Kitengo cha 6: Siku ya 2
2 Nefi 6–8
Utangulizi
Kumbukumbu ya Nefi ya sehemu ya kwanza ya mahubiri yaliyofunzwa na kaka mdogo Yakobo yanapatikana katika 2 Nefi 6–8. (Sehemu ya pili ya mahubiri ya Yakobo yanapatikana katika 2 Nefi 9–10.) Yakobo alitoa unabii kwamba tangu wakati Lehi aliondoka Yerusalemu,Wayahudi walikuwa wamechukuliwa mateka na kutawanywa kwa sababu ya uovu wao. Hata hivyo, Bwana angewakusanya kwa huruma Wayahudi na kuwarudisha Yesusalemu. Yakobo pia alitoa unabii kwamba Wayahudi wangetawanywa mara ya pili baada ya kumkataa Mwokozi wakati wa huduma Yake hapa duniani; tena Bwana ataonyesha rehema na kuwakusanya katika siku za mwisho watakapomjua Mwokozi. Kwa kuongeza, Yakobo alinukuu unabii wa Isaya kuonyesha uaminifu wa Mwokozi kwa agano Lake kwa watu, rehema Zake, na ukuu wa ahadi Zake kwa waaminifu.
2 Nefi–6
Yakobo anatoa unabii juu ya kutawanyika na kukusanyika kwa Israeli
Je! Ungefanya nini kama watu uwapendao wangekufanyia vibaya? Vipi kama wangeonesha kwa matendo au mitazamo yao kwamba uhusiano wenu haukuwa tena na umuhimu kwao? Tafakari ikiwa wewe umeshafanya hivyo Bwana. Katika 2 Nefi 6–8, Yakobo alifundisha jinsi Bwana hujibu kwa wale ambao, kwa mitazamo na matendo yao, wamegeuka kutoka Kwake.
Soma 2 Nefi 6:3–5; 9:1, 3, na utafute ni sababu gani zilimfanya Yakobo atoe mahubiri haya.
Unapojifunza leo, tafuta jinsi mafundisho ya Yakobo yanaweza kukusaidia “ujifunze na kulitukuza jina la Mungu wenu” (2 Nefi 6:4), ili mfahamu vyema maagano mliyofanya na Bwana (ona 2 Nefi 9:1), na kukupatia sababu yenu “kushangilia, na kuinua vichwa vyenu juu milele” (2 Nefi 9:3).
-
Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Yakobo alianza mahubiri yake kwa kutoa unabii wa kile kilichowatokea Wayahudi baada ya Lehi kuondoka Yesusalemu kwa sababu ya kumkataa Bwana. Je! Yeye alikielezea vipi katika 2 Nefi 6:8?
-
Lehi, Yeremia na manabii wengine walitoa unabii kuhusu maangamizo haya. Wakati Wababeli walipowashinda Wayahudi takribani miaka 587 Kabla Kristo, wengi waliuawa na wengine kuchukuliwa mateka katika Babeli. Wayahudi hatimaye walilainisha mioyo yao kwa Bwana. Kulingana na sentensi ya kwanza ya 2 Nefi 6:9, Yakobo alitoa unabii upi kuhusu kitu gani kingetokea kwao?
-
Yakobo alitoa unabii kwamba Mwokozi angeishi maisha Yake duniani miongoni mwa Wayahudi baada ya wao kurudi kutoka utumwani. Kulingana na 2 Nefi 6:9–10, Wayahudi wangetenda na kuhisi vipi kwa Mwokozi?
-
Kulingana na 2 Nefi 6:10–11, ni nini kingetokea kwaWayahudi waliomkataa Mwokozi?
-
Soma 2 Nefi 6:11, 14, na uangalie vishazi ambavyo vinaelezea jinsi Bwana anahisi kuhusu nyumba ya Israeli ingawa wao walimkataa Yeye. Unaweza kutaka kuweka duara vishazi “atawarehemu” na “kuwakomboa” katika maandiko yako.
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika majibu yako kwa maswali yafuatayo:
-
Inamaanisha nini “kukomboa” mtu au kitu?
-
Je! Upendeleo wa Bwana wa kuikomboa Israeli mara ya pili kunaonyesha rehema Zake vipi?
-
Katika mistari hiyo hiyo Yakobo alifunza kile Wayahudi sharti wafanye ili wapokee baraka kutoka kwa Bwana. Soma 2 Nefi 6:11, 14 tena, na utafute kishazi “watakapo” katika kila mstari. Zingatia maneno ambayo yanakamilisha kishazi. Kulingana na mistari hii, Israeli itahitimu vipi kwa rehema za Bwana? Mistari hii inafundisha kanuni: Bwana ni mwenye rehema kwa wale wanaorudi Kwake.
-
Tafakari njia ambazo umeshuhudia rehema na upendeleo wa Bwana wa kusamehe wale wanaorudi Kwake. Katika shajara yako ya kujifunza maandiko andika: Mimi najua Bwana ni mwenye rehema kwa sababu … Kisha kamilisha kauli hii kwa mawazo na hisia zako mwenyewe. Unaweza kutaka kurudia zoezi hili unapofikiria njia tofauti Bwana ameonyesha kwamba Yeye ni mwenye rehema.
Katika 2 Nefi 6 kuna ahadi kuu ya matumaini kwa Israeli—ambayo inatujumuisha sisi sote. Soma 2 Nefi 6:17–18, na ukamilishe ahadi zifuatazo zilizofanywa na Mwokozi:
“Mwenyezi Mungu ata (2 Nefi 6:17).
“Miili yote itafahamu kwamba ” (2 Nefi 6:18).
2 Nefi 7–8
Yakobo ananukuu unabii wa Isaya kuhusu uaminifu wa Mwokozi kwa watu wa agano na uwezo Wake wa kutukomboa.
Kama ilivyoandikwa katika 2 Nefi 7–8, Yakobo alinukuu unabii wa Isaya kuhusu hamu na uwezo wa Bwana wa kuikomboa Israeli kutokana na mateso yanayosababishwa na dhambi zao. Soma 2 Nefi 7:1–2, na utambue maswali ambayo Bwana aliiuliza Israeli ambayo yanaonyesha Yeye bado anawapenda na alitaka kuwakomboa.
Itaweza kusaidia kuelewa kwamba Bwana alitumia lugha ya ishara kulinganisha talaka na utumwa, na desturi za kijamii zilizokuwa zinafahamika na watu wa siku hizo, ili kuwafundisha kwa njia ya athira na kukumbukwa. Vishazi “nimekuweka kando,” “cheti cha talaka ya mama yako” na “nimekuuza” vinalenga wazo la kuvunjika au kuvunja agano. Maswali yanaweza kugeuzwa kama ifuatavyo: “Je! Mimi nimegeuka kutoka kwako? Je, nimeweka kando agano ambalo tumelifanya?” Jibu la maswali haya ni, “La.” Bwana kamwe hatageuka kutoka kwetu au kusahau maagano Yeye amefanya. Maswali Yake ni njia ya kusisitiza kwamba Yeye kamwe hatavunja agano Lake na Israeli.
Hapo mwisho wa 2 Nefi 7:1, weka mstari chini ya maelezo ya Bwana ya kwa nini Israeli ilitenganishwa na Mungu na kuteseka katika utumwa.
-
Jibu moja ya maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Kwa nini ni muhimu kuelewa kwamba mawazo, maamuzi, na matendo yetu yanaweza kututenga kutoka kwa Mungu?
-
Kwa nini ni muhimu kwako kujua kwamba Bwana kamwe hasahau au kututelekeza sisi, hata ingawa sisi tunaweza kumsahau na kumtelekeza?
-
Katika 2 Nefi 7:2 Bwana aliiuliza Israeli swali muhimu sana ambalo linatumika kwa kila mmoja wetu. Tafuta na uangazie swali hili.
Unafikiria Bwana alimaanisha nini wakati alipouliza, “Je, mkono wangu umefupishwa kwamba siwezi kukomboa? Ili kutusaidia kupiga twasira ya haya, fikiria wewe unayoosha mkono wako, ukijaribu kumfikia mtu fulani aliye na mahitaji. Kama ungeweza kurefusha mfiko wako, wewe ungekuwa unajaribu kufanya nini kwa ajili ya huyu mtu mwenye mahitaji? Kama badala yake ulifupisha au kurudisha mkono wako nyuma, ingesemekana vipi kuhusu hamu yako ya kumsaidia mtu yule. Ukiwa na picha hii akilini, njia nyingine ya kuuliza swali la Bwana kwa Israeli ni: “Kwani mimi ninajizuia na siwezi kukufikia ili kukukomboa wewe?
Kishazi “kwani sina uwezo wa kukomboa?” alialika Israeli kutafakari juu ya imani yao kwamba Bwana alikuwa na nguvu za kuwakomboa kutoka kwa mateso yaliyosababishwa na dhambi zao.
Katika salio la 2 Nefi 7–8, Isaya alitoa mifano kadhaa ya hamu na nguvu za Mwokozi za kukomboa watu Wake wa agano.
Soma 2 Nefi 7:5–7, na utafute vishazi katika unabii huu ambavyo vinaelezea kile Masiya angefanya na kupitia kama sehemu ya dhabihu ya upatanisho wake ili kutukomboa. Katika 2 Nefi 7:6, tanbihi a, kuna marejeo mtambuko ambayo yanaelezea na kuonyesha utimizo wa unabii huu. Unaweza kutaka kuweka alama Mathayo 27:26 katika tanbihi; kisha usome Mathayo 27:26–31, ukitafuta njia ambazo unabii wa Isaya ulitimizwa.
-
Jibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni nini2 Nefi 7:2, 5–7 utuonyesha kuhusu hamu ya Mwokozi na upendeleo wa kutukomboa?
Ili kukusaidia kugundua ushahidi zaidi wa rehema na nguvu za Bwana katika salio la unabii wa Isaya, fikiria umeombwa kutoa hotuba katika kanisa juu ya kanuni hii : Mwokozi ana hamu ya kukomboa watu Wake wa agano na ana nguvu zote za kufanya hivyo. Ili kutayarisha hotuba yako, soma 2 Nefi 8:3, 11–13, 16, 22, na uchague vishazi ambavyo unahisi vinatoa hakikisho la hamu na nguvu za Bwana za kutukomboa sisi.
-
Tengeneza muhtasari wa hotuba yako katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa:
-
Orodhesha vishazi viwili au vitatu ambavyo vinaonekana wazi kwako na uelezee jinsi kila kishazi ni mfano wa hamu ya Mwokozi ya kutukomboa sisi au nguvu Zake za kufanya hivyo.
-
Ukichagua mojawapo wa vishazi hivi na kuelezea jinsi wewe aidha umepata, au ungependa kupata, hiyo baraka katika maisha yako.
-
Unapokamilisha somo hili, kumbuka kwamba Yakobo alifundisha kweli ulizojifunza leo “ili mjifunze na kulitukuza jina la Mungu wenu”.(2 Nefi 6:4), “ili mfahamu kuhusu yale maagano ya Bwana” (2 Nefi 9:1), na “kwamba mshangilie, na muinue vichwa vyenu juu milele” (2 Nefi 9:3). Tafuta nafasi leo ya kushiriki uthamini wako kwa Bwana na upendo Wake kwenu pamoja na mtu mwingine.
-
Andika yafuatayo katika sehemu ya chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza2 Nefi6–8 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: