara yako ya kujifunza maandiko: Tukimgeukia Mungu nyakati za shida, tunaweza kupokea hakikisho takatifu ambalo linaweza kuimarisha imani yetu na kutupa matumaini.

Licha ya udhaifu wa jeshi lake, Helamani na watu wake waliweza kuuteka mji wa Manti (onaAlma 58:13–41). Helamani alihusisha mafanikio yote ya jeshi na msaada wa Bwana (ona Alma 58:37).

Helamani aliendelea kustaajabu kwa mafanikio ya askari vijana. SomaAlma 58:39–40, na utafute maneno na vishazi vinavyoonyesha njia ambazo askari vijana walikuwa hodari wakati wa hali ngumu. Fikiria kuweka alama maneno haya au vishazi katika maandiko yako.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko juu ya wakati ulipomgeukia Mungu kwa msaada wakati wa shida na kuona msaada Wake.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaAlma 53; 56–58 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha