Seminari
Kitengo cha 14: Siku ya 3, Mosia 28–29


Kitengo cha 14: Siku ya 3

Mosia 28–29

Utangulizi

Baada ya kuongoka kwao, wana wa Mosia walihisi hamu kubwa ya kuhubiri injili kwa Walamani. Mfalme Mosia aliunga mkono maamuzi yao, lakini yeye basi alibakia bila mrithi kwa kiti chake cha enzi na mlinzi wa kumbukumbu za kimaandiko. Alimpatia Alma (mwana wa Alma) jukumu la kutunza kumbukumbu. Badala ya kumchagua mfalme mwingine, yeye alianzisha mfumo wa waamuzi kama aina mpya ya serikali.

Picha
Mosia na wanawe

Mosia 28:1–9

Wana wa Mosia wana hamu ya kuhubiri kwa Walamani

Karibu na kila kauli hapo chini, pima hamu yako katika maeneo yafuatayo. Tumia ratili ya 1 mpaka 10 (1 ikionyesha “hamna hamu,” na 10 ikionyesha “hamu kubwa sana”).

  • Mimi nina hamu ya dhati ya kuwasidia wengine kupata furaha ya milele.

  • Mimi niko radhi kujitolea kuwasaidia wengine.

  • Mimi nina hamu ya kushiriki injili na wengine.

  • Kama wewe ni mvulana, tathimini hamu yako ya kuhudumu misheni ya muda. (Kama wewe ni msichana, unaweza pia kuchagua kutathimini hamu yako.)

Katika misheni yao Mosia 27:8–10, na utambue jinsi Alma na wana wa Mosia wangekadiriwa katika kauli zilizopo juu kabla ya uongofu wao.

Sasa soma Mosia 28:1–3, na utambue jinsi wana wa Mosia walibadilika katika maeneo yaliyotambuliwa hapo juu. Unaposoma, kumbuka kwamba neno angamia linalenga kupotea kiroho

Andika majibu yako ya maswali yafuatayo:

Ni na kina nani wana wa Mosia walitaka kushiriki injili?

Kutokana na kile ulichojifunza katika Kitabu cha Mormoni kufikia hapo, ni ugumu gani au hatari gani wana wa Mosia wangekabiliana nazo katika misheni kwa Walamani?

Soma Mosia 28:4, na ufikirie jinsi wewe ungeisema upya kwa maneno yako mwenyewe. Angalia jinsi uongofu wa wana wa Mosia ulishawishi hamu zao za kushiriki injili. Katika Mosia 28:1–4 tunajifunza kanuni hii: Uongofu wetu unapopata kina, hamu yetu ya kushiriki injili huongezeka.

Picha
Mzee Dallin H. Oaks

Soma kauli ifuatayo kutoka kwa Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili (unaweza kutaka kuiandika pembezoni mwa maandiko yako karibu na Mosia 28:1–4): “Uzito wa hamu yako ya kushiriki injili ni kiashirio kikuu cha kiasi cha uongofu wetu binafsi” (“Sharing the Gospel,” Ensign, Nov. 2001, 7).

Katika sentensi ya kwanza ya Mosia 28:4, weka alama jinsi wana wa Mosia walishawishika katika hamu zao za kushiriki injili. Fahamu kwamba Roho wa Bwana ana nafasi muhimu katika kuongeza hamu yetu ya kushiriki injili.

  1. Jibu moja ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Jinsi gani hamu yako ya kushiriki injili iliongezeka ulipoimarisha ushuhuda wako?

    2. Ni uzoefu gani katika maisha yako uliokuelekeza kutaka kushiriki injili na wengine?

    3. Kama hauhisi kwamba una hamu kubwa ya kushiriki injili wakati huu, unaweza kufanya nini kuimarisha hamu hiyo? (Soma Alma 17:2–3.)

  1. Fikiria mvulana ambaye ni muumini wa Kanisa lakini ana hamu kidogo au hana hamu ya kuhudumu misheni. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, mwandikie barua, ukipendekeza kile yeye angefanya ili kuongeza hamu yake ya kushiriki injili. Unaweza kutaka kukumbuka kile kilichoongezea kina uongofu wako hata kushiriki injili ya Yesu Kristo na upendekeze shughuli hizo hizo au uzoefu huo huo kwa mvulana huyu. Kumbuka unapoandika huo uongofu mkuu utaelekeza kwa hamu iliyoongezeka ya kushiriki injili pamoja na wengine.

Unapoendelea kujifunza Mosia 28, fikiria jinsi ungehisi kama mtu umpendae alitaka kuishi miongoni mwa watu wakatili ambao wanawachukia wale ambao si kama wao. Soma Mosia 28:5–9, na utambue kwa nini Mosia aliwaacha wanawe kwenda kwenye misheni hatari kama hiyo. Katika kitabu cha Alma, utajifunza kuhusu “wengi [ambao] wataamini maneno yao” (Mosia 28:7)—maelfu ya Walamani ambao waliongoka kama matokeo ya juhudi za wana wa Mosia.

Mosia 28:10–20

Mosia anatafsiri mabamba ya Wayaredi na anatoa kumbukumbu zote alizoweka kwa Alma

Salio la Mosia 28 limeandikwa kwamba Mfalme Mosia alikuwa anazeeka na alihisi haja ya kumchagua mtunza kumbukumbu takatifu atakayefuatia kabla yeye kufa. Kwa vizazi vilivyofuata viwili, mfalme alimpa mabamba mfalme aliyefuatia Kwa sababu wana wa Mfalme Mosia walikuwa wameenda katika misheni, yeye hakuwa na mwana wa kuridhi kiti cha enzi na kwa hivyo hakuwa na mtunzaji wa kumbukumbu. Kilichojumuishwa katika kumbukumbu hizi, ilikuwa ni mabamba ya Wayaredi, ambayo Mosia alitafsiri kwa uwezo wa Mungu (ona Mosia 28:11–19).

Picha
taji
Picha
mabamba ya dhahabu

Kama ungekuwa unachagua mtu wa kutunza kumbukumbu takatifu, ni sifa zipi ungetaka huyo mtu awe nazo?

Elezea jinsi ungehisi kama mtu angekuchagua wewe kutunza mabamba hayo.

Soma Mosia 28:20, na utafute jina la mtu Mosia alimchagua atunze mabamba hayo.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile uamuzi wa Mfalme Mosia unakufunza kuhusu mabadiliko ya moyo wa Alma. Ili kujibu swali hili, unaweza kuhitaji kurejelea matendo ya awali ya Alma, yaliyoandikwa katika Mosia 27.) Pia, elezea jinsi imani ya Mosia katika Alma inaweza kuwapa matumaini wale ambao walitubu.

Mosia 29

Watu wa Mosia walichagua mfumo wa waamuzi kama aina mpya ya serikali

Kama ilivyoandikwa katika Mosia 29, Mfalme Mosia alipendekeza kwamba serikali ya Wanefi haitaongozwa tena na mfalme, bali kwa mfumo wa waamuzi. Soma na ulinganishe Mosia 23:7–8 na Mosia 29:13, 16–18. Kulingana na maandiko haya, chini ya mazingira au hali gani mfumo wa ufalme (kutawaliwa na mfalme au malkia) ni aina nzuri ya serikali? Kwa nini Mosia aliwashauri Wanefi dhidi ya kuendelea na mfumo wao wa ufalme?

Picha
Alma kama mwamuzi

SomaMosia 29:11, 25, na uweke mviringo majibu yafuatayo ambayo yanaonyesha kile Mosia alisema kuhusu jinsi waamuzi wangewahukumu watu: (a) kwa rehema kuu, (b) kulingana na sheria, (c) kulingana na amri za Mungu, (d) kwa ukweli kabisa.

Soma Mosia 29:26, 30, 33–34, 37–38, na ugundue wajibu wa watu katika aina mpya ya serikali Mfalme Mosia alipendekeza.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa nini unaamini ni muhimu kwa kila mwananchi “abebe sehemu yake” katika kutumikia nchi yake (Mosia 29:34).

Alma aliteuliwa kuwa mwamuzi mkuu wa kwanza, na alitimiza wajibu wake kwa haki (ona Mosia 29:41–43).

Kwa maneno yako mwenyewe, andika kanuni moja uliyojifunza kutoka kwa Mosia 29

Kanuni moja sura hii inafundisha ni: Kila mtu ana wajibu wa kutetea sheria na viongozi wa haki.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko njia moja unaweza kutetea sheria na viongozi wa haki katika nchi yako.

  2. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaMosia 28–29 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha