Seminari
Kitengo cha 32: Siku ya 2, Moroni 8–9


Kitengo cha 32: Siku ya 2

Moroni 8–9

Utangulizi

Moroni 8 ni waraka (barua) Mormoni alimwandikia mwanawe Moroni kuhusu sababu watoto wadogo hawahitaji ubatizo. Katika waraka, Mormoni alifundisha pia kuhusu jinsi tunaweza kujitayarisha kuishi na Mungu. Alihitimisha kwa kueleza wasiwasi kwa ajili ya uovu na uangamizi uliokaribia wa Wanefi. Moroni 9 ina waraka wa mwisho wa Mormoni ulioandikwa kwa mwanawe. Alieleza huzuni kwa ajili ya hali ya uovu ya Wanefi na alimuhimiza Moroni afanye kazi kwa bidii ili kusaidia Wanefi watubu. Bila kujali hali ya uovu ya watu wake, alimhimiza mwana wake kuwa mwaminifu katika Kristo na kuacha ahadi ya maisha ya milele ibaki kwenye akili yake milele.

Moroni 8:1–24

Mormoni alimwandikia mwanawe Moroni kuhusu wale wanaohitaji ubatizo.

Je, umewahi kushangaa ni kwa nini watoto katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho huwa hawabatizwi hadi wawe na umri wa miaka minane? Katika barua ilioandikwa kwa mwanawe Moroni, Mormoni alifundisha baadhi ya kweli muhimu kuhusu wokovu wa watoto wadogo na ubatizo, ikiwa ni pamoja na sababu watoto huwa hawabatizwi hadi wawe na umri wa miaka minane. Mormoni aliianza barua yake kwa Moroni kwa kuzungumza kuhusu ugomvi (kutokukubaliana) Wanefi walikuwa nao. Soma Moroni 8:4–6, na utafute fundisho Wanefi walikuwa wanabishana kuhusu. (Unaposoma, huenda ikasaidia kujua kwamba kubwa katika muktadha huu inamaanisha nzito sana.)

Soma Moroni 8:7, na utambue kile Mormoni alifanya aliposikia kuhusu shida hili. Mwokozi alijibu ombi la Mormoni kwa kueleza sababu watoto wadogo hawahitaji ubatizo kabla ya umri wa kuwajibika. Soma Moroni 8:8–9, na utafute kile Mwokozi alisema kuhusu ni kwa nini watoto wachanga na watoto wadogo huwa hawabatizwi.

Katika Moroni 8:8, “laana ya Adamu” inarejea utengano wa Adamu kutoka kwa uwepo wa Mungu kwa ajili ya Anguko. Hatimaye, baadhi ya Wanefi hawakuelewa fundisho la ubatizo. Hivyo basi, waliamini kimakosa kwamba watoto wadogo walikuwa hawastahili kuwa katika uwepo wa Mungu bila agizo la ubatizo, na walitaka kubatiza watoto walipokuwa wachanga sana. Katika kuelewa mstari huu, inaweza kusaidia kukumbuka kwamba dhambi ni “kutotii kwa kutaka amri za Mungu” (Guide to the Scriptures, “Sin,” scriptures.lds.org). Ili kuelewa fundisho katika mstari huu vyema zaidi, unaweza kutaka kurejelea Moroni 8:8 na makala ya imani ya pili.

Soma Moroni 8:10, na utafute maneno yanayokamilisha ukweli ufuatao: Toba na ubatizo ni muhimu kwa wote ambao .

Kwa sababu toba na ubatizo unahitajika tu kwa wale ambao wanawajibika na wanao uwezo wa kutenda dhambi, Mormoni alifundisha kwamba ni makosa kubatiza watoto wadogo kabla wawajibike. Soma Moroni 8:11–13, 18–22, na utafute elezo la Mormoni la kwa nini kubatiza watoto wadogo ni makosa. Mistari hii inafundisha fundisho hili: Watoto wadogo wameokolewa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Bwana ameweka umri ambapo uwajibikaji huanza— umri wa miaka minane (ona M&M 68:25–27; Joseph Smith Translation, Genesis 17:11 [in Bible appendix]). Kabla watoto wafikie umri wa miaka nane, hawawezi kutenda dhambi kwa sababu Shetani hajapewa nguvu ya kuwajaribu watoto wadogo (ona M&M 29:46–47). Makosa yoyote ambayo watoto hutenda kabla ya umri wa miaka nane hayazingatiwi kuwa dhambi.

msichana akibatizwa
Mzee Dallin H. Oaks

Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alieleza ni kwa nini watoto wadogo hawawezi kutenda dhambi: “ Tunaelewa kutoka kwa mafundisho yetu kwamba kabla ya umri wa kuwajibika mtoto ‘hana uwezo wa kutenda dhambi (Moro. 8:8). Wakati huo, watoto wanaweza kufanya makosa, hata makubwa sana na ya kuharibu ambayo lazima yarekebishwe, lakini matendo yao hayahesabiwi kama dhambi” (“Sins and Mistakes,” Ensign, Oct. 1996, 65).

Kama sehemu ya waraka wake, Mormoni pia alishuhudia kwamba, watoto wadogo “ni wazima katika Kristo” na kwamba wakifa kabla ya umri wa miaka minane, wanakombolewa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Moroni 8:12–15, 22).

Wakati akielezea ni kwa nini watoto wachanga na watoto wadogo hawana haja ya ubatizo, Mormoni alishuhidia kanuni hii: Mungu ni mwenye haki kikamilifu katika shughuli Zake na watoto Wake.Hii ina maana Mungu atahakikisha kwamba kila mmoja ana nafasi ya haki na usawa kwa kupokea wokovu.

  1. ikoni ya shajaraShughuli ifuatayo inaweza kukusaidia kujifunza kueleza mafundisho yanayofundishwa katika sehemu ya kwanza ya Moroni 8. Chagua moja (ama yote) ya hali ya hapo chini na, katika shajara yako ya kujifunza maandiko, tambua mstari moja au miwili kutoka Moroni 8:8–24 inayosaidia kujibu sikitiko la mtu katika hali hiyo. Kisha andika aya moja ama mbili ukikabiliana na hali hiyo. Tumia mistari ya maandiko katika jibu lako.

    1. Kama mmisionari, unakutana na mtu ambaye anatafuta ukweli kwa dhati. Anaeleza kwamba maisha yake yote alifundishwa kwamba watoto wadogo wana dhambi wanapozaliwa kwa sababu ya kosa la Adamu. Ana uhakika kwamba watoto wachanga wanapokufa bila kubatizwa, wao ni wenye dhambi na hawawezi kuokolewa .

    2. Mwogofu wa hivi karibuni anakubaliana kwamba ubatizo wa watoto wenye umri wa miaka minane ni wazo nzuri lakini anauliza, Hakika haijalishi kama watu wanabatizwa wakiwa na umri wa miezi minane, ama umri wa miaka minane, je, inajalisha?

Moroni 8:25–30

Mormoni afundisha kile ambacho lazima tufanye ili kuishi na Mungu.

Baada ya kufundisha kwa nini watoto wadogo hawana haja ya ubatizo, Mormoni alifundisha kwamba watu ambao wamefikia umri wa uwajibikaji lazima wabatizwe. Pia alielezea kile ambacho ni lazima tufanye baada ya ubatizo wetu ili kuishi na Mungu.

Soma Moroni 8:25–26, na utafute kile ambacho lazima tufanye na sifa lazima tukuze ili tuishi na Mungu. Huenda ukataka kuweka alama mambo haya katika maandiko yako. Inaweza kuwa na manufaa kuelewa kwamba “unyenyekevu” maana yake ni kuwa mtiifu kwa mapenzi ya Mungu, na “upole wa moyo” maana yake ni kuwa mnyenyekevu kwa kweli.

Huenda ukataka kuandika kanuni ifuatayo katika maandiko yako kando ya Moroni 8:25–26: Kupitia utiifu wa uaminifu kwa amri, tunaweza kupokea Roho Mtakatifu, ambaye anatutayarisha kuishi na Mungu.

  1. ikoni ya shajaraMaswali yafuatayo yatakusaidia kuelewa zaidi Moroni 8:25–26. Zingatia maswali yote, na kisha chagua mawili ama zaidi kati ya hayo kujibu katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kwa nini unafikiria kwamba kupokea ondoleo la dhambi zako kunaweza sababisha unyenyekevu na upole wa moyo?

    2. Kuwa mnyenyekevu na mpole wa moyo kunawezaje kualika Roho Mtakatifu maishani mwako?

    3. Kuwa na Roho Mtakatifu kutakusaidiaje kujitayarisha kuishi na Mungu?

    4. Mormoni alifundisha kwamba tukitaka kujazwa na upendo unaodumu, lazima tuombe kwa bidii. Kwa nini unadhani kwamba maombi kwa bidii yanahitajika ikiwa tunataka kujazwa na upendo?

Kama ilivyoandikwa katika Moroni 8:27, Mormoni alilaani dhambi ya kiburi miongoni mwa Wanefi. Soma Moroni 8:27, na utafute matokeo ya kiburi cha Wanefi. Kisha linganisha matokeo haya na matokeo ya kuwa mnyenyekevu na mpole wa moyo, yanayopatikana katika Moroni 8:26.

Mormoni alimhimiza Moroni awaombee Wanefi ili kwamba pengine wangetubu na kupokea baraka alizoelezea katika barua yake (ona Moroni 8:28–30). Ukitumia ushauri wa Mormoni kwa mwanawe, zingatia kuwaombea watu maalum unaojua wanahitaji kupokea baraka za injili, na utafute kupata njia za kuwasaidia watu hao.

Moroni 9:1–20

Mormoni aelezea uovu wa Wanefi na Walamani

Kumbuka wakati ulijaribu kumsaidia mtu na mtu huyo akakataa juhudi zako. Watu fulani wanaweza kuchukuliaje wakati nia zao nzuri zinakataliwa mara kwa mara na wale wanaojaribu kusaidia? Unaposoma waraka wa pili wa Mormoni kwa mwanawe Moroni, unaopatikana katika Moroni 9, tafuta kile Mormoni alichosema ili kumhimiza mwanawe asife moyo juu ya Wanefi.

Soma Moroni 9:1, na utafute neno Mormoni alitumia kuelezea hali atakayojadili katika barua yake. Kumbuka kwamba mazito katika muktadha huu linamaanisha jambo linalokera kabisa. Kama ilivyoandikwa katika Moroni 9:2–19, Mormoni alielezea baadhi ya mambo yanayokera sana yaliyokuwa yanatendeka miongoni mwa watu, kuonyesha jinsi watu walivyokuwa waovu. Kama Etheri, aliyekuwa nabii miongoni mwa Wayaredi, Mormoni alishuhudia hasira na uovu uliokuwa umewashinda watu wake. Aliogopa kwamba Roho wa Bwana alikuwa ameacha kuwa nao (ona Moroni 9:4).

Tafakari ni kwa nini Mormoni aliendelea kufanya kazi miongoni mwa Wanefi ingawa walikuwa wamefanya mioyo yao kuwa migumu kwa neno la Mungu na kukataa juhudi za manabii za kuwasaidia.

Mormoni alimpa Moroni baadhi ya ushauri wa nguvu kuhusu jinsi alivyopaswa kuwatumikia watu ambao mioyo yao ilikuwa haijafunguka. Soma Moroni 9:3–6, na ualamishe maneno na vishazi vinavyofundisha kanuni hii: Tunapaswa tufanye kazi kwa bidii katika huduma ya Mungu hata ikiwa wale tunaowatumikia hawaipokei. Mstari wa nb}6 ni muhimu hasa katika kufundisha kanuni hii.

Moroni 9:21–26

Mormoni anamhimiza Moroni awe mwaminifu

Fikiria juu ya matukio ya hivi karibuni katika jamii yako, taifa, au dunia ambayo watu wanaweza kuhisi kukata tamaa juu yake. Soma Moroni 9:25–26 kugundua ushauri Mormoni alimpa Moroni kuhusu kile cha kufanya katika hali za kukatisha tamaa.

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Mormoni alimwambia Moroni ni nini kinafaa “kuwa katika akili yake milele”? (Moroni 9:25). Kumkumbuka Mwokozi na Upatanisho Wake kunawezaje kukusaidia wakati uko katika shida ama umezingirwa na uovu?

Kutoka kwa ushauri wa Mormoni kwake Moroni, tunaweza kujifunza kanuni hii: Tukiwa waaminifu katika Yesu Kristo, anaweza kutuinua juu hata wakati matatizo na uovu umetuzingira. Kuwa “waaminifu katika Kristo” inaweza kuwa na maana ya kujitahidi wakati wote kutenda kama mfuasi wa kweli wa Mwokozi, kumkumbuka Mwokozi na Upatanisho Wake, na kwa uaminifu kutii amri Zake.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika kuhusu tukio maishani mwako ama maishani mwa mtu aliye karibu nawe linaloonyesha kwamba kanuni iliyotangulia ni ya kweli.

Fikiria juu ya njia moja unaweza kuwa mwaminifu zaidi katika Kristo wakati umezingirwa na uovu au hali ngumu.

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaMoroni 8–9 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu: