Seminari
Kitengo 22: Siku ya 4, Helamani 6–9


Kitengo 22: Siku ya 4

Helamani 6–9

Utangulizi

Kufuatia jitihada za kimisionari za Nefi na Lehi, Walamani waliongezeka kwa haki yao. Kwa bahati mbaya, wakati huo huo Wanefi walikuwa waovu na kuunga mkono wezi wa Gadiantoni, kusababisha Roho wa Bwana kuondolewa kutoka kwao. Nabii Nefi alitabiri kwamba ikiwa Wanefi waliendelea kuishi katika uovu, wangeangamia. Katika majibu, majaji wafisadi waliwachochea wengi wa watu kuwa na hasira dhidi ya Nefi, ilhali watu wengine walimtetea nabii kwa ujasiri. Kama ushahidi kwamba maneno yake yatatimia, Nefi alifunua kuwa jaji mkuu alikuwa ameuawa na ndugu yake. Wakati maneno ya Nefi yalipothibitishwa, baadhi ya watu walimpokea kama nabii.

Helamani 6

Walamani wanakuwa wenye haki na wanapigana dhidi ya wezi wa Gadiantoni, ilhali Wanefi wasaidia makundi ya siri

  1. Chora yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko, na kuacha nafasi ya kuandika juu na chini ya mchoro:

    Picha
    mshale wa juu

    Kama ulivyojifunza kitabu cha Helamani, umeona kwamba Wanefi walifanya maamuzi yaliyosababisha Roho wa Bwana kujiondoa katika maisha yao, ilihali Walamani walifanya maamuzi yaliyoalika Roho kuongeza katika maisha yao. Soma Helamani 6:1–5, 16–17, 34–36; angalia kile ambacho Walamani walifanya ambacho kilisababisha Roho wa Bwana kuongezeka; na uyaandike juu ya mshale wa juu. Katika mistari hiyo hiyo, angalia kile Wanefi walifanya ambacho kilisababisha Roho wa Bwana kupungua, na uyaandike chini ya mshale wa chini.

Kanuni muhimu tunayoweza kujifunza kutoka kwa Wanefi na Walamani ni: Tunapoamini katika na kutii maneno ya Bwana, atamimina Roho wake juu yetu. Kinyume cha kanuni hii ni kweli pia: Ikiwa hatuko tayari kuamini na kutii maneno ya Bwana, Roho wa Bwana atajiondoa kutoka kwetu.

Angalia kile ambacho umeandika kwenye mchoro katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Fikiria jinsi vitendo hivyo kwenye nusu ya juu ni mifano ya kuwa tayari kuamini na kutii maneno ya Bwana, ilhali yale ya chini ni mifano ya kuwa na moyo mgumu na kutokuwa na nia ya kusikiliza Bwana.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Chagua moja ya hatua ya kusaidia (juu ya nusu ya juu ya mchoro wako) ambayo unafanya au uliofanya katika maisha yako. Jinsi gani hatua hii imealika Roho Mtakatifu katika maisha yako?

    2. Tazama matendo kwenye nusu ya chini ya mchoro wako. Kwa nini unataka kuepuka kufanya mambo haya?

Chagua jambo moja unayoweza kufanya ili kukaribisha Roho wa Bwana kuongezeka katika maisha yako, na kujitahidi kuifanyia kazi katika wiki ijayo.

Helamani 7

Nefi ahubiri kwa Wanefi waovu na kuwamuru kutubu

Nabii Nefi alihudumu kama misionari katika nchi upande wa kaskazini kwa miaka sita. Alirudi nyumbani kwake baada ya kujaribu kuwafundisha Wanefi, ambao walikuwa wamekataa maneno yake na kubakia katika hali zao za uovu. Alivunjika moyo sana. Soma Helamani 7:6–11 ili kujifunza kile Nefi alifanya.

Baada ya watu kukusanyika kusikia Nefi akiomba juu ya mnara katika bustani yake, Nefi alianza kuwafundisha (ona Helamani 7:12–29). Aliwaonya juu ya matokeo ya maamuzi yao na kusisitiza kanuni hii:Tukikataa kutubu dhambi zetu, tutapoteza ulinzi wa Bwana na baraka za uzima wa milele.

Helamani 8:1–26

Majaji wafisadi wachochea watu kuwa na hasira dhidi Nefi

Ni mvuto gani unaokuvuruga kwa kusikiliza maneno ya manabii? Unapojifunza Helamani 8, angalia ufahamu katika kile unapaswa kufanya unapokabiliwa na mvuto kama huo.

Soma Helamani 8:1–6, ukiangalie jinsi majaji wa Nefi (ambao pia walikuwa wezi wa Gadiantoni) walivyofanya juu ya mafundisho ya Nefi. Unaposoma, tafakari maswali yafuatayo: Ujumbe mkuu wa majaji kwa watu ulikuwa gani? Kulingana na Helamani 8:4, kwa nini majaji hawakumkamata Nefi?

Fikiria juu ya kile ungependa kufanya ikiwa mtu angejaribu kukushawishi kupuuza yale manabii wamefundisha. Katika Helamani 8, baadhi ya watu walizungumza dhidi ya kile majaji walikuwa wakisema kuhusu Nefi. Soma Helamani 8:7–9, na ufikirie kusisitiza kile watu walisema kwa kusaidia Nefi.

Angalia Helamani 8:10, na utambue athari ambayo maneno yao ilikuwa nayo juu ya hali hiyo. Unaweza kutaka kuandika kanuni ifuatayo kando na Helamani 8:7–10: Tukikataa uovu, tunaweza kuuzuia kuendelea.

  1. Katika shajra yako ya kujifunza maandiko, andika mstari fupi ukielezea ni kwa nini unafikiri kanuni iliyoelezwa hapo juu ni muhimu katika siku zetu.

  2. Jibu moja ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Jinsi gani unaweza kukataa vishawishi vinavyojaribu kukushawishi kupuuza au kupinga mafundisho ya nabii?

    2. Ni njia gani inaweza kuwa sahihi ya kuongea dhidi ya vishawishi hayo na kuunga mkono manabii wa Bwana?

    3. Ni lini ambapo wewe au mtu unayemjua alisimama dhidi ya vishawishi kama hayo? Matokeo yalikuwa yapi?

Kama ilivyoandikwa katika Helamani 8:11–23, Nefi aliwakumbusha watu juu ya nabii baada ya nabii walioshuhudia juu ya Yesu Kristo. Aliwafundisha Wanefi kanuni hii: Tunapotumia imani katika Yesu Kristo na kuwa watiifu, tutapata uzima wa milele. Licha ya wingi wa manabii ambao mafundisho yao yalithibitisha maneno ya Nefi, watu walikataa Nefi na ujumbe wake. Soma Helamani 8:24–26, na utambue madhara zilizowakabili Wanefi ikiwa wangeendelea kukataa ushahidi wa manabii. Kisha utafakari maswali yafuatayo: Kwa nini unafikiri wale ambao hukataa ukweli mara kwa mara na kuaasi dhidi ya Mungu wanapitia madhara hayo makubwa?

Helamani 8:27–9:41

Nefi anafunua kuwa jaji mkuu aliuawa na ndugu yake

Kama ushahidi kwamba watu walikuwa katika hali ya dhambi na kwamba kile aliwaambia kuhusu maangamizi yao yapate kutimia, Nefi alifunua kuwa jaji mkuu wa Wanefi alikuwa ameuawa. Nefi pia alitangaza kwamba yule aliyeuawa na ndugu yake walikuwa washiriki wa wezi wa Gadiantoni. (Ona Helamani 8:27–28.)

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kanuni ifuatayo: Maneno ya manabii yatatimia. Fikiria kuwa wewe ni mpelelezi anayechunguza mauaji ya jaji mkuu. Pata majibu ya maswali yafuatayo kwa kusoma mistari katika mabano. Andika majibu yako katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

    Siku ya kwanza ya Upelelezi:

    1. Wakati watu watano walipochunguza madai ya Nefi, ni nini walipata? Kwa nini walianguka chini? (Helamani 9:1–5)

    2. Ni nani ambaye watu walishuku kuwa muuaji? (Helamani 9:7–8)

    Siku ya Pili ya Upelelezi:

    1. Ni nani aliyethibitishwa kukosa hatia? (Helamani 9:10–14, 18)

    2. Ni nani aliyeshitakiwa? (Helamani 9:16, 19)

    3. Ni ushahidi gani wa hatia yake ambayo Nefi alitoa? (Helamani 9:25–36)

    4. Ni nani alikuwa muuaji? (Helamani 9:37–38)

Fikiria kuwekea alama majibu ya maswali yafuatayo katika maandiko yako:

  • Kulingana na Helamani 9:5, ni nini ambacho wale watu watano ambao waligundua jaji mkuu aliyeuawa waliamini na kuhofia?

  • Kulingana na Helamani 9:36, ni nini Nefi alisema ambacho Seantumu atashuhudia kuhusu atakapokiri juu ya mauaji ya ndugu yake?

  • Kulingana na Helamani 9:39–41, ni kwa nini baadhi ya watu wanaamini Nefi?

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaHelamani 6–9 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha