Seminari
Kitengo cha 14: Siku ya 2, Mosia 27


Kitengo cha 14: Siku ya 2

Mosia 27

Utangulizi

Mosia 27 husimulia uongofu wa Alma (mwana wa Alma) na wana wa Mfalme Mosia. Husimulia juu ya majaribio yao ya uasi kuangamiza Kanisa la Mungu, matembezi ya malaika, mabadiliko ya kimiujiza ya Alma, na juhudi za wavulana hawa ili kurekebisha madhara waliyokuwa wamefanya. Maelezo ya uongofu wa Alma yanasisitiza haja ya watu wote kuzaliwa tena na kuishi katika haki. Sura hii pia inaonyesha baraka za kuwaombea wale ambao wamechagua kutofuata injili ya Yesu Kristo.

Alma Amka

Mosia 27:1–23

Malaika anamwita Alma Mdogo na wana wa Mosia kutubu

Fikiria kuhusu wale unaowajua ambao hawana shuhuda za injili au wameanguka kutoka kwenye Kanisa. Ungefanya nini kama mmoja wao angekataa juhudi zako zote za kumsaidia? Tafuta umaizi wa swali hili unapojifunza leo.

Soma Mosia 27:8–10, na utambue jinsi aya hizi zinamwelezea Alma na wana wa Mosia. Alma na wana wa Mosia walikuwa wanajaribu kufanya nini kwa Kanisa na washiriki wake?

Ni sehemu gani ya maelezo ya Alma na wana wa Mosia iliyo wazi sana kwako? Kwa nini?”

Nyakati zingine, tunaweza kuhisi kujaribiwa kuamini kwamba watu fulani kamwe hawatabadilika na kuja kwa Bwana. Fikiria kuhusu mtazamo huu unapoendelea na kujifunza katika Mosia 27.

Soma Mosia 27:11–14, na uweke mstari kwa nini malaika alikuja kwa Alma na wana wa Mosia.

Mosia 27:14 hufunza kanuni hii: Bwana hujibu maombi yetu ya uaminifu kwa wengine. Unaweza kutaka kuandika kanuni hii katika maandiko yako karibu na Mosia 27:14. Sio kila mtu ambaye anahitaji kutubu na sio kila mtu ambaye kwake tunamwombea atapokea matembezi ya malaika. Bwana hujibu maombi yetu ya uaminifu kwa wengine kulingana na hekima Zake mwenyewe.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu moja au maswali yote mawili yafuatayo:

    1. Ni lini umewahi kuhisi kwamba maombi yako yameleta tofauti katika maisha ya mtu fulani?

    2. Kuamini kwamba Bwana hujibu maombi yetu ya uaminifu kwa niaba ya wengine kunaathiri vipi jinsi unavyoomba?

Tafakari jinsi unaweza kufananisha maelezo ya Alma na wana wa Mosia na maisha yako. Unaweza kuendelea kuwaombea wale unaowajua na kuwapenda ambao wanachagua kutenda kinyume na mafundisho ya Bwana. Unaweza kukumbuka kwamba Bwana husikia maombi yako na kujibu katika njia na wakati Wake mwenyewe na bado huruhusu kila mtu uwakala wake. Pia, kwa makini fikiria kuhusu maswali yafuatayo: Ni nani anaweza kuwa anaombea maslahi yako? Ni kwa jinsi gani Bwana anataka wewe ubadilike? Unahitaji kufanya nini ili mabadiliko hayo yatokee?

Soma salio la maneno ya malaika kwa Alma, kama ilivyoandikwa katika Mosia 27:15–16. Kumbuka kwamba malaika alizungumza “kwa sauti kama radi, iliyosababisha ardhi kutetemeka” (Mosia 27:11). Fikiria jinsi uzoefu huu ungekuathiri kama ungekuwa pamoja na Alma na wana wa Mosia.

Jinsi gani unaweza kufanya muhtasari wa ujumbe wa malaika?

Baba Yake Alifurahia

Baada ya ujumbe wa malaika, Alma hakuweza kusema. Akawa mdhaifu, na “alibebwa kama hajiwezi” (Mosia 27:19) hadi kwa baba yake. Wakati baba ya Alma aliposikia kile kilichotokea, “alifurahia kwani alijua kwamba ulikuwa ni uwezo wa Mungu” (Mosia 27:20). Aliwakusanya umati “ili ushuhudie yale ambayo Bwana alikuwa amemtendea mwana wake” (Mosia 27:21). Baba yake Alma aliwauliza makuhani wafunge na kuomba ili kwamba mwanawe aweze kupokea nguvu zake na uwezo wa kuzungumza (ona Mosia 27:22). Bwana alijibu maombi yao.

Mosia 27:24–31

Alma Mdogo na wana wa Mosia walitubu na kuzaliwa tena

Soma Mosia 27:23–24, 28–30 ili kugundua jinsi Alma Mdogo alibadilika kama matokeo ya tukio lake na malaika. Katika chati ifuatayo, andika maneno au vishazi kutoka kwa aya hizi ambavyo vinaelezea hali ya kiroho ya Alma kabla na baada ya mabadiliko ya moyo.

Kabla

Baadaye

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kishazi kimoja ambacho uliandika katika safu ya Baada ambacho unatumaini kitakuelezea wewe katika maisha yako yote. Elezea kwa nini.

Chambua Mosia 27:24, 28, na uweke alama kile Alma alifanya na kile Bwana alifanya ambacho kilibadilisha moyo wa Alma.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kwa nini ni muhimu kuelewa kile sharti tufanye tunapotafuta kubadilisha maisha yetu na pia kile Bwana atatufanyia sisi.

  2. ikoni ya shajaraJibu moja au maswali yote yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa jinsi gani Mosia 27 inaweza kuwasidia watu ambao wamevunjika moyo na kufikiria hawawezi kutubu na kuja kwa Bwana?

    2. Ni kwa jinsi gani Mosia 27 inaweza kuwasidia watu ambao wanaamini kwamba mtu fulani kamwe hatatubu na kuja kwa Bwana?

Soma Mosia 27:25–26, na utambue ni nani sharti abadilishwe kupitia Upatanisho —au kwa maneno megine, ni nani sharti azaliwe na Mungu.

Aya hizi zinafunza kanuni: Kila mmoja wetu sharti azaliwe tena kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo. Kuzaliwa na Mungu humaanisha kwamba Roho wa Bwana husababisha mabadiliko makuu katika moyo wa mtu ili kwamba yeye hana hamu tena ya kufanya maovu, badala yake ana hamu ya kutafuta mambo ya Mungu (ona Mosia 5:2). Alma na wana wa Mosia walipata mabadiliko makuu ya moyo upesi, lakini wengi wetu tunabadilishwa kupitia Upatanisho pole pole zaidi. Kuzaliwa na Mungu ni mchakato zaidi kuliko tukio.

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Je! Umebadilishwa vipi kupitia Upatanisho ulipotubu na kujaribu kila siku kumfuata Mwokozi?

    2. Ni kitu kimoja gani unaweza kufanya vyema ili kuja kwa Bwana na kuruhusu Upatanisho ulete tofauti katika maisha yako?

Mosia 27:32–37

Alma Mdogo na wana wa Mosia wasafiri kote katika nchi, wakiungama dhambi zao na kuimarisha Kanisa

Alma akihubiri

Aya zifuatazo utajifunza katika Mosia 27 zinaonyesha kanuni: Kutubu kikweli, mtu sharti afanye kila kitu kinachowezekana ili kurekebisha uharibifu alioufanya. Malipo humaanisha kufanya kile tunaweza kurekebisha madhara ya chaguo zetu mbaya na kurejesha kile kilichoharibiwa na matendo yetu. Kwa mfano, kama mtu aliiba kitu kutoka kwa jirani, kufanya malipo kungejumuisha kurudisha kitu kilichoibiwa. Soma Mosia 27:32–37, na utambue kile Alma na wana wa Mosia walifanya ili kufanya malipo kwa dhambi zao.

Andika jinsi mtu fulani angeweza kufanya malipo kwa dhambi zifuatazo:

  • Kumdanganya mzazi:

  • Kueneza udaku kuhusu mtu mwingine:

  • Kudanganya katika kazi za shule:

Unapofikiria kuhusu jinsi unaweza kubadilishwa kupitia Upatanisho, fikiria jinsi unaweza kutubu na kufanya malipo kwa dhambi zako.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Mosia 27na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: