Seminari
Kitengo 3: Siku 4, 1 Nefi 12–14


Kitengo 3: Siku ya 4

1 Nefi 12–14

Utangulizi

Maelezo ya ono la Nefi, ambayo yanaanza katika 1 Nefi 11, yanaendelea katika 1 Nefi 12–14. Katika ono lake Nefi aliona majanga ya kutisha, ikiwemo kuangamizwa mwishowe kwa uzao wake. Aliona waovu wakitoa kweli halisi na za thamani kutoka kwenye Biblia, kuwasababisha wengi kujikwaa kiroho. Hata hivyo, ono la Nefi pia lilimpatia sababu ya kuwa na matumaini katika siku zijazo. Aliona Columbus na ukoloni wa Marekani Aliona kwamba Bwana angetayarisha njia ya Urejesho wa injili katika siku za mwisho, ikiwemo kurejesha kweli nyingi halisi na za thamani ambazo zilikuwa zimepotea. Nefi alishuhudia vile katika siku za mwisho Bwana atawasaidia na kuwalinda wale watakaoishi kwa haki. Unapojifunza 1 Nefi 12–14, tafakari umuhimu katika maisha yako wa kweli halisi na za thamani zinazofundishwa katika Kitabu cha Mormoni na maandiko mengine ya siku za mwisho. Unapojitahidi kuishi kwa haki na kutii maagano yako na Mungu, wewe pia unaweza kushinda dhidi ya uovu.

1 Nefi 12

Nefi anaona siku zijazo za mataifa ya Wanefi na Walamani

Katika 1 Nefi 12 Nefi alieleza kile aliona kwa ajili ya siku zijazo za uzao wake na jinsi wataathirika na vishawishi vilivyowakilishwa na ukungu wa giza na jengo kubwa na pana. Alitumia neno mbegu ili kumaanisha uzao.

Nefi aliona kwamba baadhi ya uzao wake watapokea baraka zote za Upatanisho. Hata hivyo, pia aliona kwamba uzao wake hatimaye utaangamizwa na Walamani. Soma 1 Nefi 12:19, na upige mstari sababu za kuaangamizwa kwa Wanefi. Fikiria jinsi unaweza kujikinga dhidi ya kiburi na kuzuia majaribu ya shetani.

1 Nefi 13:1–9

Nefi anaona kanisa kuu na la machukizo

Zungushia mojawapo ya michezo ifuatayo ambayo umecheza au kutazama, na uongeze mchezo mwengine kwenye orodha ambayo umecheza au kutazama:

  • Kandanda

  • Kriketi

  • Mpira wa Kikapu

  • Besiboli

  • Tenisi ya Mezani

  • Tenisi

  • Ragbi

  • Hoki ya Barafuni

  • Voliboli

  • Kandanda ya Kimerikani

Katika michezo ya kulipwa, timu mara nyingi huchunguza michezo iliyopita na mikakati ya timu pinzani kabla hawajashindana. Kuelewa nia ya timu pinzani, mbinu na mikakati kunaweza kutusaidia kujiandaa ili kujilinda dhidi yao.

Katika 1 Nefi 13, Nefi alieleza kile aliona kuhusu wale wanaopinga Kanisa la Mungu katika siku za mwisho. Soma 1 Nefi 13:1–6, na utambue kile Nefi aliona ambacho kitaundwa miongoni mwa Wayunani na kile malaika alisema kukihusu.

Picha
Mzee Bruce R. McConkie

Hii “kanisa kuu na la machukizo” ambao Nefi aliona haliwakilishi kikundi fulani. Mzee Bruce R. McConkie wa Akidi ya wale Mitume Kumi na Wawili alikieleza kama “mashirika yote … ya jina au hali yoyote ile … ambayo yameundwa ili kuwapeleka watu kwenye njia ambayo inawaelekeza mbali na Mungu na sheria zake na basi kuondoka kwa wokovu katika ufalme wa Mungu” (Mormon Doctrine, 2nd ed. [1966], 137–38). Unaweza kutaka kuandika maelezo ya Mzee Bruce R. McConkie karibu na 1 Nefi 13:4–6.

Soma 1 Nefi 13:8–9, na utambue mapenzi na motisha ya kanisa kuu na la machukizo

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Unafikiria kwa nini ni muhimu kujua kwamba Shetani amepanga majeshi yake kutuelekeza mbali kutoka kwa Mungu na sheria Zake?

Unaposoma 1 Nefi 13 zaidi, utaona njia moja ambayo kwayo kanisa kuu na la machukizo limejaribu kuzuia wale wanaomtafuta Mwokozi.

1 Nefi 13:10–42

Nefi anawaona Wayunani wa siku zijazo wakiwa na Biblia, Kitabu cha Mormoni, na maandiko ya siku za mwisho.

Ili kukabiliana na madhara ya kanisa kuu na la machukizo, Bwana alitayarisha njia kwa Urejesho wa injili Yake. Katika 1 Nefi 13, Nefi aliona matukio kama vile Columbus na wahamiaji wakija katika nchi ya ahadi kwa sababu “Roho ya Mungu … ilishuka [kukaa au kufanya kazi] juu [yao] (ona 1 Nefi 13:12–13). Pia alitabiri Vita vya Marekani vya Uhuru—wakati Wayunani ambao walitoka utumwani wakipigana na Wayunani wa nchi ya mama yao [ambao] walikusanyika pamoja dhidi yao, lakini walikombolewa na nguvu za Mungu kutoka mikononi mwa mataifa mengine yote. 1 Nefi 13:16–19).

Picha
maandiko

Soma 1 Nefi 13:20–23, na utambue kitabu ambacho Nefi aliona wakoloni wayunani wa mapema katika nchi ya ahadi wakibeba miongoni mwao.

Andika “Biblia” katika maandiko yako karibu na1 Nefi 13:20. Nefi alieleza kwamba Biblia itakuwa “ya thamani kuu” kwetu (1 Nefi 13:23) na kuwa wakati ilipoandikwa kiasili “ilikuwa na ujalivu wa injili ya Bwana” (1 Nefi 13:24). Tumia 1 Nefi 13:26–27, 29 ili kujaza mapengo katika muhtasari ifuatayo:

Kanisa kuu na la machukizo liliondoa “sehemu nyingi ambazo ni na zaidi ; na pia wamepunguza maagano mengi ya Bwana” kutoka kwa Biblia (1 Nefi 13:26). Waliondoa vitu hivi ili “ njia nzuri za Bwana, kwamba wazewe macho na mioyo ya watoto wa watu” (1 Nefi 13:27). Kwa sababu vitu hivi vimepotea, “wengi zaidi watapotea ” (1 Nefi 13:29).

Soma tena muhtasari hapa juu baada ya kujaza mapengo.

Lengo moja la kanisa kuu na la machukizo ni “kuchafua njia nzuri za Bwana” (1 Nefi 13:27) kwa kuondoa mengi ya kweli halisi na za thamani. “Kuchafua” ni kusababisha kugeuka kando au mbali na kitu ambacho ni sahihi. Fikiria kuhusu athari mbaya ya kugeuka kando au kutoka mbali na “njia sahihi za Bwana.”

Tumia maandiko yako kujibu maswali yafuatayo:

  • Kulingana na 1 Nefi 13:34, ni nini Bwana atalete kwa sababu ya neema zake? (Itakuwa muhimu kujua kwamba kichwa “mwana Kondoo” inahusu Mwokozi, Yesu Kristo.)

  • Katika 1 Nefi 13:35–36, ni nini Mwokozi alisema kitafichwa ili kuja kutokea kwa Wayunani?

  • Katika 1 Nefi 13:36, ni nini malaika alisema kiliandikwa katika kumbukumbu kilichofichwa— Kitabu cha Mormoni?

  • Kama ziada kwa Kitabu cha Mormoni, ni “vitabu vingine” gani ambayo 1 Nefi 13:39 inalenga?

Soma 1 Nefi 13:40–41, na uweke mstari kile Kitabu cha Mormoni na hivi “vitabu vingine” vitawafunulia watu wote. Ni muhimu kutambua kuwa ni lazima tuje kwa Mwokozi “kulingana na maneno ambayo yatafumbuliwa kwa mdomo wa Mwana Kondonoo” (1 Nephi 13:41)—maandiko.

Kupitia sehemu hii ya ono la Nefi, tunajifunza kuwaKitabu cha Mormoni na maandiko ya siku za mwisho yanarejesha kweli halisi na za thamani ambazo zinatusaidia kujua kuwa Yesu Kristo ndiye Mwana wa Mungu na zinatusaidia kujua jinsi ya kuja Kwake.

  1. Andika jibu kwa swali lifuatalo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Jinsi gani kweli halisi na za thamani katika Kitabu cha Mormoni na maandiko mengine za siku za mwisho zimeongoza ushuhuda wako wa Yesu Kristo?

    2. Zimekusaidia vipi kuelewa na kuishi injili Yake?

Chukua muda kutathmini jinsi kujifunza maandiko vyema kunakusaidia kuja karibu na Mwokozi.

1 Nefi 14:1–17

Nefi aliona vita kati ya kanisa kuu na la machukizo na lile Kanisa la Mwanakondoo wa Mungu.

Katika 1 Nefi 14 tunasoma kuhusu vita kati ya kanisa kuu na la machukizo na lile Kanisa la Mwanakondoo wa Mungu. Soma 1 Nefi 14:10–13, na utambue ni upande gani utakao kuwa na watu wengi. Tazama katika 1 Nefi 14:12 kwa nini idadi ya watu wanaounga mkono Kanisa la Mwanakaondoo watakuwa wachache na kwa nini kanisa kuu na la machukizo liliweza kukusanya pamoja umati mkubwa.

Utahisi vipi ikiwa mna idadi kidogo na mnapigana katika vita? Soma 1 Nefi 14:14, na upige mstari chini ya vishazi vinavyotambua usaidizi “watakatifu wa kanisa la Mwanakondoo” na “watu wa agano wa Bwana” wanaopigana dhidi ya uovu watapokea.

Kanuni muhimu ya injili inayofundishwa katika 1 Nefi 14:1–17 ni tunapoishi kwa haki na kutii maagano yetu, uwezo wa Mungu utatusaidia kushinda dhidi ya uovu.

  1. Andika kifungu kifupi katika shajara yako ya kujifunza maandiko ukieleza jinsi kuwa mmoja wa “watu wa agano wa Bwana” na “kujikinga kwa utakatifu” (kuishi kwa haki) kumeweza kukusaidia kushinda dhidi ya majaribu ambayo yanaweza kukuelekeza mbali na Mungu na amri Zake.

Nefi aliona kuwa katika siku za mwisho wale wanaounga mkono kanisa kuu na la machukizo “wataangamizwa kabisa” (1 Nefi 14:3). Unaweza kuwa na matumaini kwamba ufalme wa Mungu utashinda katika siku za mwisho.

  1. Andika yafuatayo mwisho wa kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    Nimejifunza 1 Nefi 12–14 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ninaotaka kushiriki na mwalimu wangu:

Chapisha