Kitengo cha 7: Siku ya 4
2 Nefi 25
Utangulizi
Baada ya kuandika unabii wa Isaya (2 Nefi 12–24), nabii Nefi alisisitiza umuhimu wa unabii huu na kuelezea kwamba wale walio na roho wa unabii wanaweza kuja kuelewa na kuthamini maneno ya Isaya (2 Nefi 25). Alielezea kwamba madhumuni ya uandishi wake ilikuwa ni: “kuwashawishi watoto wetu, na pia ndugu zetu, kumwamini Kristo, na kupatanishwa na Mungu” (2 Nefi 25:23). Aliwaalika wote kumwamini Yesu Kristo na “kumwabudu kwa uwezo wako wote, akili, na nguvu, na nafsi yako yote” (2 Nefi 25:29).
2 Nefi 25:1–8
Nefi anafundisha kwamba tunaweza kuelewa maneno ya Isaya tunapokuwa na roho wa unabii
Watu kila mara wanatumia makufuli kuweka mali zao za thamani salama. Wanaweza kuhifadhi ufunguo muhimu tu wa kufuli, au wanaweza kumpa nakili ya ufunguo kwa rafiki anayeaminika au mwanafamilia. Nefi alijua kwamba unabii wa Isaya ulikuwa “wa thamani kuu” (2 Nefi 25:8), na alitaka kila mtu kuzielewa. Alitoa ufunguo kwa mtu yeyote ambaye anataka kufungua maana ya maneno ya Isaya.
Soma sentensi ya kwanza katika 2 Nefi 25:4, na utafute ufunguo wa kuelewa maneno ya Isaya. Inamaanisha nini kuwa na “roho ya unabii”? Unafikiria roho ya unabii inaweza kukusaidia vipi kuelewa vyema maandiko, hasa maneno ya Isaya?
Roho ya unabii inahusisha roho ya ufunuo. Hii inamaanisha kwamba unapojifunza maandiko kwa bidii na maombi na kutafuta kuelewa maana yake, unaweza kuwa na roho ya ufunuo, na Roho Mtakatifu ataangaza akili yako na uelewa wako. Pia, maandiko yanafunza kwamba “ushuhuda wa Yesu ni roho ya unabii” (Ufunuo wa Yohana 19:10). Unapokua katika elimu na ushuhuda wako wa Mwokozi, uelewa wako wa maandiko—ikijumuisha mafundisho ya Isaya—utaongezeka na utaelewa vyema jinsi mafundisho yanavyo husiana nawe.
Nefi alishiriki mawazo mengine ambayo yanaweza kuongeza ufahamu wetu wa maneno Isaya. Pekua maandiko yafuatayo, na utambue funguo tatu zaidi za kuelewa maneno ya Isaya:
Kumbuka kwamba lugha ya kiistairi na kishairi mara nyingi zinatumika katika unabii wa Kiyahudi (ona 2 Nefi 25:1). Pia, kujifunza tamaduni, historia, na jiografia ya Israeli ya kale kutakusaidia kuelewa maneno ya Isaya (ona 2 Nefi 25:5–6). Kuishi katika siku za mwisho na kuona utimilifu wa unabii mwingi pia hutusaidia kuelewa Isaya (ona 2 Nefi 25:7–8).
2 Nefi 25:9–19
Nefi anatoa unabii kuhusu Wayahudi
Kama ilivyoandikwa katika 2 Nefi 25:9–19, Nefi alitoa unabii kuhusu Wayahudi na nchi yao katika Yerusalemu na maeneo yaliyozunguka . Alisema kuwa Wayahudi ambao walikuwa wamechukuliwa utumwani Babeli baada ya maangamizo ya Yerusalemu watarudi kwenye “nchi yao ya urithi” (ona 2 Nefi 25:9–11). Yesu Kristo, Masiya, ataishi miongoni mwao, lakini wengi watamkataa na kumsulubisha (ona 2 Nefi 25:12–13). Baada ya kifo na Ufufuo wa Mwokozi, Yerusalemu ingeharibiwa tena, na Wayahudi wangetawanywa na kuumizwa na mataifa mengine (ona2 Nefi 25:14–15). Hatimaye wataamini katika Yesu Kristo na Upatanisho Wake, na Bwana atawarudisha “kutoka kwa hali yao ya kupotea na kuanguka”(ona 2 Nefi 25:16–19).
2 Nefi 25:20–30
Nefi anashuhudia juu ya Yesu Kristo
Fikiri kuhusu jinsi unavyoweza kumjibu mtu ambaye anadai kuwa Watakatifu wa Siku za Mwisho hawaamini katika Yesu Kristo. Unapojifunza salio la 2 Nefi 25, tafuta vifungu ambavyo unaweza kushiriki katika hali kama hio.
Kwa upesi tazama 2 Nefi 25:20–30, na ufikirie kuweka alama jina “Kristo” kila mara linapotokea.
-
Soma 2 Nefi 25:28–29, na utambue kile Nefi alisema kilikuwa “njia iliyo sahihi.” Pekua 2 Nefi 25: 23–26 kwa sababu za kwa nini kuamini katika Yesu Kristo ni “njia iliyo sahihi.” (Kumbuka kwamba 2 Nefi 25:23, 26 ni kifungu cha umahiri wa maandiko. Unaweza kutaka kukiweka alama katika njia ya kipekee ili uweze kukipata wakati ujao.) Andika majibu yako katika shajara yako ya kujifunza maandiko.
Neno kupatanishwa katika 2 Nefi 25:23 humaanisha kuletwa katika uwiano na Mungu. “Neema” za Bwana ndiyo jinsi hatimaye upatanisho na Mungu hutokea. Soma maelezo yafuatayo ya neema za Bwana:
“Neno neema, kama linavyotumiwa katika maandiko, linamaana ya kimsingi kwa msaada mtakatifu na nguvu tunazopokea kupitia Upatanisho wa Bwana Yesu Kristo.
Kupitia neema, inayopatikana na dhabihu ya upatanisho wa Mwokozi, watu wote watafufuka na kupokea kutokufa. [Lakini ikiwa tutahitimu kwa uzima wa milele katika uwepo wa Mungu, ni sharti tuwe wasafi kutoka kwa dhambi zetu kupitia neema Zake.]
“Kishazi ‘baada ya kutenda yote tunayoweza’ [2 Nefi 25:23] hutufunza kwamba juhudi zinahitajika kutoka upande wetu ili kupokea utimilifu wa neema za Bwana na kufanywa wastahiki kuishi pamoja Naye. Bwana ametuamuru sisi kutii injili Yake, ambayo inajumuisha kuwa na imani katika Yeye, kutubu dhambi zetu, kubatizwa, kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, na kuvumilia mpaka mwisho. …
“Kama ziada ya kuhitaji neema kwa wokovu wako kimsingi, unahitaji nguvu hizi za kuwezesha kila siku ya maisha yako. Unapomkaribia Baba yako wa Mbinguni kwa bidii, unyenyekevu, na upole, Yeye atakuinua na kukuimarisha kupitia neema Yake” (True to the Faith: A Gospel Reference [2004], 77–78).
-
Katika shajara yako ya kujifunza maandiko, andika majibu kwa maswali yafuatayo:
-
Kuna uhusiano gani kati ya neema ya Bwana na juhudi zetu za kuishi injili?
-
Inamaanisha nini kwako kuokolewa kwa neema?
-
Kishazi “yote tunayoweza” kinamaanisha nini kwako?
-
Tafakari ukweli ufuatao: Kwa sababu ya Yesu Kristo, tunaweza kuokolewa kwa neema baada ya yote tunayoweza kufanya. Fikiria wakati ulipofanya yote unayoweza kufanya na ukabarikiwa kwa msaada na nguvu takatifu.
Ukweli mwingine ambao Nefi alifunza (ona 2 Nefi 25:26) ni: Kupitia Upatanisho wa Mwokozi, tunaweza kupokea ondoleo la dhambi zetu.
Fikiria kuandika barua kwa rafiki au mwana familia kuhusu imani yako katika Yesu Kristo au kushuhudia juu ya imani yako katika mkutano wa ushuhuda au mazingira mengine yanayofaa.
-
Soma 2 Nefi 25:26 tena, na kisha ujibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
-
Ni kwa njia gani wewe unamwabudu au kumstahi Yesu Kristo? Ni shughuli gani zinaonyesha wengine kwamba wewe unaamini katika Yesu Kristo na kumwabudu?
-
Unaweza kufanya nini ili kumwabudu vyema Mwokozi kwa uwezo, akili, na nguvu zako zote?
-
Umahiri wa maandiko—2 Nefi 25:23, 26
Tumia mfumo ufuatao ili ukusaidie kukariri 2 Nefi 25:26:
“Na tunazungumza kuhusu Kristo,
tunafurahia katika Kristo,
tunahubiri kuhusu Kristo,
tunatoa unabii kumhusu Kristo,
na tunaandika kulingana na unabii wetu,
ili watoto wetu wajue
asili ya kutegemea
kwa msamaha wa dhambi zao.”
Baada ya kurudia kifungu hiki mara chache, funika mstari wa juu kwa mkono wako na ujaribu tena. Kisha ufunike mstari mwingine, na uendelee mpaka unapohisi umekariri kifungu hiki.
-
Tongoa 2 Nefi 25:26 kwa mwana familia, na uandike kwamba umeikariri katika shajara yako ya kujifunza maandiko.
-
Andika yafuatayo chini ya kazi za leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:
Nimejifunza 2 Nefi 25na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).
Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningependa kushiriki na mwalimu wangu: