Seminari
Kitengo cha 6: Siku ya 1, 2 Nefi 4–5


Kitengo cha 6: Siku ya 1

2 Nefi 4–5

Utangulizi

Katika 2 Nefi 4 utasoma jinsi Lehi aliukusanya pamoja uzao wake ili awapatie ushauri wake wa mwisho na kuwabariki kabla hajakufa. Baada ya kifo cha Lehi, Lamani na Lemueli walimkasirikia Nefi kwa kuwahubiria “maonyo ya Bwana” (ona 2 Nefi 4:13–14). Akisumbuliwa na mitazamo na matendo ya kaka zake na kwa udhaifu na dhambi zake mwenyewe, Nefi aliandika hisia zake kwa lugha ya uwazi na kwa ushairi (ona 2 Nefi 4:15–35). Kama ilivyoandikwa katika 2 Nefi 5, Bwana alimwonya Nefi na wale ambao walimsaidia kutoroka kutoka kwa Lamani, Lemueli, na wana wa Ishmaeli. Kufuatia utengano huu, Wanefi waliishi kwa haki na furaha, huku wale waliobaki na Lamani na Lemueli walijikatilia mbali kiroho kutoka kwa Bwana. Uchaji wa Bwana wa Nefi ulimuimarisha hata kushinda dhambi na kuvunjika moyo. Nefi kisha akaandika jinsi yeye na watu wake “waliishi kwa furaha” (2 Nefi 5:27).

2 Nefi 4:3–11

Lehi anashauri na kubariki familia yake

Fikiria wakati ambapo wewe ulipokea ushauri au wasia kutoka kwa mama, baba, au viongozi wako. Je! Uliufuata wasia huu? Kwa nini ulifuata au kwa nini haukufuata wosia huo? Je! Una majuto yoyote? Katika 2 Nefi 4:1–11, Nefi aliandika ushauri na baraka za mwisho za Lehi kwa familia yake. Soma 2 Nefi 4:4–5, na utambue ushauri ambao Lehi aliwapa watoto wake ambao pia wewe unaweza kutumia. Je! Wazazi wako, wanafamilia, au viongozi wako wameshawahi kukupatia ushauri kama huo?

Picha
Lehi akishikilia mabamba ya shaba
  1. Tengeneza orodha katika shajara yako ya kujifunza maandiko ya baadhi ya baraka ambazo zimekuja katika maisha yako kutokana na kusikiliza ushauri wa wale wanaokujali wewe. Ni baraka gani ambazo zimekuja kutokana na kuwa mtiifu kwa amri za Bwana?

2 Nefi 4:12–35

Nefi alionyesha matumaini yake katika Bwana na kukiri udhaifu wake.

Katika 2 Nefi 4:12–35, Nefi aliandika “mambo ya nafsi [yake]” (2 Nefi 4:15). Soma 2 Nefi 4:15–16, na utafute kile Nefi alifurahishwa nacho.

Fikiria kuhusu mambo ya burudani safi ambayo yanakuletea shangwe kuu. Kamilisha kishazi kifuatacho na maswali kadhaa: Nafsi yangu hufurahia katika .

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile unafikiria inamaanisha kufurahia katika mambo ya Bwana.

Nefi alitaja kwamba “moyo wake utafakari” (2 Nefi 4:15) maadiko. Kutafakari haimaanishi tu kutaamali na kufikiria kwa kina kuhusu maandiko bali pia kufungua mioyo yetu kwa ufunuo na uelewa.

Nefi alipata uzoefu wa nyakati za shangwe kuu katika maisha yake; hata hivyo, yeye pia alikabiliana na nyakati ngumu. Rejea tena kwa 2 Nefi 4:12–13 ili kugundua baadhi ya changamoto kali zilizomkabili Nefi wakati huo katika maisha yake.

Soma 2 Nefi 4:17–18, na utafute kingine kile kilimfanya Nefi kuhuzunika. Unaposoma, weka maelezo yafuatayo akilini: Huzunika humaanisha mnyonge au maskini. Nyama inalenga udhaifu katika hali yetu maisha ya mauti. Zonga humaanisha kuzunguka au kufinya pande zote, kusumbua, au kuangaisha. Ingawa Nefi alihisi huzuni kwa sababu ya dhambi zake, hii haifai kukosewa kumaanisha kwamba yeye alikuwa na hatia ya makosa yoyote makubwa.

Fikiria wakati katika maisha yako ambapo unaweza kulinganisha na jinsi Nefi alihisi (kama vile wakati umempoteza mpendwa, wengine wamekuwa wamekasirika nawe kwa kumfuata Bwana, umekabiliwa na shida au kuvunjika moyo, au umehisi huzuni kwa sababu ya dhambi, udhaifu, na majaribu yako). Soma 2 Nefi 4:19, na utambue kishazi ambacho kinaonyesha matumaini ya Nefi licha ya huzuni wake. Unafikiri ni nini Nefi alimaanisha wakati aliposema, “Ninajua ninayemwamini.”? Je! Unaweza kuweka imani kuu katika Mungu?

Unapoendelea na mafunzo yako, tafuta ushahidi wa kanuni ya injili kwamba Mungu huwahimili wale ambao wanaweka matumaini yao Kwake.

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, jibu maswali haya katika chati kifuatacho;

Marejeo ya Maandiko

Jinsi Mistari Hii Ilivyotumika kwa Nefi

Jinsi Mistari Hii Inaweza Kutumika Kwako.

2 Nefi 4:20–25

  1. Ni kwa Jinsi gani Bwana alikuwa amembariki Nefi hapo awali kwa kuweka matumaini yake Kwake?

  1. Ni kwa jinsi gani Bwana amekubariki wakati umeweka matumaini Kwake?

2 Nefi 4:26–30

  1. Je! Kukumbuka baraka zake ziliathiri vipi hamu ya Nefi ya kuwa mwema?

  1. Ni kwa jinsi gani baraka za Bwana zimeathiri hamu yako ya kuwa mwema?

2 Nefi 4:31–33

  1. Nefi aliomba nini?

  1. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia mistari hii katika maombi yako?

Soma 2 Nefi 4:34–35, na uweke alama vishazi ambavyo vinaonyesha imani ya Nefi katika Bwana.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kile umejifunza kutoka kwa kujifunza 2 Nefi 4:17–35 na njia ambazo ungependa kuongeza imani yako katika Bwana.

2 Nefi 5:1–8

Bwana anawatenganisha Wanefi kutoka kwa Walamani

Unapojifunza 2 Nefi 5, fikiria shida ngumu na maamuzi unayoweza kuwa unapata au umeshapata. Katika sura hii Nefi alielezea kwamba kaka zake “walitafuta kunitoa uhai” (2 Nefi 5:2). Tazama katika 2 Nefi 5:1 kile Nefi alifanya ili kupata suluhisho la shida. Kisha weka alama katika maandiko kile Bwana alifanya ili kumsaidia Nefi katika 2 Nefi 5:5.

Picha
kundi la Wanefi

Kama matokeo ya onyo hili, Nefi na “wote wale ambao waliamini katika maonyo na ufunuo wa Mungu” (2 Nefi 5:6) waliacha nchi ya urithi wao wa kwanza. Walisafiri “kwa muda wa siku nyingi” (2 Nefi 5:7) na wakafanya makazi katika sehemu iliyoitwa Nefi. Uzoefu huu unaonyesha kwamba usalama huja kutokana na kutii ufunuo wa Mungu.

Soma ushuhuda ufuatao kutoka kwa Mzee Paul V. Johnson wa Sabini: “Haishangazi kwamba katika makabiliano ya majaribu na uovu mkali, Bwana hatuachi sisi kutafuta njia yetu wenyewe. Kwa kweli, kuna zaidi kuliko mwongozo wa kutosha unaopatikana kwa kila mmoja wetu kama sisi tutasikiliza. Umepokea kipawa cha Roho Mtakatifu ili akuelekeze na akupatie maongozi. Mna maandiko, wazazi, viongozi na walimu wa Kanisa. Pia mna maneno ya manabii, waonaji, na wafunuaji ambao wanaishi katika siku yetu. “Kuna maelekezo na miongozo mingi inayopatikana kiasi kwamba huwezi kufanya makosa makubwa katika maisha yako isipokuwa upuuze kimakusudi mwongozo uliopokea” (“The Blessings of General Conference,” Ensign, Nov. 2005, 51).

  1. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika onyo ambalo umepokea kutoka kwa Bwana, manabii Wake au viongozi wengine wa Kanisa. Unafanya nini ili kufuatia onyo hilo? Je! Kufuata onyo hilo kumekusaidia vipi katika maisha yako, na ni kwa jinsi gani itakusaidia katika siku za usoni?

2 Nefi 5:9–18, 26–27

Wanefi waliishi kwa hali ya furaha

Baada ya kusimulia hali zilizoleta mgawanyiko wa familia ya Lehi, Nefi alielezea vile maisha yalikuwa miongoni mwa “watu wa Nefi” (2 Nefi 5:9). Soma 2 Nefi 5:27, na uweke alama kishazi kile kinachoonyesha jinsi Wanefi walivyoishi. Unafikiri inamaanisha nini kuishi “kwa furaha”?

  1. Soma kwa makini 2 Nefi 5:10–18, 26, na uweke alama katika maandiko yako kile Wanefi walikuwa nacho au walifanya ambacho kilichangia furaha yao. Chagua moja ya vitu hivi, na uandike katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi kitendo au mtazamo huu ulichangia kwa furaha yako. Kwa mfano, kama utachagua jambo kwamba Wanefi walijenga hekalu (ona 2 Nefi 5:16), unaweza kuandika jinsi hekalu limeleta furaha kuu kwako au kwa familia yako.

Matendo na mitazamo ambayo umetambua ni sehemu ya kuishi injili ya Yesu Kristo. Unaweza kutaka kuandika kanuni ifuatayo katika maandiko yako karibu na 2 Nefi 5:27: Injili ya Yesu Kristo inapokuwa njia yetu ya maisha, tunaongezeka katika furaha. Hii ilikuwa kweli kwa Wanefi hata katika nyakati ngumu sana. Tathimni maisha yako na uamue kitu ambacho wewe utafanya hili kuishi njia ya furaha kamilifu. Kiandike katika shajara yako ya kibinafsi au katika maandiko yako. Kanuni ambazo umejifunza leo zinaelekeza kwenye furaha.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 2 Nefi 4–5 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha