Seminari
Kitengo cha 13: Siku ya 2, Mosia 19–20


Kitengo cha 13: Siku ya 2

Mosia 19–20

Utangulizi

Baada ya Alma na watu wake kutoroka kutoka kwa jeshi la Mfalme Nuhu, watu ambao walibakia na Nuhu walianza kupatwa na matokeo yaliyotolewa unabii na Abinadi. Simulizi za Wanefi katika nchi ya Lehi-Nefi hutukumbusha kwamba tunapokataa ushauri wa watumishi wa Bwana, tutapatwa na madhara makali. Kwa upande mwingine, wakati tunapotii manabii, tunafurahia amani na usalama hata katika majaribio yetu. Unapojifunza somo hili, fikiria kuhusu jinsi unaweza kupokea amani na usalama ambao huja kutokana na kusikia ushauri wa manabii wa kisasa wa Bwana.

Mosia 19–20

Wanefi katika nchi ya Lehi-Nefi walipata ukamilisho wa unabii wa Abinadi

Soma uzoefu ufuatao ulioshikirikiswa na Mzee David R. Stone, ambaye alikuwa anahudumu kama mshiriki wa Sabini, na ufikirie kuhusu umuhimu wa maonyo ya kiroho tunayopokea kupitia manabii:

Jumapili moja asubuhi tuliamka kwa siku maridadi katika Santo Domingo katika Jamhuri ya Dominika. Jua la Karibiani likikuwa linaangaza, na anga ilikuwa safi. Upepo mwanana ulikuwa unavuma, usiweze kutumua majani kwenye miti; ilikuwa joto na amani na tulivu. Lakini mbali huko baharini, kupita mfikio wa hisia zetu za kimwili siku ile, mwangamizi mkali alikuwa anakuja katika njia yetu, asiyetulizika na asiyezuilika. Kituo cha kimbunga, kilicho na majukumu ya kufuatilia, na kutabiri mapito ya Harikeni Georges, kilikuwa kila dakika kinatoa habari zilizopatikana katika Intaneti. Ilikuwa asubuhi ya amani, tulivu sana, kwa njia ya yale macho ya kuona katika anga, niliona mapito yaliyotabiriwa ya tufani, imelenga kama mshale katika kitovu cha Santo Domingo.

Katika masaa 48 tufani ilipiga kisiwa kwa ukali mwingi, ikiacha katika mapito yake maangamizo, majonzi, na vifo. …

Ukuu kama uharibifu na maangamizo na vifo kutoka kwa tukio kubwa la nguvu za asili inavyoweza kuwa, kuna hata majonzi mengi yanayosababishwa katika maisha ya watu na vimbunga vya kiroho. Hizi nguvu kali mara nyingi zinasababisha uharibifu mbaya sana kushinda vimbunga vya asili, kwa sababu zinaangamiza nafsi zetu na kutuibia sisi mwonekano wa milele na ahadi zetu. …

Sisi tunajiweka wenywewe katika mapito ya vimbunga hivi vya kiroho wakati tunapojihusisha na hasira, pombe, na dhuluma, ashiki na uasherati; uzinzi na picha za ngono; madawa, kiburi, ulafi, vurugu, kijicho, na uongo—orodha ni ndefu. …

Jamii ya Mitume Kumi na Wawili

“Lakini pia sisi tuna walezi wetu wa vimbunga vya kiroho, wale ambao wito wao ni kutazama na kuonya, kutusaidia sisi kuepuka uharibifu, maangamizo, na hata kifo cha kiroho. Walinzi wetu kwenye mnara wanajulikana kwetu kama mitume na manabii. Wao ndiyo macho yetu ya kiroho huko angani, na wanajua, kupitia maongozi na umaizi na akili halisi, njia hizi tufani zitaweza kuchukua. Wao wanaendelea kupaza sauti zao katika kuonya kutuambia madhara makali ya kuvunja amri za Bwana kwa makusudi na kwa utundu. Kwa makusudi kupuuza maonyo yao ni kualika dhiki, huzuni, na maafa. Kuwafuata wao ni kufuata watumishi wateule wa Bwana kwenye malisho ya kiroho ya amani na maridhawa” (”Spiritual Hurricanes,” Ensign, Nov. 1999, 31–32).

Chukua dakika moja na utafakari ni hatari gani umeshasikia manabii na mitume wakituonya kuzihusu. Maneno yao yanaweza kutulinda vipi dhidi ya “vimbunga vya kiroho”?

Mungu alimtuma Abinadi kuwaonya watu wa Lehi-Nefi kuhusu maangamizo ambayo yalikuwa yanakuja kama wao hawatatubu.

  1. ikoni ya shajaraNakili chati ifuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko, ukiacha nafasi ya kutosha kuandika chini ya kila rejeo:

    Unabii kuhusu watu wa Mfalme Nuhu (Mosia 12:1–2)

    Utimilifu (Mosia 19:10, 14–15; 20:20–21; 21:3–4, 8, 10–13)

    Unabii kuhusu Mfalme Nuhu (Mosia 12:3)

    Utimilifu (Mosia 19:18–20)

    A.

    B.

    Rejea unabii wa Abinadi kwa Wanefi katika nchi ya Lehi-Nefi kwa kusoma marejeo ya maandiko katika safu ya kushoto ya chati. Chini ya marejeo ya maandiko yanayofaa, andika matokeo Abinadi alisema Mfalme Nuhu na watu wake yatawapata kama hawatatubu. Hapo chini ya safu ya kushoto (A), andika jinsi unafikiria ungeweza kuwa ulihisi na kile ungefanya kama ungesikia maonyo ya Abinadi.

Kabla hujaanza kufanya kazi katika safu ya kulia ya chati, kamilisha shughuli iliyopo hapo chini katika kitabu cha kiada. Shughuli hii itakusaidia kujifahamisha zaidi na matukio ya Mosia 19–20 na kutambua utimilifu wa unabii wa Abinadi ulioandikwa katika sura hizi.

Unapojifunza Mosia 19–20, tia nambari matukio 11 yafuatayo katika utaratibu ambao yanatokea katika maandiko. Muhtasari wa sura hapo mwanzoni wa kila sura utatoa vidokezo vyenye usaidizi wa kukuongoza.

  • Gidioni atafuta kumuua Mfalme Nuhu.

  • Wanawake na watoto Wanefi wanawasihi Walamani wasiwaue.

  • Mfalme Nuhu anapatwa na kifo cha moto.

  • Jeshi la Walamani linakuja kwenye mipaka ya Shemloni.

  • Makuhani wa Mfalme Nuhu wanawatorosha (teka nyara) mabinti 24 wa Walamani.

  • Mfalme Mlamani anasihi jeshi lake liwanusuru watu wa Limhi.

  • Baadhi ya watu wa Nuhu wanatoroka kabla ya Walamani, wakiwaacha nyuma wanawake na watoto.

  • Limhi anawamuru watu wake wasimue mfalme Mlamani.

  • Kunakuwa na amani kati ya Wanefi na Walamani kwa miaka miwili.

  • Limhi anaahidi kwamba watu wake watalipa nusu moja ya mali yao kwa Walamani.

  • Wanefi wanazuia shambulizi la Walamani na kumteka mfalme Mlamani.

(Majibu ya shughuli hii yanapatikana hapo mwisho wa somo hili.)

  1. ikoni ya shajaraBaada ya kuweka kauli 11 nambari kwa ufanisi, rudi kwenye chati katika shajara yako ya kujifunza maandiko. Pekua maandiko katika safu ya kulia kwa utondoti kuhusu jinsi unabii wa Abinadi ulivyotimia. Andika utondoti huu katika chati yako katika safu ya kulia. Hapo chini ya safu ya kulia (B), elezea nini wewe umejifunza kuhusu matokeo ya kukataa maneno ya maonyo ya nabii.

Soma Mosia 20:21, na uweke alama kauli ya Gidioni ambayo inaonyesha uelewa wake kwamba kukataa maneno ya watumishi wa Bwana huleta kuteseka na huzuni.

Soma Mafundisho na Maagano 133:63, 70–72 ili kuona jinsi kanuni hii inatumika kwa wale katika siku za mwisho ambao hawatamsikia Bwana au watumishi Wake. Unaweza kutaka kuandika rejeo hili katika maandiko yako kama rejeo mtambuko kwa Mosia 20:21. Tafuta hotuba za mkutano mkuu wa majuzi katika magazeti ya Ensign au Liahona ya (matoleo ya Mei na Novemba) au kwenye LDS.org ili kupata maneno ya manabii kuhusu mambo haya.

Tafakari swali hili: Nini umesikia manabii wakifundisha majuzi ambacho kingewasaidia watu, familia, na mataifa kuepuka kuteseka na huzuni?

Ili kuona mfano wa huzuni na kuteseka ambako kunaweza kuja kutokana na kuwakataa manabii wa Bwana, tafuta matokeo ambayo Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema yangekuja kwa wale ambao wanajihusisha na picha za ngono:

Mzee Dallin H. Oaks

“Picha za ngono zinalemeza uwezo wa kufurahia uhusiano wa kawaida wa kimhemko, kimapenzi, na kiroho na mtu wa jinsia ingine. Hubomoa ulinzi wa maadili ambao unasimama dhidi ya tabia zisizofaa, mbaya, au tabia haramu. Dhamira inapopunguzwa fahamu, wateja wa picha za ngono wanaongozwa kufanya kile wanachoshuhudia, bila kujali madhara yake katika maisha yao na maisha ya wengine.

“Picha za ngono pia zinalevya. Zinalemaza uwezo wa kufanya maamuzi na “hunasa” watumiaji wake, kuwavuta tena kwa kuwanasa kwa zaidi na zaidi” (“Pornography,” Ensign or Liahona, May 2005, 89).

Fikiria baadhi ya mifano ya huzuni na mateso ambayo yanatokana na kupuuza ushauri wa manabii juu ya mada kama vile kamari, picha za ngono, Neno la Hekima, kudanganya, chale, kudunga vipini, kuvalia vibaya, au kufanya miadi kabla umri wa miaka 16.

  1. ikoni ya shajaraJibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Je! Kufuata ushauri kutoka kwa watumishi Bwana juu ya mada kama vile kuimarisha familia, kuishi sheria ya usafi wa kimwili, au kutii Neno la Hekima kunaweza kusaidia watu na familia vipi kuepuka baadhi ya mateso na huzuni wanayopata?

Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alishuhudia kwamba tunaweza kuwa na amani na kurudi katika uwepo wa Mungu kwa kuwafuata manabii:

“Mimi natoa ushuhuda wangu kwamba manabii wa siku hii wana uwezo wa manabii wa kale na wale manabii wengine wa kipindi hiki. …

“… Usalama wetu wa kiroho unategemea kugeukia sauti safi ya nabii wetu aliye hai. Kama tutasikiliza sauti yake na kutii ushauri wake, tutaweza kuishi kama vile Kristo angependa sisi tuishi na kuvumilia hadi mwisho ili kwamba siku moja, sisi pamoja na familia zetu, turudi katika uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni na Mwokozi wetu Yesu Kristo” (”Hear the Prophet’s Voice and Obey,” Ensign, May 1995, 17).

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu jinsi ungependa kujifunza kwako kwa Mosia 19–20 kuathiri jinsi unavyosikia ushauri wa manabii wa Bwana. Fikiria uzoefu kuhusu jinsi ulivyopokea amani na usalama wa kiroho kwa kufuata ushauri wa watumishi wa Bwana na uandike katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo mwisho wa kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Mosia 19–20 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Majibu ya shughuli za utaratibu: 1, 4, 5, 2, 8, 11, 3, 10, 7, 6, , 9.