Seminari
Kitengo 3: Siku 3, 1 Nefi 10–11


Kitengo 3: Siku ya 3

1 Nefi 10–11

Utangulizi

Mafundisho ya Lehi kuhusu mti wa uzima na unabii wake kuhusu Wayahudi iliongeza hamu ya Nefi ya kuona, kusikiza, na kujua mwenyewe mambo ambayo baba yake alikuwa ameona. Wakati Nefi alikuwa akitafakari juu mambo ambayo baba yake alikuwa amesema, “alinyakuliwa na Roho wa Bwana” (1 Nefi 11:1) na kuona ono la mti wa uzima mwenyewe. Katika ono lake aliona pia maisha ya Mwokozi, huduma, na kifo—Nefi alishuhudia upendo wa Mwokozi kwetu sisi. Unapojifunza somo hili, tafakari kile unaweza kujifunza kutoka kwa mfano wa Nefi wa kutafuta ufunuo wa binafsi. Pia fikiria juu ya maisha na kazi ya Mwokozi na upendo Wake mkuu kwetu sote.

1 Nefi 10:1–16

Lehi anatoa unabii

Baada ya kusimulia ono la mti wa uzima, Lehi alitoa unabii kuhusu matukio ya siku zijazo. Unabii wake umeandikwa katika 1 Nefi 10:1–16. Soma 1 Nefi 10:4–6, na uweke alama kwa majibu ya maswali yafuatayo katika maandiko yako:

  • Ni lini Lehi alitoa unabii kwamba Masiya—Mwokozi—angekuja?

  • Lehi alisema nini kingewatokea wale “wasio mtegemea huyu Mkombozi”?

1 Nefi 10:17–11:6

Nefi anatafuta kuona, kusikia, na kujua kweli kama zile za baba yake

Fikiria tukio lifuatalo, na ufikirie jinsi watu waliohusika katika hali sawa wanaweza kuwa na uzoefu tofauti: Vijana watatu walihudhuria mkutano wa Kanisa mmoja. Mmoja wao anahisi kwamba mkutano ulikuwa wa kuchosha na wa kupoteza wakati. Mwingine anafikiria mkutano ulikuwa mzuri lakini haukujifunza chochote. Wa tatu alihisi ameinuliwa na Roho Mtakatifu na kupokea maongozi ya binafsi na mwelekeo hata zaidi ya kile kilifunzwa katika mkutano.

Unapojifunza uzoefu wa Nefi katika 1 Nefi 10:17–11:6, tambue kile Nefi alifanya ambacho kilimruhusu kupokea ufunuo wa ziada zaidi ya kile baba yake alimfunza.

Soma 1 Nefi 10:17, na uweke mstari kile Nefi alihisi baada ya kusikia kuhusu ono la Lehi.

Soma 1 Nefi 10:19, na upate kishazi kinachofundisha jinsi siri za Mungu zinafunuliwa kwetu.

Kulingana na 1 Nefi 10:19, wale wanaotafuta kwa bidii hufunguliwa siri za Mungu. Andika kile unafikiri inamaanisha kutafuta kwa bidii.

Nefi alipeana mfano bora wa kutafuta ufunuo kwa bidii. Soma 1 Nefi 10:17–19 na 11:1–6; chagua mbili ya mada tatu zilizoorodheshwa katika chati ifuatayo—hamu, imani, na kutafakari; na uandike majibu yako kwa ulinganifu na maswali katika chati.

Hamu

Ni nini ambacho Nefi alikuwa na hamu kuona?

Hamu zetu zinaathiri vipi uwezo wetu wa kupokea ufunuo?

Ni nini ambacho unatamani kujua kutoka kwa Bwana?

Imani

Ni baadhi ya mambo gani ambayo Nefi aliamini katika ambayo yaliongoza kwa ufunuo?

Unafikiri imani hizi zinaweza kuathiri vipi uwezo wetu wa kupokea ufunuo leo?

Unaamini kile Bwana amekufunulia?

Kutafakari (kufikiria kwa undani kuhusu kitu fulani; kufungua akili na moyo wako kwa Roho Mtakatifu)

Ni nini ilitendeka wakati Nefi akikaa na akitafakari? (Ona 1 Nefi 11:1.)

Unafikiri ni kwa njia gani kutafakari huelekeza kwa ufunuo?

Unaweza kufanya nini ili kutafakari injili katika maisha yako?

Fanya muhtasari wa kanuni ya injili uliyojifunza kutoka kwa uzoefu wa Nefi kwa kukamilisha taarifa ifuatayo: Mungu hufunua kweli kwa wale wote wanao .

  1. Andika jibu kwa moja au maswali yote yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni lini ulihisi Mungu alijibu maombi yako au kuhisi uvuvio kutoka kwa Roho wakati ulipokuwa ukitafuta usaidizi au mwongozo kutoka kwa Bwana?

    2. Ni njia gani moja unaweza kutafuta uongozi kutoka kwa Bwana?

1 Nefi 11:7–36

Nefi alishuhudia ufadhili wa Yesu Kristo

Nefi aliendelea kutafakari na kutafuta mwongozo mtakatifu wakati wa ono lake Soma taarifa ifuatayo kutoka kwa Rais Boyd K. Packer, Rais wa Akidi ya Wale Mitume Kumi na Wawili, na utambue kile alisema kilikuwa lengo kuu la ono la Nefi:

“Unabii kuhusu Masiya unapatikana katika Agano la Kale. Lakini Kitabu cha Mormoni kinaandika ono la tukio lisilo na kipimo katika Agano la Kale

“Baada ya watu wa Lehi [kutoka Yerusalemu], Lehi alipata ono la mti wa uzima. Mwanawe Nefi aliomba ili kujua maana yake. Kwa majibu, alipewa ono la ajabu la Kristo.

“Katika ono hilo aliona:

  • Bikira akimbeba mtoto mikononi mwake,

  • Yule atakayetayarisha njia—Yohana Mbatizaji,

  • Huduma ya Mwana wa Mungu,

  • Wengine kumi na wawili wakimfuata Masiya,

  • Mbingu zikifunguka na malaika wakiwahudumia,

  • Umati wa watu hubarikiwa na kuponywa,

  • Kusulubishwa kwa Kristo,

  • Hekima na kiburi cha ulimwengu kinapinga kazi yake. (Ona 1 Ne. 11:14–36.)

“Ono hilo ndilo ujumbe muhimu wa Kitabu cha Mormoni” (“The Things of My Soul,” Ensign, May 1986, 60–61).

Malaika alimsaidia Nefi kutambua maana ya mti wa uzima na kisha akauliza, ““Je! Unajua maana ya ule mti ambao baba yako aliuona? (1 Nefi 11:21). Rejea maana ya mti kwa kuweka mstari kwa vishazi ambavyo Nefi na malaika walivitumia kuelezea mti katika 1 Nefi 11:21–24.

Soma 1 Nefi 11:16 na uweke mstari kwa swali la mwanzo ambalo malaika aliuliza Nefi. Unaweza kuandika katika maandiko yako kuwa neno ufadhili linamaanisha kuteremka kwa hiari kutoka kwa cheo cha juu ili kusaidia au kubariki wengine.

Katika 1 Nefi 11:17, tambua majibu ya Nefi kwa swali la malaika Nefi alijua nini? Hakujua nini? Baada ya majibu ya Nefi, malaika alimuonyesha kwamba ufahdili wa Yesu Kristo huonyesha upendo wa Mungu kwetu sisi.

Baada ya kujifunza maana ya neno ufadhili, soma 1 Nefi 11:13–21, kisha usome dondoo ifuatayo kutoka kwa Mzee Gerald N. Lund, ambaye alikuwa akihudumu kama mshiriki wa Wale Sabini, na utafakari jinsi kuzaliwa kwa Yesu kunaonyesha ufadhili wake na upendo wake kwetu: “Hapa alikuwa Yesu—mshiriki wa Uungu, Mzaliwa wa kwanza wa Baba, Muumba, Yehova wa Agano la Kale—sasa akiacha sehemu Yake tukufu na takatifu; akivua Mwenyewe utukufu na ufahari wote na kuingia katika mwili wa mtoto mchanga; hasiyejiweza, mwenye kutegemea kabisa mama na baba Yake wa ulimwenguni. Kwani Yeye hakuja kwenye kasri za kifahari za ulimwenguni na kuvalishwa kwa zambarau [ishara ya ufalme] na kupatiwa johari bali akaja kwenye hori la chini ikawa inashangaza. Cha kushangaza zaidi ni kwamba malaika alimwambia Nefi, ‘Tazama ufadhili wa Mungu!’” (Jesus Christ, Key to the Plan of Salvation [1991], 16).

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko kinachomaanisha kwako kuwa Yesu Kristo “Atashuka kutoka ufalme wake takatifu” (“I Stand All Amazed,” Hymns, no. 193) na wadhifa wake tukufu katika maisha kabla ya maisha ya dunia kuzaliwa kama

Soma 1 Nefi 11:27, na utambue jinsi ubatizo wa Mwokozi pia unaonyesha ufadhili Wake. Ingawa hakuwa na dhambi, alibatizwa ili kuonyesha utiifu Wake kwa amri za Mungu. Pia inaonyesha upendo Wake kwetu kwa kutupatia mfano wa kufuata.

Picha
Yohana Mbatizaji Anabatiza Yesu

Soma 1 Nefi 11:28–31, na ufikirie jinsi maisha ya Yesu Kristo ya utumishi kwa wengine unaonyesha ufadhili Wake. Tambua ni nani Mwokozi alihudumia na kuponya.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko jinsi kile ulichosoma katika 1 Nefi 11:28–31kinaonyesha upendo wa Mwokozi kwa watu Wake. Unahisi hii inahusiana vipi na upendo Wake kwako leo?

Soma 1 Nefi 11:32–33, na utafakari jinsi kusulubishwa kwa Yesu Kristo kunaonyesha ufadhili Wake. Soma taarifa ifuatayo kutoka kwa Mzee Earl C. Tingey, ambaye alikuwa mshiriki anayehudumu wa Urais wa Wale Sabini, na utafute kile alisema kuhusu jinsi Upatanisho wa Mwokozi unaonyesha upendo Wake na kukubariki:

Kama mmoja aliyechaguliwa kutimiza mahitaji ya Upatanisho, Yesu Kristo alikubali . kujaribiwa, kukejeliwa, kuhukumiwa, na kusulubiwa, ingawa alikuwa na uwezo na mamlaka ya kuzuia matendo kama hayo.

Picha
Rais John Taylor

“Rais John Taylor alieleza ufadhili wa Kristo katika maneno haya matamu: ‘Ilikuwa muhimu zaidi kwamba ajishushe chini ya vitu vyote, ili aweze kuinua wengine juu ya vitu vyote …’ [The Mediation and Atonement (1882), 144].

“Mateso ya Kristo katika Bustani ya Gethsemani inaashiria sifa muhimu zaidi ya Kristo, upendo Wake kamili. Hapa tunaona kuwa alitupenda sote kwa kweli. …

“Upatanisho ni tukio linalotuwezesha kupatanishwa na Mungu. … Kwa namna ya familia, inamaanisha kuunganishwa mmoja na mwengine na pamoja na Mungu na Mwanawe, Yesu Krsito. Inamaanisha huzuni kwa kutengana utakuwa furaha kupitia kuungana” (“The Great Plan of Happiness,” Ensign or Liahona, May 2006, 73–74).

Upatanisho wa Yesu Kristo ulikuwa sehemu muhimu ya ufadhili Wake na onyesho muhimu la upendo Wake kwetu.

  1. Andika katika shajara yako ya kujifunza maandiko vile kujua kuhusu ufadhili wa Yesu Kristo kunaathiri hisia zako na upendo Kwake.

Hitimisha somo la leo kwa kuimba, kusikiza, au kusoma maneno ya wimbo “I Stand All Amazed” (Hymns, no. 193). Tambua vishazi vinavyoshuhudia yale uliyojifunza leo. Tafakari kwa nini baraka za Upatanisho wa Yesu Kristo ni za “kutamaniwa sana” na “kufurahisha sana” kwako (ona 1 Nefhi 11:22–23). Kama Nefi, unapotafuta kwa bidii uelewa kupitia ufunuo, utasogea karibu na Bwana na kuhisi uwezo wa dhabihu Yake katika maisha yako na shangwe iletayo.

  1. Andika yafuatayo mwisho wa kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 1 Nefi 10–11 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha