Seminari
Kitengo cha 28: Siku ya 1, 4 Nefi 1


Kitengo cha 3: Siku ya 1

4 Nefi 1

Utangulizi

Baada ya ziara na huduma ya Yesu Kristo kule Amerika, watu walitumia mafunzo Yake na kufurahia miaka 200 ya umoja, ustawi na furaha. Hatimaye, hata kama, watu walianza kuwa na kiburi na wakawa waovu zaidi. Punde si punde wakagawanyika katika Wanefi na Walamani tena, na baada ya miaka 300, Wanefi na Walamani walikuwa wamekuwa waovu, pakibaki watu wachache tu wema.

4 Nefi 1:1–18

Watu wote walikuwa wameongoka na walikuwa na amani na furaha

Picha
wasichana watatu wakitabasamu

Ni nini kinachokusaidia kufurahia kwa kweli?

Unadhani ni nini tofauti kati ya vitu vinavyokuletea furaha ya muda na vitu vinavyoweza kukuelekeza kwa furaha ya kudumu? Soma 4 Nefi 1:16 ili kupata kile Mormoni aliandika kuhusu watu baada ya Mwokozi kuwatembelea. Unaweza kuamua kutia alama kishazi “kwa kweli hakujakuwa na watu ambao wangekuwa na furaha zaidi.”

  1. Andika kichwa Kusingekuwa na Watu Wenye Furaha Zaidi katika shajara yako ya kujifunza maandiko na uchore duara chini yake, kama ilivyoonyeshwa katika mchoro ufuatao. (Utaandika vitu ndani na nje kuzunguka duara.) Soma 4 Nefi 1:1–2, na utafute kitu kile watu walifanya kiwezesha furaha yao. Orodhesha yale uliyopata ndani ya duara.

Picha
duara

Kwa sababu watu walitumia mafunzo ya Mwokozi, walikuwa “wote wamemgeukia Bwana” (4 Nefi 1:2) na walifurahia furaha kuu.

Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alielezea jinsi uongofu na furaha zinahusiana pamoja. Unaposoma maneno yake, piga mstari kinachomaanisha kuongoka:

Picha
Mzee Richard G. Scott

“Furaha yako sasa na milele inategemea kiwango chako cha uongofu na mabadiliko ambayo huleta maishani mwako. Ni vipi basi unaweza kuongoka kwa kweli? Rais [Marion G.] Romney alieleza hatua ambazo ni sharti uzifuate:

“Ushirika Kanisani na uongofu hasa hayana maana sawa”. Kuongoka na kuwa na ushuhuda sio hasa kitu sawa vile vile. Ushuhuda huja wakati Roho Mtakatifu anapompa mtafutaji wa dhati ushahidi wa ukweli. Ushuhuda wa dhati hustawisha imani. Yaani, inavutia toba na utiifu kwa amri. Uongofu ni tunda ama zawadi ya toba na utiifu’ [katika Conference Report, Guatemala Area Conference 1977, 8–9].

“Ikielezwa kwa njia rahisi, uongofu ni tunda la imani, toba, na utiifu wa kila mara. …

“Uongofu wa kweli huzaa matunda ya furaha ya kudumu inayoweza kufurahiwa hata wakati dunia imo katika masumbuko na wengi hawana chochote ila furaha” (“Full Conversion Brings Happiness,” Ensign, Mei 2002, 25, 26).

  1. Soma 4 Nefi 1:2–3, 5, 7, 10–13, 15–18, na utafute maneno na vishazi vinavyoeleza kile watu walipitia kwa sababu kila mtu alikuwa ameongoka kwa Bwana. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika baadhi ya maneno na vishazi nje ya duara uliochora katika zoezi la awali.

Tunaweza kujifunza kutoka kwa kipindi hiki cha furaha tele na ustawi miongoni mwa Wanefi kwamba wakati kikundi cha watu kinaongoka kwake Bwana, huleta umoja na furaha.Unaweza kuamua kuandika kanuni hii katika maandiko yako karibu na 4 Nefi 1:16 au katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

Tafakari vile unafikiria ingekuwa ikiwa kila mtu karibu nawe angekuwa ameongoka kwa kweli kwa Bwana?

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni faida gani unadhani zinaweza kujia famila yako ikiwa kila mtu katika famila yako angeishi kama watu katika 4 Nefi?

    2. Fikiria kuhusu wakati maishani mwako ambapo umebarikiwa kwa kuwa sehemu ya kikundi kilichokuwa kimeungana katika haki—kama vile katika familia yako, jamii ama darasa, ama kundi la marafiki. Unadhani nini kilisaidia kikundi hiki kuungana katika haki? Wewe na wale uliokuwa nao mlipokea baraka gani?

4 Nefi 1:19–49

Uovu unarejea na kusambaa hadi watu wema wachache tu wanabaki.

Ni nini unafikiria kinaweza kuharibu jamii yenye furaha kama ile ya watu waliozungumziwa katika 4 Nefi walikuwa nayo?

  1. Andika kichwa “Angamizi la Jamii yenye Furaha” katika shajara yako ya kujifunza maandiko, na uchore duara chini yake, sawa na mchoro katika zoezi la kwanza. Soma 4 Nefi 1:20, 23–24, na utafute kile kilichoanza kuangamiza furaha na amani ya watu. Andika yale umepata katika duara.

Unaweza kuamua kuandika kauli ifuatayo ya Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza katika maandiko yako karibu na 4 Nefi 1:24 ama katika shajara yako ya kujifunza maandiko: “Kiburi ni adui mkubwa wa umoja” (“Our Hearts Knit as One,” Ensign ama Liahona, Nov. 2008, 70). Ni kwa njia gani unafikiri kiburi ni adui wa umoja?

Kauli ifuatayo kutoka kwa Rais Dieter F. Uchtdorf wa Urais wa Kwanza inatoa umaizi juu ya kiburi. Tia mstari vishazi ambavyo vinaelezea kwa nini kiburi ni angamivu hivi.

Picha
Rais Dieter F. Uchtdorf

“Kiburi ni dhambi kwa sababu kinakuza chuki na uhasama na kutuweka katika upinzani na Mungu na binadamu wenzetu. “Katika kiini chake, kiburi ni dhambi ya kulinganisha, kwani ingawa kwa kawaida huanza na “Tazama jinsi nilivyo bora na vitu vikuu nilivyofanya, kila mara huonekana kuishia na “Kwa hivyo mimi ni bora kuliko wewe”.

“Wakati mioyo yetu imejawa na kiburi, tunatenda dhambi mbaya, kwani tunavunja amri mbili kuu [ona Mathayo 22:36–40]. Badala ya kumwabudu Mungu na kumpenda jirani yetu, tunafunua lengo la kweli la ibada yetu na upendo —picha tunayoiona katika kioo. (“Pride and the Priesthood,” Ensign ama Liahona, Nov. 2010, 56).

  1. Soma 4 Nefi 1:25–27, 30–35, 38–45, na utafute maneno na vishazi vinavyoeleza madhara ya kiburi miongoni mwa watu. Andika maneno haya na vishazi nje ya duara katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwenye zoezi la 4.

Ukweli moja tunaweza kujifunza kutoka matukio haya ni kwamba dhambi ya kiburi huleta utengano na huelekeza kwa maovu makubwa zaidi.Unaweza kuamua kuandika kishazi hiki katika maandiko yako. Kiburi cha mtu moja ama watu wawili kinawezaje kuadhiri furaha ya kundi zima?

Zingatia ni nani katika hali zifuatazo anaweza kuadhiriwa vibaya na kiburi cha mtu moja:

  • Mshiriki katika Darasa la Wasichana hataki kusikiliza somo ambalo mwalimu ametayarisha kuhusu baraka zinazokuja kutokana na utiifu wa Neno la Hekima. Anahisi kwamba hahitaji kufundishwa tena kuhusu Neno la Hekima na anakuwa msumbufu na kukataa kushiriki katika darasa.

  • Rafiki kila mara anamtania ama kumdunisha mshiriki mwingine wa kikundi kwa sababu jinsi anavyojivalia inaonyesha kuwa hana pesa nyingi.

  1. Tafakari kama kuna ama hakuna vidokezo vya kiburi katika maisha yako mwenyewe. Inaweza kuwa na usaidizi kurejelea kauli ya Rais Uchtdorf unapotafakari. Fikiria juu ya kile unaweza kufanya ili kuepuka kiburi na kutafuta usaidizi katika kuongeza umoja na haki katika familia yako, jamii, darasa, ama kundi la marafiki. Andika mawazo na malengo yako katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 4 Nefi 1 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha