Seminari
Kitengo cha 11: Siku ya 3, Mosia 4


Kitengo cha 11: Siku ya 3

Mosia 4

Utangulizi

Mafundisho ya Mfalme Benyamini yalikuwa na athari nzito kwa watu ambao walimsikia. Watu hawa walifanya imani katika Upatanisho, wakatubu, na wakapokea ondoleo la dhambi zao. Mfalme Benyamini kisha aliwafunza kile sharti wafanye ili kubakiza ondoleo la dhambi zao. Alitangaza kwamba sisi ni kama waombaji kwa sababu sisi tunamtegemea Mungu sana kabisa kwa wokovu wetu. Mfalme Benyamini alionya kwamba sisi sharti daima tuchunge fikra, mambo, na matendo.

Mosia 4:1–8

Umati ulishikwa na Roho na unapokea ondoleo la dhambi zao

Fikiria kwamba rafiki anakuuliza, Ninaweza kujua vipi kama nimesamehewa dhambi fulani? Ungemjibu vipi?

Jifunze Mosia 4:1–3, na utafute mawazo ya kukusaidia kujibu swali la rafiki yako. Andika jinsi unavyoweza kujibu:

Mojawapo wa kanuni zilizofunzwa katika aya hizi ni: Tunapofanya imani katika Yesu Kristo na kutubu kwa uaminifu, tunapokea ondoleo la dhambi zetu. Toba kama hiyo ni kitu muhimu katika kupata shangwe na amani ya dhamiri.

Kwa kawaida, mtu anapotuuliza swali tunataka kutoa jibu. Wakati huu, unapofikiria kuhusu jinsi ya kujibu swali la rafiki yako, fikiria jinsi unavyoweza kujibu swali kwa swali. Tafakari juu ya Mosia 4:1–3 na kauli ifuatayo ya Mzee F. Burton Howard, mshiriki aliyepumzishwa na kubaki wa Sabini: “Unapotubu kikamilifu, unahisi amani ya ndani. Unajua kwa njia fulani umesamehewa kwa sababu mzigo uliokuwa umebeba kwa muda mrefu, ghafula haupo tena. Umetoweka na unajua umetoweka” (“Repentance,” Ensign, May 1983, 59).

Fikiria swali unaloweza kumuuliza rafiki yako ili kumsaidia yeye kugundua jinsi tunaweza kujua kama tumesamehewa.

Inaweza kusaidia kuelewa maneno mawili katika Mosia 4:1–3 unapofikiria kuhusu swali la kuuliza. Kujiona wenyewe katika “hali ya kimwili” yetu humaanisha kutambua hali yetu ya kuanguka au ya yetu kilimwengu. Kujiona wenyewe kama “hafifu kuliko mavumbi ya dunia” humaanisha kwamba mavumbi ya dunia ni matiifu kwa amri za Mungu (ona Helamani 12:7–8), lakini watoto wa Mungu kila mara si watiifu kwa amri Zake.

Mfano wa kujibu swali la rafiki yako kwa swali unaweza kuwa hivi: Unahisi imani ya dhamiri unapofikiria kuhusu kuwa umetubu dhambi yako? Umejazwa na shangwe?

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Watu wa Mfalme Benyamini walisamehewa kwa sababu ya “imani tele waliyokuwa nayo katika Yesu Kristo” (Mosia 4:3). Ni matendo gani yaliyoandikwa katika Mosia 4:1–2 yaliyoonyesha imani yao? Ni mitazamo na hisia gani unazopaswa kuwa nazo ambazo zingekuwa zinafanana na zile za watu wa Mosia?

    2. Ni kwa jinsi gani unaweza kufanya imani yako katika Yesu Kristo unapotafuta ondoleo la dhambi zako?

Baada ya kushuhudia mitazamo ya toba ya watu wake, Mfalme Benyamini aliwafundisha baadhi ya vitu sharti wafanye ili kupokea wokovu. Unaposoma Mosia 4:4–8, tafuta kile sharti sisi tupokee wokovu.

Elezea au toa mifano ya jinsi unavyojaribu kufanya vitu Mfalme Benyamini alivyoelezea:

“Weka imani yako katika Bwana”:

“Awe mwenye bidii katika kushika amri zake”:

“Kuendelea katika imani hata hadi mwisho wa maisha [yako]”:

Mosia 4:9–30

Mfalme Benyamini anafunza jinsi ya kubakiza ondoleo la dhambi

Baada ya Wanefi kupokea ondoleo la dhambi zao, Mfalme Benyamini aliwafunza jinsi ya kubakiza (au kuwa na) hiyo hali safi na halisi. Pekua Mosia 4:9–11, 26, 28, 30, ukitafuta kile sharti tuamini na kufanya ili tubakize ondoleo la dhambi zetu. Andika kile unachogundua katika chati ifuatayo:

Kubakiza Ondoleo la Dhambi

Amini

Fanya

Mfalme Benyamini alifunza watu wake vitu vingi, kama ilivyoandikwa katika Mosia 4:9–30, lakini mojawapo wa kanuni muhimu sana alizofundisha : Kama tukijinyenyekeza wenyewe mbele za Mungu na kujitahidi kukuza sifa kama za Kristo, tunaweza kutunza ondoleo la dhambi.

  1. ikoni ya shajaraMfalme Benyamini alifunza kwamba sharti sisi “tuamini katika Mungu” (Mosia 4:9) na siku zote tukumbuke “ukuu wa Mungu” (Mosia 4:11). Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea ni uzoefu gani wewe au mtu unayemjua amepata ambao umekusaidia wewe kufahamu kwamba Mungu ni halisi, kwamba Yeye ni Mwenyezi, na kwamba Yeye anakupenda. Kwa nini unafikiria ni muhimu kuelewa na kukumbuka nguvu, wema na upendo wa Mungu? Unapokumbuka vitu hivi, ni kwa jinsi gani vinaathiri maisha yako?

Mfalme Benyamini alielezea matendo ya watu ambao wanajaribu kubakiza ondoleo la dhambi zao. Jifunze Mosia 4:12–16 ili ujifunze baadhi ya matendo Mfalme Benyamini alitambua. (Neno saidia katika Mosia 4:16 humaanisha kutoa msaada au usaidizi wakati wa mahitaji.)

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi matendo yaliyoelezewa na Mfalme Benyamini yanaonyesha kwamba mtu anajitahidi kubakiza ondoleo la dhambi zake. Je! Unaweza kuorodhesha matendo machache mengine ambayo yanaweza kuonyesha mtu anajitahidi kubakiza ondoleo la dhambi” Orodhesha njia moja au zaidi ambazo kwazo wewe umeweza kutoa usaidizi kwa wale walio na mahitaji.

Mfalme Benyamini alilinganisha kila mmoja wetu na mtu omba omba, kwani kila mmoja wetu anamtegemea Mungu kabisa kwa kila kitu tulich onacho. Analogia hii inaweza kukusaidia kuthamini baraka tulizopokea kutoka kwa Bwana. Soma Mosia 4:19–21, ukitafuta jinsi kila mmoja wetu ni kama muombaji katika macho ya Mungu.

Fikiria juu ya utegemezi wenu kwa Mungu. Ni baraka gani moja ambayo unaweza kumshukuru Baba wa Mbinguni wakati huu?

Baada ya kufundisha kwamba tuko daima katika haja ya usaidizi kutoka kwa Mungu, Mfalme Benyamini alituomba tufikirie jinsi tunapaswa kuwachukulia wale wanatuomba sisi msaada. Jifunze Mosia 4:26–27, ukitafuta jinsi tunapaswa kuwachukulia wale walio na mahitaji.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jibu lako kwa swali lifuatalo: Ni kwa jinsi gani kukumbuka mafundisho ya Mfalme Benyamini katika Mosia 4 kunaweza kukusaidia kuwa na huruma zaidi kwa wale ambao wana mahitaji ya kiroho na kimwili?

  2. ikoni ya shajaraChukua dakika kutafakari maandiko uliyojifunza leo. Je! Umeshahisi msukumo kutoka kwa Roho Mtakatifu kuhusu kile unapaswa kufanya, kulingana na kile umejifunza kutoka kwa mafundisho ya Mfalme Benyamini? Andika msukumo huu katika shajara yako ya kujifunza maandiko.

Kumbuka kwamba Bwana ana upendo mwingi kwako. Unapotubu makosa yoyote na kujitahidi uwezavyo kufuata mfano wa Mwokozi, unaweza kubakiza ondoleo la dhambi zako.

ikoni ya umahiri wa maandiko
Umahiri wa Maandiko—Mosia 4:30

Soma kwa sauti Mosia 4:30. Kuna uhusiano gani kati ya fikra zako, maneno yako, na matendo yako?

mchoro wa fikra

Rais Ezra Taft Benson alielezea uhusiano huu: “Fikiria fikra safi. Wale ambao wanafikiria fikra safi hawafanyi matendo machafu. Wewe hauwajibiki mbele ya Mungu kwa matendo yako tu bali pia kwa udhibiti wa fikra zako. Msemo wa kale bado ni kweli kwamba unapanda fikra na unavuna matendo, unapanda matendo na unavuna tabia, unapanda tabia na unavuna silka, na silka yako inaamua kudra yako ya milele. ‘Aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo’ (Ona Mithali 23:7.) (in Conference Report, Oct. 1964, 60).

  1. ikoni ya shajaraUnapojifunza kudhibiti fikra zako, utavuna baraka za kuwa zaidi kama Kristo katika maneno na matendo yako. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika njia moja au zaidi ambazo kwazo unaweza kudhibiti fikra zako na kuziweka zaidi kama za Kristo.

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Mosia 4 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: