Kitengo cha 14: Siku ya 1
Mosia 26
Utangulizi
Kama ilivyoandikwa katika Mosia 26, baadhi ya Wanefi wasioamini wa kizazi chipukizi waliwashawishi waumini wa Kanisa kwa maneno ya kubembeleza na kuwaelekeza wao kwenye dhambi. Alma aliomba ili kujua jinsi ya kuhukumu waumini hawa kulingana na mapenzi ya Mungu. Bwana alifunua kwa Alma jinsi ya kuwawajibisha waumini wa Kanisa kwa ajili ya dhambi zao. Bwana pia aliweka masharti ya toba. Alma alijifunza utayari wa Mungu wa kuwasamehe wale wanaotubu kwa kweli.
Mosia 26:1–6
Wengi wa kizazi chipukizi hawaanini , na wanatenda dhambi
Chukua dakika kufikiria kuhusu swali lifuatalo: Kwa nini unafikiria baadhi ya vijana hawana shuhuda au hawana shuhuda thabiti, hata wakati wameshawasikiliza manabii na kufunzwa na wazazi wao?
Mosia 26 hutoa umaizi wa swali hili. Jifunze aya na ujibu maswali katika chati ifuatayo (andika majibu yako katika kitabu cha kiada):
Ni vitu vitatu gani ambavyo wengi wa hiki kizazi chipukizi hakikuamini? | |
Kusoma maandiko au kusikiliza manabii kwa mtazamo wa kutoamini kunaweza kutuathiri sisi vipi? | |
Ni nini ilikuwa mojawapo wa sababu kuu watu hawa hawakuwa na imani katika Mwokozi na kujiunga na Kanisa? | |
Andika kanuni moja uliyojifunza kutoka kwa kujifunza aya hizi: |
Kishazi “mila za babu zao” katika Mosia 26:1 humaanisha kweli za injili zilizopitishwa kutoka vizazi vilivyopita; kishazi hiki wakati mwingine pia humaanisha mawazo ya uongo (kwa mfano, ona Alma 9:16). Mojawapo wa kanuni zilizofunzwa katika Mosia 26:1–4 ni: Hamu ya kuamini na juhudi za kibinafsi ni muhimu katika kukuza ushuhuda.
Soma kauli ifuatayo kutoka kwa Rais Henry B. Eyring wa Urais wa Kwanza, na uweke mstari matendo gani yaliyo muhimu ili kupata na kudumisha ushuhuda:
“Ushuhuda unahitaji kushamirishwa na maombi ya imani, kuwa na njaa ya neno la Mungu katika maandiko, na utiifu kwa ukweli tuliopokea. Kuna hatari katika kupuuza maombi. Kuna hatari kwa ushuhuda wetu katika kujifunza na kusoma maandiko kiholela tu. Kuna virutubisho muhimu kwa ushuhuda wetu. …
“Kusherekea neno la Mungu, maombi ya dhati, na utiifu kwa amri za Bwana sharti vitumike kwa usawa na kwa kuendelea ili ushuhuda wako ukue na kunawiri” (“A Living Testimony,” Ensign or Liahona, May 2011, 127).
Fahamu kwamba katika nyakati za Alma, wale waliokuwa katika kizazi chipukizi walikuwa hawafanyi vitu vilivyotajwa na Rais Eyring.
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Kutokana na uzoefu wako, kwa nini ni muhimu kuwa na mtazamo wa kuamini unapoomba, kusoma maandiko, na kujitahidi kutii amri?
-
Elezea uzoefu wa wakati maombi ya uaminifu, kusoma maandiko, au utiifu wa amri kuliimarisha ushuhuda wako.
-
Fikiria kwa dakika kama umewahi kuona watu wasio na shuhuda za injili wakiwashawishi washiriki wa Kanisa. Soma Mosia 26:5–6, utafute jinsi wasioamini walivyowashawishi wale walio katika Kanisa.
Unapoendelea kujifunza, inaweza kusaidia kujua maana ya kauli hii kutoka kwa Mosia 26:6: “Wale ambao walikuwa kanisani, na kutenda dhambi, waonywe [warudiwe na kurekebishwa] na kanisa.” Hii inamaanisha kwamba ilikuwa muhimu kwa washiriki wa Kanisa waasi wakuhumiwe kulingana na dhambi zao na kupewa nafasi ya kutubu.
Mosia 26:7–39
Alma anauliza jinsi ya kuhukumu wale ambao wanatenda dhambi
Ili kujitayarisha kujifunza salio la Mosia 26, fikiria wewe ni askofu wa kata ambayo inajumuisha baadhi ya waumini ambao wametenda dhambi nzito sana. Kama askofu, umepewa jukumu na Bwana la kuwawajibisha waumini hawa na kuwasaidia wao kutubu. Fikiria jinsi wewe ungewatendea hawa waumini na jinsi ungewasaidia vizuri zaidi.
Hali kama hii ilikuwa ngumu kwa Alma. Kama viongozi wa ukuhani wenye mamlaka leo, alikuwa na jukumu la kuwasaidia washiriki wa Kanisa ambao wametenda dhambi nzito kutubu, kupata msamaha, na kurudi katika ushiriki kamili na sifa nzuri katika Kanisa. Soma Mosia 26:7–14, na utafute jinsi Alma alifanya kwa hali hii na kile alifanya ili kupokea jibu kutoka kwa Bwana.
-
Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko, kwa nini ni muhimu kwetu kujua kwamba viongozi wa ukuhani wanatafuta na kupokea mwongozo wa Bwana wanapowasaidia wale waliotenda dhambi.
Kumbuka kwamba Alma alikuwa kuhani wa Mfalme Nuhu mwovu kabla ya uongofu wake. Soma Mosia 26:15–18, na utambue kile Alma na watu wake walikuwa wamefanya ili kurudi kwa Bwana na ni baraka gani Bwana alitoa kwao.
-
Soma Mosia 26:29–30. Kisha jibu moja au yote ya yafuatayo:
-
Elezea kwa nini unafikiria kanuni ifuatayo ni muhimu kwa kila mtu kuielewa, ikijumuisha yeyote ambaye anaweza kuwa alitenda dhambi nzito: Bwana atawasamehe wale ambao wanatubu kwa uaminifu wa mioyo yao.
-
Andika ushuhuda wako wa kanuni ifuatayo: Bwana atawasamehe wale ambao wanatubu katika uaminifu wa mioyo yao.
-
Baada ya Alma kuomba mwongozo kuhusu jinsi ya kusaidia waumini wa Kanisa ambao wametenda dhambi nzito, Bwana alimpatia maelekezo. Alikuwa awape waumini nafasi ya kutubu, lakini kama hawakutubu, walikuwa wasihesabiwe miongoni mwa watu wa Mungu. Maelekezo haya yanatoa umaizi muhimu katika kanuni ya toba. Soma Mosia 26:21–31, ukitafuta umaizi wa toba.
-
Ili kukusaidia kuchanganua kile unasoma katika aya hizi, jibu mawili au zaidi ya kazi zifuatazo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Jinsi gani ungefanya muhtasari wa maneno ya Mwokozi katika Mosia 26:23? Kwa nini unafikiria ni muhimu kwetu kutambua kwamba Mwokozi Mwenyewe alilipia dhambi zetu?
-
Ni vishazi gani katika Mosia 26:21–31 vinavyoonyesha matumaini na imani ya Mwokozi katika Alma kama kiongozi wa ukuhani? Je! Kuwa na usaidizi wa kiongozi wa ukuhani kunaweza kuwasidia wale wanaosumbuliwa na dhambi au majaribu magumu?
-
Nini unafikira inamaanisha kutubu “kwa uaminifu wa moyo [wa mtu]”? (Mosia 26:29).
-
Kwa nini unafikiria ni sharti tuwasamehe wengine ili tupokee msamaha wa Bwana? (ona Mosia 26:31).
-
Kwa maneno yako mwenyewe, andika kanuni ambayo umegundua katika Mosia 26:21–31:
Ingawa unaweza kuwa umetambua kanuni tofauti, au unaweza kuwa umetumia maneno tofauti, ifuatayo ni baadhi ya mifano ya kanuni zilizofunzwa katika Mosia 26:21–31:
-
Maaskofu na marais wa matawi wanamwakilisha Bwana katika kutusaidia kutubu na kupata msamaha.
-
Maungamo ya dhambi zetu yanaelekeza kwenye msamaha. (Dhambi zote sharti ziungamwe kwa Mungu, na dhambi nzito ziungamwe kwa kiongozi wa ukuhani ambaye anaweza kusaidia katika mchakato wa toba.)
-
Sisi ni sharti tuwasamehe wengine ili kupokea msamaha wa Bwana.
-
Ili kukusaidia kuchanganua kanuni hizi, soma utafiti ufuatao. Chagua utafiti mmoja na uandike katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi aya na kanuni ulizojifunza leo zinaweza kuwasaidia watu katika hali iliyoelezewa:
-
Msichana ametenda dhambi nzito, lakini anaogopa kusema na askofu wake.
-
Mvulana ana hamu ya kutubu, lakini hajui jinsi ya kufanya hivyo.
-
Msichana anarudia dhambi ambayo alikuwa ametenda mapema, na ana wasiwasi kwamba Bwana hatamsamehe kabisa.
-
Mvulana anaamua kutubu, lakini anakataa kumsamehe mtu ambaye amemuudhi.
-
-
Chagua kanuni moja uliotambua katika somo hili na utafakari jinsi ungeweza kuitumia kwa juhudi zako mwenyewe kutubu. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi utatumia kanuni hii.
Soma Mosia 26:37–39 ili kugundua kile kilitokea Alma alipokuwa akitekeleza ushauri wa Bwana. Uzoefu wa Alma na watu wake unafundisha kwamba tunapotubu na kuishi kwa haki, tunaweza pia kuwa na amani na ufanisi.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza Mosia 26na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: