Seminari
Kitengo 2: Siku ya 4, 1 Nefi 5–6; 9


Kitengo 2: Siku ya 4

1 Nefi 5–6; 9

Utangulizi

Mkewe nabii Lehi, Saria, alikuwa na hofu kwamba wanawe hawatarudi kutoka Yerusalemu. Lehi alimfariji kwa kuonyesha imani yake katika Bwana. Wakati wanawe walirudi salama na mabamba, Saria alipata ushahidi imara wa mkono wa Mungu katika kuelekeza na kuhifadhi familia yake. Lehi alipoyasoma mabamba ya shaba, “alijawa na Roho, na akaanza kutoa unabii kuhusu uzao wake” (1 Nefi 5:17). Unapojifunza somo hili, fikiria kuhusu kujifunza maandiko kwako kibinafsi na kile unaweza kufanya ili kupokea nguvu inayopatikana kutokana na kutafuta neno la Mungu.

1 Nefi 5:1–9

Wana wa Lehi walirudi salama kwa familia yao huko nyikani

Safari ya kwenda Yerusalemu na kurudi ilichukua Nefi na nduguze karibu wiki kadhaa. Waza kuhusu wakati ndugu, dada, mzazi, au mtu mwengine unayemjua aliondoka nyumbani kwa muda mrefu—kama vile kwa ajili ya misheni, shule, au utumishi wa jeshi. Ni shauku au wasiwasi gani uliyokuwa nayo (au ni shauku gani unafikiri mzazi anaweza kuwa nayo) anapotenganishwa na mpendwa kwa muda mrefu? Soma 1 Nefi 5:1–3, na utambue shauku ambazo Saria alieleza Lehi kuhusu safari ya wanawe kurudi Yerusalemu.

Jifunze 1 Nefi 5:4–6, na utafute jinsi Lehi alijibu mashaka ya Saria.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, tamka katika maneno yako mwenyewe majibu ya Lehi kwa mkewe.

Angazia kwenye maswali yafuatayo:

  • Ni nini kilikuvutia kuhusu jinsi Lehi alivyojibu mashaka ya Saria?

  • Maneno ya Lehi yanaonyesha vipi imani na ujasiri aliopata kutoka kwa funuo ambazo Mungu alimpatia?

Kulingana na 1 Nefi 5:6, ushuhuda wa Lehi ulikuwa na matokeo gani kwa Saria?

Kweli mbili tunazoweza kujifunza kutokana na uzoefu huu wa Lehi na Saria ni kuwa Bwana anaweza kutubariki na imani tunapofuata uongozi Wake na tunaweza kufariji na kuimarisha wengine tunapoonyesha imani yetu kwa Mungu.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea wakati ulipohisi imani tulivu wakati wa hali ngumu, kushiriki ushuhuda wako ili kufariji na kuimarisha mtu mwengine, ama ulifarijiwa na kuimarishwa na maneno ya imani ya mtu mwengine.

Soma 1 Nefi 5:7–9, ukitafuta matokeo ya uzoefu huu kwa imani ya Saria.

  • Ni nini Saria alijifunza kutokana na uzoefu huu?

  1. ikoni ya shajaraJibu swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Jinsi gani ushuhuda wa Saria katika 1 Nefi 5:8 unafanana na ushuhuda wa Nefi katika 1 Nefi 3:7?

1 Nefi 5:10–22

Lehi anapekua mabamba ya shaba

Nefi na nduguze walihatarishi maisha yao, wakajitolea mali ya familia yao, kusafiri mwendo mrefu, na walilindwa na Mungu katika safari yao ya kupata mabamba ya shaba. Kama ungekuwa mwanafamilia wa Lehi, jitihada zao zingevutia vipi fikra zako za kusoma kile kilichokuwa katika mabamba ya shaba?

Baada ya wanawe kurejea salama, Lehi alianza kupekua yaliyomo ndani ya mabamba ya shaba. Soma 1 Nefi 5:11–14, na uweke mstari chini kwa yaliyomo ndani ya mabamba ya shaba.

Soma 1 Nefi 5:17–20, ukitafuta jinsi kuchunguza mabamba ya shaba ilimwathiri Lehi. Kulingana na kile ulisoma katika vifungu hivi, unawezaje kukamilisha kutamka kanuni ifuatayo? (ona1 Nefi 5:17): Tunapopekua maandiko, tunaweza kuwa

Mzee Robert D. Hales wa Jamii ya Wale Mitume Kumi na Wawili alidhibitisha ukweli huu:

“Tunapotaka kusema na Mungu, tunaomba. Na wakati tunapotaka Yeye kuongea nasi, tunayapekuea maandiko; kwani maneno Yake husemwa kupitia manabii Wake. Kisha Yeye atatufunza sisi tunaposikiliza mnong’ono wa Roho Mtakatifu.

“Kama haujasikia sauti Yake ikiongea nawe hivi majuzi, rudi kwa macho mapya na masikio mapya kwenye maandiko. Ni tegemeo kuu la kiroho” (“Holy Scriptures: The Power of God unto Our Salvation,” Ensign or Liahona, Nov. 2006, 26–27).

  1. ikoni ya shajaraAndika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kuhusu wakati ulipopekua maandiko na kuhisi Roho wa Bwana.

Soma 1 Nefi 5:21–22, na utafute ni kwa nini mabamba yalikuwa “yenye thamani kubwa” kwa Lehi na familia yake.

Geukia wimbo “As I Search the Holy Scriptures” (Wimbo, no. 277), na utaona baraka inayoweza kuja kupitia kupekua maandiko. Tafakari juu ya masomo yako ya kila siku ya maandiko. Unawezaje kuboesha katika masomo yako ya kila siku ya maandiko?

Kuna hekima katika kujifunza maandiko tunaposafiri kupitia maisha—nyikani mwetu. Kumbuka kuwa mabamba ya shaba yalipatikana kupitia kwa imani na kujitolea na kwamba bila mabamba ya shaba Lehi na familia yake, hawangepokea baraka zifaazo katika safari yao (ona 1 Nefi 5:22). Unapopekua maandiko, utajawa na Roho wa Bwana na kupokea nguvu na imani ili kutii amri Zake.

1 Nefi 6:1–6

Nefi anaandika ili kushawishi wote kuja kwa Yesu Kristo

Chagua kitabu nyumbani kwako au fikiria kuhusu kitabu unachofahamu. Unafikiria lengo la mwandishi lilikuwa nini katika kuandika kitabu hicho? Kujua lengo la mwandishi itakusaidiaje unaposoma?

Soma 1 Nefi 6:3–6, na uweke mstari chini ya lengo la Nefi katika kuandika kumbukumbu. Kishazi “Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo” (kifungu 4) inamaanisha Yehova, ambaye ni Yesu Kristo. Lengo la Nefi liliendelezwa na wale wote ambao maadiko yao yanapatikana katika Kitabu cha Mormoni: Dhumuni moja la Kitabu cha Mormoni ni kuwashawishi watu kuja kwa Yesu Kristo.

  1. ikoni ya shajaraKatika shajara yako ya kujifunza maandiko, elezea jinsi kuelewa madhumuni ya Nefi ya kuandika kumbukumbu yake yanaweza kuathiri vile unajifunza Kitabu cha Mormoni.

Nefi anatengeneza mabamba

1 Nefi 9

Nefi anatengeneza seti mbili za mabamba

Katika 1 Nefi 9 (ona pia sura 6), Nefi alielezea kwamba aliamuriwa kutengeneza seti mbili za kumbukumbu—hizi zinajulikana kama mabamba madogo na mabamba makubwa ya Nefi. Mabamba madogo yalipatikana katika historia takatifu ya watu wake—huduma ya manabii na funuo za Bwana—na mabamba makubwa yalipaswa kuwa na historia ya ulimwengu (ona 1 Nefi 9:2–4). Nefi alitumia maneno “haya mabamba” na “mabamba mengine” kumaanisha seti mbili za mabamba ambayo Bwana alimwamuru kutengeneza. Pembeni mwa maandiko yako karibu na 1 Nefi 9, andika muhtasari kama ifuatavyo ili kukusaidia kukumbuka seti gani ya mabamba ambayo Nefi alikuwa akimaanisha: “haya mabamba” ” = mabamba madogo (wakfu); “mabamba mengine” = mabamba makubwa (kilimwengu).

Unaposoma Kitabu cha Mormoni utakuja kuelewa kwa nini Nefi aliweka seti mbili za kumbukumbu. Nefi aliongozwa kutengeneza muhtasari, toleo lililofupishwa, la historia la baba yake (inayopatikana katika 1 Nefi 1–8) kwenye mabamba madogo. Kwa karibu miaka 1,000 baadaye, nabii Mormoni aliamuriwa na Bwana kujumuisha mabamba madogo ya Nefi pamoja na mabamba ya dhahabu (ona Maneno ya Mormoni 1:7). Watu wote wawili hawakujua ni kwa nini iliwabidi kufanya kile walichofanya (ona 1 Nefi 9:5), bali walifuata amri ya Bwana.

  1. ikoni ya shajaraUnaposoma 1 Nefi 9katika kijiufunza kwako kwa binafsi, tafakari juu ya na uandike kumbukumbu katika shajara yako ya kujifunza maandiko kwa nini ni muhimu kumtii Bwana hata kama hawaelewi kamili sababu Zake.

  2. ikoni ya shajaraAndika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza1 Nefi 5–6 na 9 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu: