Seminari
Kitengo 22: Siku ya 3, Helamani 5


Kitengo 22: Siku ya 3

Helamani 5

Utangulizi

Wanefi waliendelea katika uovu mpaka wengi wao walipochagua maovu badala ya haki. Wakiongozwa na maneno ya baba yao, Nefi na Lehi walijitolea wenyewe kwa kuhubiri Injili. Baba yao, Helamani, alikuwa amewafundisha kuhusu umuhimu wa kujenga maisha yao juu ya msingi wa Mwokozi. Baada ya kufundisha Wanefi, Lehi na Nefi walihubiria Walamani na wakatupwa gerezani. Baada ya Bwana kuwakombowa Nefi na Lehi kimiujiza kutoka gerezani, wengi wa Walamani waliongoka kwa injili.

Helamani 5:1–13

Helamani aliwafundisha wanawe Nefi na Lehi kukumbuka amri ya Mungu na nguvu za Yesu Kristo ili kuwasaidia

Soma maneno sita na vishazi vifuatavyo. Ili kukusaidia kukamilisha shughuli ifuatayo, jaribu kukumbuka kila mmoja wao. Utaulizwa kuziandika kutoka kwa kumbukumbu katika shajara yako ya kujifunza maandiko: familia, wazazi, Upatanisho wa Yesu Kristo, manabii, toba inaelekeza kwa wokovu, shika amri

  1. Funga mwongozo wako, na uandike maneno haya sita au vishazi katika shajara yako ya kujifunza maandiko kutoka kwa kumbukumbu.

Angalia majibu yako. Hebu fikiri kidogo kama ilikuwa rahisi au vigumu kukumbuka vishazi. Je, unafikiri ilileta tofauti kwamba uliambiwa kuwa utaulizwa kuandika vitu kutoka kwa kumbukumbu?

Picha
Rais Spencer W. Kimball

Soma taarifa ifuatayo kutoka kwa Rais Spencer W. Kimball na ufikiri ni kwa nini kumbuka ni neno muhimu sana tunapojaribu kuishi injili: “Unapoangalia katika kamusi kwa neno muhimu zaidi, unajua ni nini? Inaweza kuwa ni kumbuka. Kwa sababu ninyi nyote mmefanya maagano—mnajua nini cha kufanya na mnajua jinsi ya kuifanya—haja yetu kubwa ni kukumbuka” (“Circles of Exaltation” [address to Church Educational System religious educators, June 28, 1968], 5).

Leo utajifunza juu ya watu wawili walioleta tofauti katika maisha ya maelfu ya watu kwa sababu wao walikumbuka kweli walizofundishwa na baba yao. Wakati wa kozi ya somo la leo, tafakari kile unafikiri Bwana anataka ukumbuke.

Kama ilivyoelezwa katika Helamani 5:1–4, Nefi alijiuzulu kama jaji mkuu kwa sababu watu walikuwa waovu sana. Yeye na kaka yake Lehi walitaka kujitolea wakati wao wote kwa kuhubiri neno la Mungu. Walipoanza huduma yao, walikumbuka mafundisho ya baba yao, Helamani. Soma mistari zifuatazo na ufupishe katika nafasi iliyotolewa kile Helamani aliuliza wanawe kukumbuka. Unaweza pia kutaka kuwea alama neno kumbuka kila wakati linapotokea katika mistari hizi.

  1. Ili kukusaidia kuelewa vyema zaidi kile ambacho umesoma, jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Jinsi gani kukumbuka mifano ya haki ya watu wengine kutakusaidia kuchagua “kufanya yaliyo mema”? Helamani 5:7

    2. Unafanya nini ili kukumbuka Upatanisho wa Yesu Kristo?

Soma tena Helamani 5:12, ukiangalia vishazi vinavyounga mkono kanuni hii: Tukijenga msingi wetu juu ya Yesu Kristo, Shetani hatakuwa na mamlaka yoyote juu yetu. (Helamani 5:12 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kuiwea alama katika njia tofauti ili uweze kutambua katika siku zijazo.)

Picha
msingi wa ukuta wa Hekalu la Nauvoo

Fikiria kwamba uliombwa kuchora jengo ambayo kamwe hautaanguka. Fikiria kuhusu majibu ya maswali yafuatayo:

  • Ni aina gani ya msingi jengo kama lile linapaswa kuwa nalo?

  • Jinsi gani msingi imara inasaidia jengo kuhimili hali ya hewa, majanga ya asili, au mazingira mengine magumu?

  • Ni maneno au vishazi gani katika Helamani 5:12 zinaonyesha kwamba kujenga juu ya msingi wa Yesu Kristo, Mkombozi wetu, haitazuia mashambulizi ya adui lakini itakupa nguvu ya kuyashinda?

  1. Andika majibu kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Unafikiri ina maanisha nini kujenga msingi wa maisha yako juu ya mwamba wa Yesu Kristo? Unajitahidi vipi kufanya hivyo katika maisha yako?

    2. Ni lini umewahi kuhimili majaribu au majaribio kwa sababu msingi wa maisha yako ulikuwa ni Yesu Kristo?

    3. Unawezaje kuboreka katika kufanya Mwokozi msingi wa maisha yako?

Helamani 5:14–52

Bwana awalinda Nefi na Lehi gerezani na kuondoa giza kutoka kwa watekaji wao wanapomlilia Yeye na kutubu

Kama ilivyoandikwa katika Helamani 5:14–19, Nefi na Lehi walihubiri injili kwa nguvu nyingi katika nchi ya Zarahemla na kubatiza maelfu ya watu hapo. Kisha walisafiri katika nchi ya Nefi, ambayo ilikuwa nchi ya Walamani. Shughuli ifuatayo imeundwa ili kukusaidia kuelewa matukio ya ajabu ya Nefi na Lehi miongoni mwa Walamani.

  1. Chora chati ifuatayo kwenye kurasa nzima katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Kisha soma mistari katika kila sanduku na uchore picha rahisi au uandike muhtasari mfupi wa kile kila kikundi cha mistari zinaeleza.

    Nefi na Lehi miongoni mwa Walamani

    Helamani 5:20–21

    Helamani 5:22–25

    Helamani 5:26–28

    Helamani 5:29–34

    Helamani 5:35–39

    Helamani 5:40–44

Katika tukio hili wingu la giza linaweza kuwakilisha dhambi na nguzo ya moto unaozunguka kila mtu unaweza kuwakilisha Roho Mtakatifu.

Chambua mistari 28 na 34, na uandike jinsi watu walihisi wakati walipokuwa katika wingu la giza:

Chambua mistari 43 na 44, na uandike jinsi watu walihisi wakati walipozingirwa kwa nguzo ya moto:

Chambua mistari 41 na 42, na uandike kile watu walifanya ili kuondoa wingu la giza, au kwa maneno mengine, kutubu dhambi zao:

Soma Helamani 5:45–47, na utafakari ni kweli zipi unazojifunza juu ya toba na tukio hili. Kanuni moja ni: Tunapoonyesha imani katika Yesu Kristo na kutubu dhambi zetu, Roho Mtakatifu huijaza mioyo yetu kwa amani na furaha.

Katika Helamani 5:48–52 tunajifunza kuwa karibu Walamani 300 walikuwa sehemu ya muujiza huu na waliongoka kabisa kwa injili. Walienda na kuhudumia watu wao mpaka “sehemu kubwa ya Walamani” walikuwa pia wameongoka (Helamani 5:50). Haya waongofu kisha kuweka chini silaha zao za vita (Helamani 5:51) na waliwapatia Wanefi nchi ya umilki wao” (Helamani 5:52). Katika hali nyingi katika Kitabu cha Mormoni, watu walipata ardhi zao kwa njia ya vita, lakini katika hali hii Wanefi walipata ardhi zao kwa sababu adui zao walitubu na kukubali injili.

  1. Fikiria kama unahisi ikiwa una imani na furaha katika maisha yako. Fikiria juu ya mawingu yoyote ya giza ambayo inaweza kuwa katika maisha yako, kama vile dhambi ya kutotubu, ugomvi na familia au marafiki, au tu kushindwa kufanya mambo kama vile kusoma maandiko na kuomba mara kwa mara. Andika moja au zaidi ya haya katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Tafakari kile unaweza kufanya ili kufuata mfano wa Walamani katika Helamani 5, na uandike kile unaweza kufanya kukaribisha Mwokozi kuondoa mawingu ya giza ambayo yanaweza kuwa juu yako. Jinsi gani toba inaweza kuwa sehemu ya suluhu unayotafuta? Jinsi gani toba itakusaidia kujenga juu ya msingi wa Yesu Kristo?

Picha
ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko—Helamani 5:12

Soma Helamani 5:12, na utambue maneno yanayoonyesha picha za kuona kwako (kwa mfano, mwamba, msingi, upepo, mvua ya mawe, dhoruba). Ili kukusaidia kukariri mstari huu, chukua kipande cha karatasi na uandike juu yake herufi ya kwanza ya kila neno katika mstari, isipokuwa neno linaonyesha picha ya kuona. Kisha, mahali pa herufi, chora picha rahisi inayowakilisha neno hilo. Fanya mazoezi ya kukariri mstari ukitumia tu kipande chako cha karatasi. Weka karatasi yako mahali fulani utakapoiona mara nyingi ili kukusaidia kukumbuka kweli katika mstari huu.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Helamani 5 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha