Seminari
Kitengo cha 12: Siku ya 4, Mosia 15–17


Kitengo cha 12: Siku ya 4

Mosia 15–17

Utangulizi

Kumbukumbu ya mahubiri ya nabii Abinadi kwa Mfalme Nuhu na makuhani wake yanaendelea katika Mosia 15–17. Alishuhudia juu ya nafasi ya Yesu Kristo kama Mkombozi. Mmoja wa makuhani wa Nuhu, Alma, alimwamini Abinadi. Mfalme Nuhu alimtupa Alma nje ya maskani yake na kuamuru Abinadi achomwe moto hadi kufa. Abinadi alikuwa mkweli kwa Mungu katika hali zote.

Mosia 15–16

Abinadi anafunza kuhusu nafasi ya Yesu Kristo kama Mkombozi

Chukua dakika chache za kutafuta na kuweka mviringo maneno komboa, kombolewa, na ukombozi katika Mosia 15–16. Urudiaji wa neno katika umbo la maandiko kila mara inaashiria umuhimu wa jambo katika ujumbe wa mwandishi. Unapojifunza leo, angalia kile Abinadi alifunza kuhusu kukombolewa.

Ili kukusaidia kuelewa nafasi ya Yesu Kristo kama Mkombozi, fikiria mchoro ufuatao:

Picha
Stick Figure

Fikiria umevunja sheria na umehukumiwa kwa adhabu kali inayoruhusiwa na sheria. Labda adhabu inajumuisha faini kubwa, kifungo gerezani, au hata kifo. Unaweza kuhisi vipi ukikabliwa na adhabu kama hizo? Unaweza kufikiria njia yoyote ya kisheria na ya haki ya kuepuka adhabu hizi?

Andika Mimi chini ya neno Mkosaji na Haki chini ya neno Adhabu katika mchoro. Sote tumevunja sheria za Mungu wakati fulani na sharti turidhie madai ya haki. Madai ya haki yanahitaji kila mwenye dhambi apokee adhabu inayohusiana na dhambi.

Picha
Mzee Richard G. Scott

Soma kauli ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na uweke mstari chini ya matokeo mawili ya kuvunja sheria za Mungu: “Haki … inahitaji kwamba kila sheria iliyovunjwa iliridhishwe. Unapotii sheria za Mungu, unabarikiwa, lakini hamna ingizo la zaida linalopatikana ambalo linaweza kuokoa ili kuridhisha sheria ambazo unavunja. Kama isiposuluhishwa, sheria zilizovunjwa zinaweza kusababisha maisha yako yawe ya taabu na zinaweza kuzuia kurudi kwa Mungu” (“The Atonement Can Secure Your Peace and Happiness,” Ensign or Liahona, Nov. 2006, 42).

Matokeo ya uvunjaji wa sheria za Mungu yanajumuisha taabu na kutoweza kuishi na Mungu. Soma Mosia 15:1, 7–9, na uweke alama vishazi ambavyo vinaonyesha jinsi Upatanisho wa Mwokozi huridhisha madai ya haki.

Tumia kamusi kupata maelezo ya maneno yafuatayo:

Komboa (Mosia 15:1)

Kusihi (Mosia 15:8)

Kati(Mosia 15:9)

Unaweza kutaka kuandika sehemu ya maelezo haya karibu na aya.

Wakati mwingine watu wanakanganywa na maelezo ya Abinadi juu ya Yesu Kristo katika Mosia 15:2–5 kama (1) Mwana wa Mungu Baba na(2) kama Baba. Kauli ifuatayo ya Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili inaelezea uhalisi mtakatifu wa Yesu Kristo kwa njia hii: “Kama vile Abinadi alivyofundisha , Kristo ‘alizaliwa kwa nguvu za Mungu’ (Mosia 15:3) na kwa hivyo ana nguvu za Baba ndani yake. Zaidi ya huo uhusiano wa uzao mtakafitu, Kristo pia anakuwa kama Baba kwa vile yeye ni Muumbaji wa mbingu na dunia [ona Mosia 15:4], ni baba wa kuzaliwa kwetu tena kiroho na wokovu, na ni mwaminifu katika kuheshimu— na kwa hivyo kudai nguvu—za mapenzi ya Baba yake juu ya yale mapenzi yake mwenyewe” (Christ and the New Covenant [1997], 183–84).

Jifunze Mosia 15:5–7, ufikirie kuhusu gharama Yesu Kristo alilipa kukomboa wewe, au kusimama kati yako na madai ya haki. Kwenye mchoro hapo juu, andika Yesu Kristo kati ya Mkosaji na Adhabu.

Ni muhimu kuelewa kwamba Mwokozi hafuti madai ya haki bali husimama kati ya haki na sisi. Kama tukitubu, Yeye huridhisha madai ya haki kwa kuchukua adhabu kwa niaba yetu.

  1. Kamilisha shughuli zifuatazo katika shajara yako ya maandiko:

    1. Andika Wale Wanaochagua Kukombolewa (Mosia 15:11–12; 16:13). Kisha pekua Mosia 15:11–12; 16:13, ukitafuta ni nani watakao kombolewa. Elezea kile umepata.

    2. Andika Wale Ambao Wanakataa Kukombolewa (Mosia 15:26–27; 16:2–5, 12). Kisha pekua Mosia 15:26–27; 16:2–5, 12, ukitafuta kwa nini watu fulani hawatakombolewa. Elezea kile umepata.

  2. Ukitumia kile umejifunza katika kazi yako iliyopita, jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya maandiko:

    1. Ni nini kitakachoamua ni nani atakayekombolewa kutoka kwenye dhambi zao?

    2. Unajifunza nini kutokana na tofauti ya “nia” ya Yesu Kristo katika Mosia 15:7 na “nia” ya wale ambao wanafanya uovu katika Mosia 16:12?

Yesu Kristo huridhisha madai ya haki kwa wote wale ambao wanatubu. Gharama Mwokozi alilipa kwa ajili yetu ni zawadi ya kibinafsi kabisa kwa yeyote ambaye anachagua kutubu na kufanya mapenzi ya Baba. Soma Mosia 15:10, na uweke mstari chini ya kishazi “ataona uzao wake.”

Picha
Mzee Merrill J. Bateman

Soma Mosia 15:10–12 na kauli ifuatayo ya Mzee Merrill J. Bateman, mshiriki wa Sabini aliyeachiliwa na kubaki wa Heshima:

“Nabii Abinadi … anasema kwamba ‘nafsi yake kutolewa kama dhabihu ya dhambi ataona uzao wake’ (Mosia 15:10). Abinadi kisha anatambua uzao wa Mwokozi kama manabii na wale ambao wanaowafuata wao. Kwa miaka mingi nilifikiria juu ya uzoefu wa Mwokozi katika bustani na kwenye msalaba kama sehemu zile ambako mzigo mkubwa wa dhambi ulirundikwa juu Yake. Kupitia maneno ya Alma, Abinadi, Isaya, na manabii wengine, hata hivyo, maoni yangu yamebadilika. Badala ya mzigo mkubwa wa dhambi, kulikuwa na foleni ndefu ya watu, Yesu alipohisi ‘mambo yetu ya udhaifu’ (Waebrania 4:15), [ameyachukua] masikitiko yetu, huzuni zetu [na] alichubuliwa kwa maovu yetu’ (Isaya 53:4–5).

“Upatanisho ulikuwa uzoefu wa undani na kibinafsi ambao kwao Yesu alikuja kujua jinsi ya kumsaidia kila mmoja wetu” (“A Pattern for All,” Ensign or Liahona, Nov. 2005, 75–76).

Picha
Kristo katika Gethsemane
  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya maandiko:

    1. Unafikiria inamaanisha nini kuwa uzao wa Yesu Kristo? (ona Mosia 15:12).

    2. Unafanya nini kuhakikisha wewe unahesabiwa miongoni mwa uzao wa Yesu Kristo?

Unaweza kutaka kubinafsisha Mosia 15:10 kwa kuandika jina lako katika mahali pa “uzao wake” katika sehemu za aya ambayo umeweka mstari. Tafakari kwa dakika kile inamaanisha kuwa na Mkombozi ambaye amekuona na anakujua wewe kibinafsi.

Nini matokeo ya mtu anayekataa kukombolewa? Angalia tena katika Mosia 16:5. Ni nini kinatokea katika mchoro kilichoonyeshwa mapema katika somo hili kama mkosaji ataendelea katika dhambi na kukataa kutubu? Soma Mafundisho na Maagano 19:16–17 ili ugundue kile kitatokea kwa wale ambao wanaokataa kukubali kitendo cha ukombozi cha Mwokozi kupitia toba.

Abinadi alifunza kwamba ukombozi wa Yesu Kristo unajumuisha si tu kuokoa kutoka kwenye dhambi bali pia kutoka kwa kifo. Kila mtu atafufuka; hata hivyo, baadhi watafufuliwa kabla ya wengine. Abinadi alitumia maneno “ufufuo wa kwanza” ili kueleza kwamba wema na maasumu wangefufuliwa kabla ya waasi (ona Mosia 15:21–22). Wenye haki watakombolewa kutoka kifo katika ufufuo wa kwanza na waovu lazima wangojee kufufuliwa mpaka baada ya Milenia (ona M&M 76:85, 106).

  1. Tafakari juu ya aya ulizojifunza katika Mosia 15. Fikiria ungepata nafasi ya mjumbe kupeleka ujumbe kutoka kwako hadi Mwokozi. Andika kile ungemwandikia katika ujumbe huo, kulingana na kile Yeye amekufanyia wewe.

Mwokozi anataka kutuleta sisi tena katika uwepo wa Baba yetu wa Mbinguni. Yeye husihi, hupatanisha, na hutetea kwa niaba yetu. Mwokozi amelipa madai ya haki kwa ajili yetu kama sisi tutatubu.

Mosia 17

Alma anamwamini Abinadi na anatupwa nje; Abinadi auawa.

Je! Umewahi kushuhudia mtu akisimama kwa kile kilicho haki ambapo ilikuwa ni vigumu kwake kufanya hivyo? Matokeo yalikuwa nini?

Abinadi alipohitimisha ujumbe wake, mmoja wa makuhani, aliyeitwa Alma, alijaribu kumshawishi mfalme kuwa Abinadi alikuwa amesema ukweli na inapaswa kuachiliwa. Mfalme alimtupa Alma nje na kuwatuma watumishi wake wamuue. Alma alijificha na kuandika maneno ya Abinadi.

Kuongoka kwa Alma ni muhimu. Kwa sababu aliandika maneno ya Abinadi, vizazi vingi na watu wamebarikiwa. Matunda ya uongofu wa Alma yatakuwa wazi kabisa unapojifunza sura zijazo. Mfalme na makuhani wake walishauriana kwa siku tatu kabla ya kumhukumu Abinadi kifo (ona Mosia 17:1–6, 13).

  1. Mosia 17:7–10 na Mosia 17:11–12 linganisha chaguo zilizofanywa na Abinadi na Mfalme Nuhu. Baada ya kujifunza aya hizi, toa majibu mafupi kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya maandiko:

    1. Ni maneno gani ya Abinadi ya mwisho yalikupendeza wewe sana?

    2. Kwa nini unafikiri maneno ya Abinadi yalimwathiri Mfalme Nuhu kwa njia yalivyofanya?

    3. Ni ushawishi wa aina gani ambao makuhani walikuwa nao juu ya Mfalme Nuhu?

    4. Ni kwa jinsi gani mfano wa Abinadi unakupatia mvuvio wa kuwa mkweli kwa Mungu katika hali zote?

Rais Gordon B. Hinckley alitangaza: “Kuwa imara—katika kusimamia haki. Tunaishi katika kipindi cha masikilizano na ridhaa. Katika hali ambazo sisi kila siku tunakabiliwa nazo, tunajua kile kilicho cha haki, lakini chini ya shinikizo kutoka kwa wenzi wetu na sauti za ulaghai za wale ambao wanaotushawishi sisi, tunasalimu amri. Tunafanya masikilizano. Tunafanya ridhaa. Tunakubali, na tunaona aibu juu yetu wenyewe. … Sisi sharti tukuze nguvu za kufuata misimamo yetu” (“Building Your Tabernacle,” Ensign, Nov. 1992, 52).

Andika Mimi ninaweza kuwa mkweli kwa Mungu katika hali zote katika maandiko yako karibu na Mosia 17:9–12.

  1. Ili kubinafsisha ujasiri wa maadili na msimamo wa kibinafsi wa Abinadi, soma Mosia 17:20 na ukamilishe sentensi ifuatayo katika shajara yako ya maandiko: Ninahitaji kuwa mkweli kwa Mungu wakati …

Unapohitimisha somo la leo, fikiria kuhusu mwana familia au rafiki ambaye anaweza kufaidika kutoka kwa kusikia kile umejifunza na kuhisi leo. Kama inawezakana, shiriki naye kile umejifunza na hamu yako ya kuwa mkweli kwa Bwana wakati wa nyakati ngumu.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya maandiko:

    Nimejifunza Mosia 15–17 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha