Seminari
Kitengo cha 31: Siku ya 4, Moroni 7:1–19


Kitengo cha 31: Siku ya 4

Moroni 7:1–19

Utangulizi

Moroni aliandika mahubiri ambayo babake, Mormoni, alikuwa ametoa kwa “ndugu zake wapendwa” miaka mingi awali Moroni 7:2). Somo hili linashughulikia sehemu ya kwanza ya mahubiri ya Mormoni yanayopatikana katika Moroni 7. Linaelezea mafundisho yake juu ya kufanya vitendo vyema na kusudi halisi na maelezo ya jinsi tunaweza kubainisha kati ya mema na maovu. Katika somo lifuatalo utasoma mahubiri yaliyosalia ya Mormoni katika Moroni 7.

Moroni 7:1–10

Mormoni afundisha wafuasi wa Yesu Kristo kuhusu vitendo na kusudi

tufaha

Je, umewahi kugundua kwamba kitu fulani hakikuwa kizuri ndani kama kilivyoonekana nje? Mfano mmoja ya hilo unaweza kuwa kipande cha tunda, kama vile tufaha ambalo lilikuwa chungu ama limeiva sana. Orodhesha mifano mengine miwili ama mitatu unayoweza kufukiria juu:

Fikiria jinsi mifano hii ya vitu ambavyo vinaonekana vizuri nje lakini kwa uhakika si vizuri inaweza kulinganishwa na vile mtu anavyoonekana kwa nje na nia za ndani za mtu. Moroni aliandika maneno ya babake, Mormoni, kuhusu hali ya mioyo yetu tunavyofanya vitendo vyema. Soma Moroni 7:2–3 ili kutambua adhara Mormoni alikuwa anahutubia.

Mormoni awareje ndugu zake ambao alikuwa anawazungumzia kama “wafuasi wa imani ya Kristo” (Moroni 7:3). Jifunze Moroni 7:4–5 ili kugundua jinsi Mormoni alijua Wanefi hawa walikuwa kwa kweli wafuasi wa Mwokozi.

Je, unafikiria mtu anaweza tu kujifanya kuwa mwema? Kwa nini ama kwa nini la?

Mormoni azungumzia swala hili katika Moroni 7:6. Unaposoma mstari huu, huenda ukataka kualamisha kifungu “kusudi jema.” Maelezo yafuatayo kutoka kwa Mzee Dallin H. Oaks wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili yanaweza kutusaidia kuelewa kile inamaanisha kuwa na kusudi jema. Tia mstari sehemu za maelezo haya yanayokuvutia.

“Hatupaswi tu kufanya kile kilicho chema. Lazima tutende kwa sababu sahihi. Neno la kisasa ni nia mzuri.Maandiko mara nyingi huonyesha mtazamo huu wa kufaa wa kiakili na maneno kusudi kamili la moyo ama kusudi jema.

“Maandiko yanaweka wazi kwamba Mungu anaelewa nia zetu na atahukumu vitendo vyetu ipasavyo” (Pure in Heart [1988], 15).

Mormoni aeleza matukio ya mtu anayejaribu kufanya vitendo vyema bila kusudi jema. Pekua Moroni 7:7–10, na utambue kile ambacho hufanyika tunapotenda vitendo vyema bila kusudi jema. Kutoka kwa mistari hii tunajifunza kwamba ili kubarikiwa kwa ajili ya vitendo vizuri, lazima tuvifanye kwa kusudi jema la moyo.Kusudi jema inajumuisha kufanya mambo mazuri kutokana na upendo kwa Mungu na wengine.

  1. ikoni ya shajaraJibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni tofauti gani umegundua wakati umefanya mambo mazuri na kusudi jema kinyume na kufanya jambo nzuri na kusudi ya ubinafsi?

  2. ikoni ya shajaraIli kukusaidia kuelewa vyema zaidi kanuni kwamba ili kubarikiwa kwa vitendo vyema, lazima tuzifanye na kusudi jema la moyo, fikiria matukio yafuatayo: Rafiki ambaye amekuwa akisoma Kitabu cha Mormoni auliza usaidizi wako katika kuelewa Moroni 7:9 na kusema, “ Nilisoma kwamba ikiwa mtu atasoma bila kusudi halisi, ‘haimsaidii chochote, kwani Mungu hampokei yeyote wa aina hii.’ Mara nyingi mimi huhisi ni kama huwa si sali kwa kusudi halisi. Je, nikome tu kusali?” Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika jinsi ungejibu swali hilo, na ueleze kwa nini ungejibu hivyo.

Rais Brigham Young alitoa ushauri huu muhimu juu ya jinsi tunavyoweza kupokea hamu ya kuomba kwa kusudi halisi: “Haijalishi kama wewe ama mimi tunajisikia kuomba, wakati wa kuomba ukija, omba. Ikiwa hatujisikii kuomba, tunapaswa tuombe hadi tujisikie” (Teachings of Presidents of the Church: Brigham Young [1997], 45).

Fikiria jinsi ushauri wa Rais Young ungeweza kuhusiana na kutii amri zingine zaidi ya maombi. Mara nyingi kufanya kile ambacho ni sahihi kunaweza kuleta nia ya kuendelea kutii amri hiyo kwa kusudi sahihi.

  1. ikoni ya shajaraIli kutumia mafunzo ya Mormoni juu ya umuhimu wa kufanya vitendo vyema na kusudi njema, chagua mmoja wa amri zifuatazo: kufunga, kulipa zaka, kuhudumia wengine, kusoma maandiko, kuwaheshimu wazazi, kubaki wasafi kimaadili. (Kubaki wasafi kimaadili inajumuisha kuwa waadilifu tunapotumia Intaneti ama mitandao ya kijamii. Inajumuisha pia kutofanya chochote ambacho kinaweza kusababisha dhambi ya ngono.) Kisha jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Umebarikiwa vipi wakati umejitahidi kutii amri hiyo kwa kusudi halisi?

    2. Ni ushauri upi ungewapa vijana wenzako juu ya jinsi ya kutii amri hiyo kwa kusudi halisi?

Moroni 7:11–19

Mormoni afundisha jinsi ya kubainisha kati ya mema na maovu

Unawezaje kujua kwamba kitu fulani ni kiovu bila ya kukijaribu? Mormoni alitoa ushauri ili kutusaidia tunapokumbana na hali kama hiyo.

  1. ikoni ya shajaraSoma Moroni 7:11–13, na utafute jinsi ya kubainisha mema kwa ovu. Huenda ukataka kualamisha vifungu ambavyo vinakuvutia. Fupisha kile unachojifunza kutoka kwa mistari hii kwa kukamilisha kauli zifuatazo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Kile ambacho ni cha Mungu 

    2. Kile ambacho huja kutoka kwa ibilisi 

Mormoni alihimiza kwamba Mungu hutualika na kutushawishi kufanya mema kila mara. Tambua kwamba kulingana na Moroni 7:12, ibilisi pia hutualika na kutushawishi. Fikiria kuhusu baadhi ya njia ambazo ibilisi hutualika na kutushawishi kutenda dhambi.

Mzee Jeffrey R. Holland

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alijadili nia ya Shetani ya kutafuta kutushawishi kutenda maovu kila mara: “Shetani, Lusiferi, ama baba wa uongo mwite chochote utakacho — ni halisi, ishara kuu ya uovu. Nia zake zipo katika kila tukio mbaya. Milele yuko kinyume na upendo wa Mungu, Upatanisho wa Yesu Kristo, na kazi ya amani na uokovu. Atapigana dhidi ya haya wakati wowote na popote anaweza. Anajua atashindwa na kutupwa nje mwishowe, lakini amejitahidi kuchukua naye wengi awezavyo” (“We Are All Enlisted,” Ensign ama Liahona, Nov. 2011, 44).

  1. ikoni ya shajaraIli kukusaidia kutumia mafunzo ya Mormoni juu ya kubainisha kati ya mema na ovu, orodhesha katika shajara yako ya kujifunza maandiko baadhi ya vipindi vya runinga, nyimbo, vikundi vya kuimba, Tovuti, programu, michezo ya video, ama mali ya kibinafsi uanyopenda. (Huenda ukataka kubadilisha orodha hii kulingana na yale unayopenda.) Utarudia tena ingizo hili la shajara baadaye katika somo hili.

Soma Moroni 7:15–17, na utafute kweli ambazo zitakusaidia kujua jinsi ya kubainisha kama kitu fulani ni cha Mungu ama cha ibilisi.

Roho ya Kristo inaitwa pia Nuru ya Kristo (ona Moroni 7:18). Rais Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, alitoa maelezo haya ambayo yanaweza kutusaidia kuelewa zaidi Nuru ya Kristo:

Rais Boyd K. Packer

“Roho Mtakatifu na Nuru ya Kristo inatofautiana. Ingawa wakati mwingine huelezewa katika maandiko na maneno sawa, ni viumbe viwili tofauti na vya kipekee. …

“Zaidi tunavyojua kuhusu Nuru ya Kristo, ndipo zaidi tutaelewa kuhusu maisha na ndipo zaidi tutakuwa na upendo wa kina kwa kila mwanadamu. …

“Bila kujali kama nuru hii ya ndani, ufahamu huu wa mema na mabaya, inaitwa Nuru ya Kristo, ufahamu wa kimaadili, au dhamiri, inaweza kutuelekeza kustani matendo yetu —isipokuwa, yaani, tuiangamize ama tuinyamazishe. …

“Kila mwanaume, mwanamke, na mtoto wa kila taifa, imani, ama rangi — kila mtu, bila kujali mahali ambapo wanaishi ama kile wanachoamini ama kile ambacho wanafanya —wanayo ndani yao Nuru isiyoisha ya Kristo. Kwa hali hii watu wote wameumbwa kwa usawa. Nuru ya Kristo katika kila mtu ni ushuhuda kwamba Mungu hana upendeleo wa watu” (“The Light of Christ,” Ensign, Apr. 2005, 8–10).

Waumini wa Kanisa waliobatizwa pia wana karama ya Roho Mtakatifu kuwasaidia kubaini mema na maovu. Rais Packer alifundisha, “Roho Mtakatifu anaweza kufanya kazi kupitia Nuru ya Kristo” (“Light of Christ,” 10).

Pekua Moroni 7:18–19 ili kupata ushauri wa Mormoni juu ya jinsi ya kuijibu Nuru ya Kristo ndani yetu. Huenda ukataka kualamisha maneno na vifungu katika mistari hii vinavyoonyesha kwamba tunapopekua kwa bidii kufuata Nuru ya Kristo, tunaweza kubainisha kati ya mema na maovu.

Rejea orodha uliotengeneza katika shajara yako ya kujifunza maandiko katika zoezi 5. Tafakari kwa makini vitu kwenye orodha yako, na “utafute kwa bidii katika nuru ya Kristo” (Moroni 7:19) kuamua kama vitu hivi vinakuja kutoka kwa Mungu. Maswali yafuatayo huenda yakawa muhimu kuzingatia:

  • Vitu hivi vinakualika vyema vipi kufanya mema, kuamini katika Kristo, kumpenda Mungu na kumtumikia?

  • Je, kuna chochote kati ya hivi kinachokushawishi “kufanya maovu kutoamini katika Kristo, kumkana, [ama] kutomtumikia Mungu”? (Moroni 7:17).

  • Je, unahisi unapaswa kuondoa kitu chochote kutoka kwa maisha yako? Ikiwa ni hivyo, utafanyaje hivi?

Mormoni alitoa ahadi kwamba unapochagua kuondoa chochote kutoka kwa maisha yako ambacho si kizuri na kutaka “kushikilia kila kitu kizuri,” unakuwa “mtoto wa Kristo” (Moroni 7:19).

  1. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaMoroni 7:1–19 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu: