Seminari
Kitengo cha 13: Siku ya 3, Mosia 21–24


Kitengo cha 13: Siku ya 3

Mosia 21–24

Utangulizi

Watu wa Limhi walikuja katika utumwa wa Walamani kama matokeo ya uovu wao (ona Mosia 20:21); walinyenyekezwa na wakamgeukia Mungu kama matokeo ya utumwa wao. Watu wa Alma waliletwa katika utumwa kama majaribio ya imani yao (ona Mosia 23:21). Makundi yote yaliomba sana ili waachiliwe kutoka utumwani. Hali makundi yote ya watu hatimaye yalikombolewa na kuwasili katika Zarahemla, Bwana alisaidia kila kundi katika njia tofauti. Kutokana na kujifunza majaribio na ukombozi wa kundi la Limhi, unaweza kuona Bwana atajibu maombi yetu katika njia Yake na wakati Wake mwenyewe tunapojinyenyekeza wenyewe. Kutokana na kujifunza majaribio na ukombozi wa watu wa Alma, unaweza kujifunza jinsi ya kumtegemea Bwana kwa nguvu katikati ya jitihada na changamoto zako mwenyewe.

Picha
Wanefi wakibeba gogo

Mosia 21–24

Wanefi katika nchi ya Lehi-Nefi wapata kuona utimilifu wa unabii wa Abinadi.

Fikiria kwamba uliishi katika nchi ya Lehi-Nefi wakati wa enzi ya Mfalme Nuhu na ukakataa mafundisho ya Abinadi. Sasa wewe na watu wako mko katika utumwa chini ya Walamani, kama vile Abinadi alivyokuwa ametoa unabii. Unafikiria ungefanya nini?

Sasa fikiria juu ya majaribio au dhiki ambayo inayokupata sasa. Soma aya zifuatazo katika maandiko yako, na uweke alama kile zinafundisha kuhusu kutafuta na kupokea ukombozi: Mosia 21:5, 14; 22:1–2; 23:23; na 24:21. Kukombolewa kwa kawaida humaanisha kuwa huru, kusaidiwa, au kutolewa kupitia kitu fulani.

Picha
Mzee Richard G. Scott

Unaposoma kauli ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, weka mstari chini ya vyanzo viwili anavyotoa vya majaribio na mateso tunakopata katika maisha yetu: “Hakuna mtu anayetaka dhiki. Majaribio, masikitiko, majonzi, na huzuni kubwa huja kwetu kutoka kwa vyanzo viwili tofauti vya kimsingi. Wale ambao wanaovunja sheria za Mungu daima watakuwa na changamoto hizo. Sababu ingine ya dhiki ni kutimiza madhumuni ya Mungu mwenyewe katika maisha yetu kwamba tuweze kupokea utakaso ambao huja kutokana na majaribio. Ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu kutambua kutoka kwa chanzo gani kati ya hivi viwili majaribio na changamoto zetu zinatoka, kwani tendo la urekebishaji ni tofauti sana” (”Trust in the Lord,” Ensign, Nov. 1995, 16).

Watu wa Limhi waliwekwa chini ya utumwa kwa sababu ya kutotii kwao, wakati watu wema wa Alma walipatwa na dhiki ambayo ingewatakasa. Watu wa Limhi walinyenyekezwa na kuletwa kwa Mungu kama matokeo ya utumwa wao. Kujifunza matukio haya mawili ya ukombozi mtakatifu kunaweza kukusaidia wewe kuongezea imani yako ya kumuomba Bwana kwa ukombozi kutoka kwa mateso yoyote unayopata.

  1. Katika chati hapo chini, swali la kwanza—Walikuja vipi katika utumwa?—limejibiwa kwa ajili yako. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu swali la pili: Walikombolewa vipi?

Watu wa Limhi

Watu wa Alma

Walikuja vipi chini ya utumwa?

(Mosia 20:21–22; 21:1–4)

Kwa sababu watu hawakutubu, Bwana aliwapa Walamani nguvu za kuwaleta watu utumwani.

(Mosia 23:1–4, 19–20, 25–38; 24:8–9)

Watu waliweka maagano yao, lakini wasalitiwa, wakatekwa, na wakateswa na watu waovu.

Walikombolewa vipi?

(Mosia 22:1–9, 13–14)

Mosia 24:17–25

Tafakari majibu ya maswali yafuatayo kuhusu watu wa Limhi:

  • Kulingana na Mosia 21:6, ushahidi gani ulikuwepo kwamba kundi la Limhi lilikuwa bado halijinyenyekeza wenyewe na kumgeukia Bwana? Hii inatofautiana vipi na jinsi watu wa Alma walivyojibu katika utumwa wao? Ukifikira sana juu ya tukio la kundi la Limhi, unajifunza nini ambacho kinaweza kukusaidia kujibu vilivyo majaribio yako mwenyewe?

  • Hata ingawa watu wa Limhi hawakukombolewa mara moja kutoka kwa mateso yao, ni kwa jinsi gani Bwana aliwabariki? (Unaweza kutaka kuweka alama kishazi “walifanikiwa nchini kiasi kwa kiasi” katika Mosia 21:16.) Je! Umeshawahi kuhisi kwamba Bwana amekusaidia kupitia majaribio kidogo kidogo kwa wakati?

  • Unafikiria mtazamo wa watu, walioelezewa katika Mosia 21:30–33, ulichangia vipi kwa ukombozi wao hatimaye?

  1. Chagua mojawapo wa kweli zifuatazo zinazopatikana kutoka kwa yale kile umejifunza kuhusu majaribio na ukombozi wa watu wa Limhi. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika aya ambayo inaelezea jinsi unavyoweza kutumia ukweli huo katika maisha yako mwenyewe.

    1. Tunapojinyenyekeza wenyewe, na kumwita Bwana, na kutubu dhambi zetu, Yeye atasikia maombi yetu na kurahisisha mizigo ya dhambi zetu katika wakati Wake mwenyewe.

    2. Tunapofanya maagano ya kumtumikia Mungu na kuweka amri Zake, Bwana atatupa njia ukombozi wetu.

Fikiria kuhusu mateso na ukombozi wa kundi la Alma unapojifunza kauli ifuatayo ya Mzee Richard G. Scott: “Wakati tu yote yanaonekana kuwa shwari, changamoto mara nyingi zinajitokeza kwa vipimo vingi vikitolewa kwa pamoja. Inapokuwa hayo majaribio si matokeo ya kutotii kwako, yanakuwa ni ushahidi kwamba Bwana anahisi wewe uko tayari kukua zaidi (ona Mithali 3:11–12). Kwa hivyo Yeye hukupa uzoefu ambao utasisimua ukuaji, uelewa, na huruma ambayo itakukwatua wewe kwa manufaa yako ya milele. Kukutoa kutoka pale wewe ulipo hadi kule Yeye anataka uwe kunahitaji kunyoroshwa sana, na hio kwa kawaida uleta maumivu na uchungu”

Weka alama maneno na vishazi katika Mosia 23:21–22 ambavyo vinaonyesha kwamba Bwana atajaribu subira na imani yetu ili kutusaidia sisi kuongeza imani yetu katika Yeye (ona pia M&M 122:5–7).

Andika majibu mafupi kwa maswali yafuatayo katika kitabu cha kiada chako:

  • Je! Wewe unafikiria nini lingekuwa jaribio gumu sana kuvumilia kama wewe ungekuwa miongoni mwa watu wa Alma wakati wa matukio yaliyoandikwa katika Mosia 23–24? Kwa nini?”

  • Je! Wewe unaweza kujifunza nini kutokana na njia Alma na watu wake walijibu majaribio yao? (Ona Mosia 24:1–12, 15–16.)

  • Ingawa Bwana hakuwakomboa mara moja watu wa Alma, Yeye aliwafanyia nini hapo mwanzoni? (Ona Mosia 24:15.)

Kanuni moja tunaweza kujifunza kutokana na uzoefu huu wa kundi la Alma ni kwamba tunapojiweka chini ya mapenzi ya Bwana kwa uvumilivu, Yeye atatuimarisha na kutukomboa kutoka kwenye majaribio yetu katika wakati Wake.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea kile unafikiria inamaanisha kujiweka chini ya mapenzi ya Bwana kwa uvumilivu wakati wa majaribio na jinsi kufanya hivyo kunaweza kukutayarisha kupokea nguvu na baraka Yeye atatoa kukusaidia kupitia ule wakati mgumu.

Hapo mwanzoni mwa somo hili, ulitakiwa kufikiria juu ya majaribio au dhiki zinazokukabili kwa sasa. Unapozikumbuka, fikiria kuandika majibu kwa maswali yafuatayo katika shajara yako ya kibinafsi au katika kipande cha karatasi tofauti:

  • Ni majaribio gani ninayokabiliana nayo katika maisha yangu?

  • Ninahitaji kufanya nini ili kujitayarisha mwenyewe kupokea nguvu za Bwana za ukombozi katika maisha yangu ?

  1. Andika yafuatayo mwisho wa kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza Mosia 21–24 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha