Seminari
Kitengo cha 11: Siku ya 1, Maneno ya Mormoni–Mosia 2


Kitengo cha 11: Siku ya 1

Maneno ya Mormoni–Mosia 2

Utangulizi

Maneno ya Mormoni yanatumika kama daraja kati ya mabamba madogo ya Nefi na ufupisho wa Mormoni wa mabamba makubwa ya Nefi. Kiliandikwa takribani miaka 400 baada ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, kitabu hiki kina maelezo mafupi ya mabamba madogo ya Nefi ni nini na kwa nini Mormoni alihisi yalihitaji kujumuishwa pamoja na maandishi matakatifu. Maneno ya Mormoni pia hutoa umaizi wa thamani kwa nini Mfalme Benyamini alikuwa na ushawishi mkubwa kama huu kwa watu wake.

Mabamba madogo ya Nefi yalikuwa yanashughulikia sana mambo ya kiroho na huduma na mafundisho ya manabii. Mabamba makubwa ya Nefi yalikuwa sana sana na historia ya kilimwengu ya watu iliyoandikwa na wafalme, kuanzia na Nefi. (Ona 1 Nefi 9:2 4.) Kutoka wakati wa Mosia, hata hivyo, mabamba makubwa pia yanajumuisha vitu vya umuhimu mkubwa wa kiroho.

Mabamba ya Mormoni, au mabamba ya dhahabu yaliyotolewa kwa Joseph Smith, yalikuwa na ufupisho wa Mormoni kutoka kwa mabamba makubwa ya Nefi, pamoja na maelezo mengi. Haya Mabamba ya dhahabu pia yana uendelezo wa historia ya Mormoni na maongezo ya mwanawe Moroni.

mchoro wa daraja

Mosia 1 ni kumbukumbu za mafundisho ya Mfalme Benyamini kwa wanawe. Aliwafunza kwamba maandiko yatatusaidia kumkumbuka Mungu na kuweka amri Zake. Mfalme Benyamini alipokuwa anafikia mwisho wa maisha yake, alitamani kuongea na watu wake kuhusu huduma yake kama mfalme na kuwahimiza wawe watiifu kwa Mungu. Hotuba ya Mfalme Benyamini imeandikwa katika Mosia 2–5 na inaelezea mateso na Upatanisho wa Kristo, kazi ya haki na rehema, na haja ya kujichukulia juu yetu wenyewe jina la Kristo kwa agano. Hapo mwanzoni mwa hotuba yake, iliyoandikwa katika Mosia 2, Mfalme Benyamini alisisitiza haja ya kumhudumia Mungu kwa kuwahudumia wengine na hali ya furaha ya wale wanaoweka amri.

Maneno ya Mormoni 1:1–11

Mormoni anafunza kwamba Mungu alihifadhi kumbukumbu tofauti kwa kusudi la busara.

Mormoni Akifupisha Mabamba

Fikiria kuhusu wakati ulipohisi msukumo wa Roho kufanya jambo fulani. Je, ulijua jinsi kila kitu kingekuwa kama wewe ungefuata mnong’ono huu? Ni nini kilichokupatia azimio na imani ya kutenda juu ya mnong’ono huu?

Nabii Mormoni alikuwa ameamriwa na Mungu kufupisha kumbukumbu za watu wake, ambazo zilikuwa zimewekwa kwenye mabamba ya Nefi. Karibu miaka 385 Baada ya Kristo, alipokuwa karibu kumkabithi kumbukumbu zake zilizofupishwa mwanawe, Moroni, alifuata maongozi hata ingawa hakujua matokeo yake.

Mormoni alipata kitu fulani alipokuwa anapekua katika kumbukumbu hizo. Soma Maneno ya Mormoni 1:3 ili ugundue nini yeye alipata. (“Mabamba haya” humaanisha mabamba madogo ya Nefi, ambayo yalikuwa katika 1 Nefi hadi Omni.) Soma Maneno ya Mormoni 1:4–6, na ufikirie kuweka alama katika maandiko yako kwa nini Mormoni alikuwa amependezwa wakati alipogundua nini kilichokuwa katika haya mabamba madogo.

Soma Maneno ya Mormoni 1:7, na utambue kwa nini Mormoni alijumuisha haya mabamba madogo pamoja na ufupisho wake wa mabamba ya Nefi. Unaweza kutaka kuweka alama kanuni hii katika maandiko yako: “Bwana anajua vitu vyote.” Kwa kuelewa na kuamini katika kweli hii, unaweza kukuza imani ya kutii minong’ono kutoka kwa Roho Mtakatifu ambao unapokea.

Bwana alimwamuru Nefi atengeneze mabamba madogo na kuandika mambo matakatifu ya watu wake juu yake (ona 1 Nefi 9:3). Wakati huo, Nefi alitangaza, “Bwana ameniamuru kuandika hizi bamba kwa kusudi lake lenye hekima, ambalo kusudi mimi silijui. (1 Nefi 9:5).

mabamba ya dhahabu

Kusudi hili lilifanywa kuwa wazi karne nyingi baadaye, mnamo 1828, wakati Nabii Joseph Smith alianza kutafsiri mabamba ya dhahabu. Alitafsiri kwanza kurasa 116 za mswaada kutoka kwa ufupisho wa Mormoni wa mabamba makubwa ya Nefi, na kisha kurasa hizi zilipotea au kuibwa wakati Joseph alipomruhusu Martin Harris kuzichukua. Bwana alimwambia Joseph hasitafsiri tena sehemu iliyopotea kwa sababu watu waovu walipanga njama ya kubadilisha maneno kwenye kurasa zilizopotea na hivyo kukashifu uhalisi wa Kitabu cha Mormoni. Bwana alimwambia atafsiri historia iliyokuwa katika mabamba madogo, ambayo ilishughulikia kipindi hicho hicho. Historia hii ililenga zaidi kwenye vitu vitakatifu. (Ona M&M 10:10, 41–43; ona pia 1 Nefi 9:3–4.)

Uzoefu huu ni ushahidi muhimu kwamba Bwana anajua vitu vyote ambavyo vitakuja. Yeye alijua kwamba historia katika mabamba madogo ingehitajika, na Yeye alimpatia Mormoni msukumo wa kujumuisha mabamba haya pamoja na ufupisho wake.

Je, kujua ukweli huu kutakusaidia vipi wakati unapopokea minong’ono kutoka kwa Roho?

  1. ikoni ya shajaraElezea katika shajara yako ya kujifunza maandiko wakati ambao wewe au mtu mwingine unayemjua alitenda juu ya mnong’ono kutoka kwa Roho Mtakatifu hata ingawa wewe au wao hawakuweza kuelewa mnong’ono huo hapo mwanzo. Andika kuhusu jinsi unavyofikiria unaweza kujitayarisha vyema kutambua na kujibu minong’ono ya Bwana. Kumbuka kwamba unapokuwa mwaminifu kwa minong’ono ya Roho wa Bwana, Yeye atafanya kazi “ndani [yako] utende kulingana na nia yake” (Maneno ya Mormoni 1:7).

Maneno ya Mormoni 1:12–18

Mfalme Benyamini anawashinda Walamani na kutawala kwa haki

Mfalme Benyamini alikuwa mfalme wa haki ambaye alikabiliwa na vikwazo vingi wakati wa utawala wake, ikijumuisha vita na Walamani na mabishano ya kimafundisho miongoni mwa watu. Mfalme Benyamini aliongoza majeshi ya Wanefi “kwa nguvu za Bwana” dhidi ya maadui zao na hatimaye akadumisha amani katika nchi (ona Maneno ya Mormoni 1:13–14). Kwa usaidizi wa “watu wengi watakatifu,” alifanya kazi kukemea manabii waongo na walimu waongo ambao walikuwa wanasababisha mabishano miongoni mwa watu, kwa hivyo pia akadumuisha amani ambayo hutokana na wema (ona Maneno ya Mormoni 1:15–18).

Soma Maneno ya Mormoni 1:12–18, na ujaze katika mapengo hapo chini pamoja na nambari za aya ambazo zinafundisha vyema kweli zifuatazo:

  • Bwana huwaita manabii ambao wanaweza kuwaongoza watu kwa amani licha ya changamoto.

  • Tunaweza kupata amani kwa kufuata uongozi wenye maongozi ya manabii.

  • Kwa nguvu za Bwana, tunaweza kushinda changamoto.

Mosia 1:1–18

Mfalme Benyamini anawafundisha wanawe umuhimu wa maandiko

Fikiria maisha yako yangekuwa vipi kama wewe kamwe haungekuwa na maandiko ya kusoma, kujifunza na kufunzwa kutoka kwayo.

Mfalme Benyamini aliwafunza wanawe jinsi maisha yao yangekuwa magumu kama wao hawangekuwa na maandiko. Kama ilivyoandikwa katika Mosia 1:3–5, mara tatu alitumia njia tofauti za kishazi “kama si sababu ya vitu hivi [maandiko]” ili kuwasaidia wanawe kuelewa umuhimu wa maandiko.

  1. ikoni ya shajaraUnaposoma Mosia 1:1–8, tafuta baraka Wanefi wangepoteza kama hawangekuwa na maandiko. Linganisha kile umejifunza na Omni 1:17–18. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika sentensi tatu au nne kukamilisha kishazi kifuatacho: Kama nisingekuwa na maandiko …

Fikiria kuandika kanuni ifuatayo katika maandiko yako karibu na Mosia 1:1–8: Kupekua maandiko hutusaidia kujua na kuweka amri.

 Katika Huduma ya Mungu Wako

Mfalme Benyamini alifunza watu wake umuhimu wa kuwa waaminifu kwa amri na kuelezea kile hutokea kwa wale ambao wanakuwa waovu baada ya kuwa “watu hawa walio heshimiwa na Bwana zaidi” (Mosia 1:13). Soma Mosia 1:13–17, na ulinganishe Mosia 1:13 na Alma 24:30. Kisha tambua angalau matokeo matano ambayo huwajia wale ambao hugeuka kutoka kwa Bwana. Unaweza kutaka kuweka alama au nambari haya matokeo katika maandiko yako.

Mosia 2:1–41

Wanefi wanakusanyika kusikiliza maneno ya Mfalme Benyamini

Soma Mosia 2:1–9, na uandike majibu ya maswali yafuatayo:

  • Ni kina nani waliokusanyika pamoja?

  • Walikusanyika wapi?

  • Ni nini kilichofanywa ili umati mkubwa jinsi hii wa uweze kusikia maneno ya Mfalme Benyamini?

Ili kuelewa vyema silka ya Mfalme Benyamini, soma Mosia 2:11–15 na utambue vishazi ambavyo vinaonyesha Mfalme Benyamini alikuwa anazingatia wema na huduma badala ya hadhi na kutambuliwa.

Rais Howard W. Hunter

Kisha tafakari kauli ifuatayo ya Rais Howard W. Hunter: “Usijishughulishe sana na hadhi. Unakumbuka ushauri wa Mwokozi kuhusu wale ambao wanatafuta ‘kuketi mbele’ au ‘viti vya mbele’? ‘Naye aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu.’ (Mathayo 23:6, 11.) Ni muhimu kushukuriwa. Lakini malengo yetu yawe kwenye haki, wala sio kutambuliwa; juu ya huduma, wala si hadhi” (“Kwa Women of the Church,” Ensign, Nov. 1992, 96).

Jifunze Mosia 2:16–17, na uweke alama kanuni tunaweza kujifunza kuhusu huduma kutoka kwa Mfalme Benyamini: Wakati tunapowahudumia wanadamu wenzetu, tunamhudumia Mungu. (Mosia 2:17 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kukiweka alama kwa njia ya kipekee ili uweze kukipata hapo baadaye.)

Fikiria kuhusu wakati ambapo mtu alibariki maisha yako kwa kukuhudumia. Ulifanya nini (au ungefanya nini) kuonyesha shukrani zako kwa Mungu kwa mtu ambaye aliwahudumia wewe na Mungu kwa wema? Ulionyesha vipi shukrani zako kwa mtu huyu?

Baada kuwafundisha watu wake kuhusu haja ya kuwahudumia wengine, Mfalme Benyamini aliwafundisha njia nyingi ambazo kwazo Mungu hutubariki sisi na haja yetu ya kuwa na shukrani Kwake.

  1. ikoni ya shajaraUnapojifunza Mosia 2:19–24, 34, fikiria njia nyingi ambazo kwazo Mungu hukubariki wewe. Fikiria kuhusu jinsi wewe unaweza kuonyesha shukrani zako Kwake. Kisha jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini Mfalme Benyamini anajiita mwenyewe, watu wake, na sisi kama “watumwa wasio na faida”?

    2. Kwa nini ni muhimu kwetu kukumbuka deni letu kwa Mungu?

Maneno ya Mfalme Benyamini yanatufunza kwamba wakati tunahisi kuwa na deni kwa Mungu, tunataka kuwahudumia wengine na shukrani zetu huongezeka.

Katika Mosia 2:34, Mfalme Benyamini alifunza kwamba tunapaswa “kutoa” kwa Mungu yale yote tuliyonayo na tuliyo. Ku toa humaanisha “kutoa au kunyenyekea.” Unaweza kutaka kuandika maelezo haya karibu na neno hili katika maandiko yako. Tafakari jinsi unaweza kumpa Mungu yale yote uliyonayo na uliyo. Kumbuka kwamba unapoweka amri za Mungu na kutafuta kutoa huduma ya uaminifu, Yeye hukubariki kwa hayo.

Aya za mwisho za Mosia 2 zina onyo muhimu kutoka kwa Mfalme Benyamini kwa watu wake. Je! Umeshaona ishara ambayo inakwambia “tahadhari”? (Kwa mfano, ishara inaweza kukuonya kuhusu nyaya za umeme wa juu, miamba inayoanguka, wanyama mwitu, au mkondo mkali.) Soma Mosia 2:32–33, 36–38 ili ugundue kile Mfalme Benyamini aliwaambia watu wake wajihadhari nacho. (Neno ole katika aya ya 33 humaanisha “huzuni na dhiki.”) Andika sentensi inayoelezea kile kitatokea kwa wale ambao “wanamuasi Mungu kiwazi” (aya ya 37) au ambao wanavunja amri za Mungu kwa makusudi.

Soma kauli ifuatayo: “Baadhi ya watu kwa makusudi wanavunja amri za Mungu, wakipanga kutubu baadaye, kama vile kabla hawajaenda hekaluni au kuhudumu misheni. Dhambi ya makusudi kama hiyo hudhihaki Upatanisho wa Mwokozi ” (For the Strength of Youth [booklet, 2011], 29).

Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema juu ya umuhimu wa kutambua wakati tunaweza kuwa tunajiondoa wenyewe kutoka kwa Roho:

Mzee David A. Bednar

“Sisi tunafaa … kujitahidi kutambua wakati “tunajitenga [wenyewe] na Roho wa Bwana …’ (Mosia 2:36). …

“Kiwango ni wazi. Kama kitu tunakifikiria, kiona, kisikia, au tunakifanya kinatupeleka mbali na Roho Mtakatifu, basi tunapaswa kukoma kukifikia, kukiona, kukisikiliza, au kukifanya kitu hicho. Ikiwa kile ambacho kimedhamiriwa kuburudisha, kwa mfano, kinatutenganisha sisi na Roho Mtakatifu, basi hakika burudani ya aina hiyo si nzuri kwetu. Kwa sababu Roho hawezi kukaa na kile ambacho ni cha utovu, kichafu, au kisicho na maadili, basi kwa uwazi vitu kama hivyo si vizuri kwetu. Kwa sababu tunatenganishwa na Roho wa Bwana tunapojihusisha na shughuli tunazojua tunapaswa kuepukana nazo, basi vitu kama hivyo sio vizuri kwetu kabisa” (“That We May Always Have His Spirit to Be with Us,” Ensign or Liahona, May 2006, 30).

Tafakari kile watu wanapoteza—wakati mwingine bila hata kutambua—wanapojiondoa wenyewe kutoka kwa Roho. Soma Mosia 2:40–41, na utambue kile Mfalme Benyamini alitaka sisi tufikirie na kile alitaka sisi tukumbuke.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Andika baadhi ya matukio ambayo yamekufunza wewe kwamba kama umtiifu kwa Bwana, utabarikiwa yote kimwili na kiroho.

    2. Chagua sehemu moja ya maisha yako ambayo kwayo ungependa kuwa mtiifu zaidi kwa amri za Mungu. Andika lengo la kuboreka katika sehemu hio.

ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko—Mosia 2:17

Soma Mathayo 22:36–40; 25:40; na Mosia 2:17. Tengeneza orodha ya maandiko, unganisha, au yapange pamoja kwa kufanya marejeo mtambako maandiko haya kwa pamoja. Mbinu hii ya kujifunza maandiko itasaidia kufafanua maana na kupanua uelewa.

Eleza mshikano kati ya vifungu ambayo umeunganisha.

Tafakari maswali yafuatayo:

  • Ni lini umepata kuhisi kwamba unamhudumia Mungu kwa kumhudumia mtu mwingine?

  • Je! Ni vitu gani mahususi unaweza kumfanyia mtu katika maisha yako ambavyo Mwokozi angefanya kama Yeye angekuwa hapa?

  1. ikoni ya shajaraBaada ya kufanya zoezi la kukariri Mosia 2:17, andika kutoka akilini katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Maneno ya MormoniMosia 2 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: