Seminari
Kitengo cha 31: Siku ya 1, Etheri 13–15


Kitengo cha 31: Siku ya 1

Etheri 13–15

Utangulizi

Nabiii Etheri alitoa unabii wa Yerusalemu Mpya. Alimuonya pia Koriantumuri, Mfalme wa Wayaredi, kwamba watu wake wangeangamizwa kwa sababu ya uovu, na alimhimiza Koriantumuri na nyumba yake watubu. Wakati Koriantumuri na watu wake walikataa kutubu, vita na uovu ilizidi kwa miaka mingi hadi taifa zima la Wayaredi liliangamizwa. Etheri na Koriantumuri tu ndio walibaki hai kushuhudia utimizaji wa unabii wa Etheri.

Picha
vita vya wayaredi

Etheri 13:1–12

Moroni anaandika unabii wa Etheri wa Yerusalemu Mpya na Yerusalemu ya kale

Zingatia miji kadhaa hivi leo ambayo ina majina ya mbadala yanayoonyesha sehemu muhimu ya mji. Kwa mfano, Paris, Ufaransa, unajulikana kama City of Light. Ili kuanza, ona kama unaweza kuambatanisha miji iliyo hapa chini na majina yake mbadala sahihi ( majibu yametolewa mwishoni mwa somo).

Kairo, Misri

The Windy City

Manila, Philippines

The City of a Thousand Minarets

Chicago, Amerika

The Eternal City

Mji wa Mexico, Mexico

The Pearl of the Orient

Roma, Italia

The City of Palaces

Somo la leo linaangazia miji miwili kuu katika siku za mwisho: (1) Yerusalemu na (2) Yerusalemu Mpya. Katika siku za mwisho miji hii miwili itajulikana kwa wema wake. Etheri alifundisha Wayaredi kwamba nchi ambapo waliishi ilikuwa mahali pa mji wa siku zijazo uitwao Yerusalemu Mpya.

Soma Etheri 13:2–8. Bwana alimfunulia Nabii Joseph Smith kwamba Yerusalemu Mpya iliyotambulishwa katika Etheri 13:6 ingejengwa katika Jackson County, Missouri, USA (ona M&M 57:1–4; 84:1–4). Etheri alisema nini kuhusu miji hii katika Etheri 13:3, 5? Tafakari huenda kukawa vipi kuishi katika mji kama huo. Soma Etheri 13:10–11 ili kujifunza kile ambacho mtu lazima apitie ili kuishi katika miji mitukufu ya Yerusalemu Mpya na Yerusalemu ya kale (ambayo itakuwa tukufu itakapojengwa kwake Bwana; ona Etheri 13:5).

Jina lingine la Yerusalemu Mpya ni Sayuni (ona Musa 7:62; Makala ya Imani 1:10). Hata kama hatuishi katika Yerusalemu ama Yerusalemu Mpya, waumini wote wa Kanisa wanaweza kutafuta kujenga Sayuni. Tunaweza kujitayarisha kuishi katika mahali patakatifu, ikiwa ni pamoja na ufalme wa selestia wa Mungu, tunapokuwa wasafi kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo.

Etheri 13:13–15:34

Wayaredi wamkataa Etheri na kuendelea katika uovu na vita hadi wakaangamizwa

SomaEtheri 13:13–19, na utafute hali ya jamii ya Wayaredi katika siku za Etheri. Soma Etheri 13:20–22 ili kugundua ujumbe wa Etheri kwake Koriantumuri na jinsi Koriantumuri na watu wake waliupokea.

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    1. Ni kwa njia gani umeona watu katika siku zetu wakifanya mioyo yao kuwa migumu na kuwakataa watumishi wa Bwana?

    2. Utafanya nini ili kujiweka kuwa imara katika imani na kutii maneno ya manabii?

Kama ilivyoandikwa katika Etheri 13:23–14:20, Koriantumuri alipigana vita na watu kadhaa ambao walijaribu kuchukua ufalme kutoka kwake, ikiwa ni pamoja na Sharedi, Gileadi na Libi. Hatimaye, taifa lote la Wayaredi lilimezwa katika vita. Adui wa Koriantumuri wa mwisho alikuwa mtu aliyeitwa Shizi. Kiwango cha maangamizo miongoni mwa Wayaredi kutokana na vita hivi kimeelezewa kwa utondoti katika Etheri 14:21–25 na Etheri 15:1–2.

Soma Etheri 15:3–6 ili kugundua kile ambacho Koriantumuri alijaribu kufanya ili kuokoa watu waliobaki kutokana na uangamizi. Fikiria ni kwa nini Shizi alikataa pendekezo la Koriantumuri na kwa nini watu katika majeshi yote mawili walikataa kujisalimisha (ona pia Etheri 14:24).

Soma Etheri 15:12–17, na utafute maelezo kwa utondoti kuhusu hali ya Wayaredi. Ni nini unapata hasa kutisha ama kuhuzunisha kuhusu hali yao? Kumbuka kwamba Etheri alikuwa ametumia miaka mingi akiwaonya watu watubu (ona Etheri 12:2–3; 13:20). Soma Etheri 15:18–19, na utambue matokeo ambayo huja kutoka kwa kukataa maonyo ya Bwana kutubu. Kulingana na kile ulichosoma, kamilisha kauli hii: Tukikataa maonyo ya Bwana kutubu, basi .

Katika nafasi iliyo hapo juu, huenda uliandika kanuni kama vile ile ifuatayo: Tukikataa maonyo ya Bwana kutubu, Roho Yake hutuacha na Shetani hupata nguvu juu ya mioyo yetu.

  1. Ukitumia Etheri 15:19 na kanuni tunayojifunza kutoka hapo, eleza ni kwa nini moja au zaidi ya vijisababu vifuatavyo ambavyo mtu huenda akatoa siku hizi kwa kukataa kutubu si sahihi:

    1. Ninajua sinema ambazo mimi hutazama haziambatani na viwango vya Kanisa, lakini hazionekani kuwa na athari kwangu.

    2. Kunywa pombe na marafiki zangu si mbaya hivyo. Tunaburudika tu.

    3. Ni ponografia kidogo tu. Si kama kwamba ninaenda nje na kuwa msherati. Hata hivyo, ninaweza kukoma wakati wowote ninajihisi.

    4. Si lazima nitubu sasa. Hiyo inaweza kungoja hadi niwe karibu kwenda misheni ama kuoa hekaluni.

Etheri 15:20–32 inaeleza jinsi majeshi mawili ya Wayaredi yalipigana hadi viongozi wao pekee, Koriantumuri na Shizi, wakabaki. Kisha Koriantumuri alimuua Shizi.

Historia ya Wayaredi inatoa mfano wazi wa kile ambacho huwatendekea watu wakati wanakataa kwa pamoja jitihada za mara kwa mara za Mungu kuwahimiza watubu. Ingawa huenda tusikumbane na maangamizo ya kimwili ya mara moja kwa kukataa kutubu, tutapata hisia za majuto tukikataa maonyo ya Bwana kutubu.

Picha
watu waliouawa kwenye uwanja wa vita
Picha
Mzee Neil L. Andersen

Tafakari kauli ifuatayo kutoka kwa Mzee Neil L. Andersen wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili: “Ninashuhudia kwamba Mwokozi anaweza na ana hamu kutusamehe dhambi zetu. Isipokuwa dhambi za wale wachache ambao huchagua kupotea baada ya kupata kujua ukamilifu, hakuna dhambi ambayo haiwezi kusamehewa. Ni fursa gani ya ajabu kwa kila mmoja wetu kugeuka kutoka dhambi zetu na kuja kwa Kristo. Msamaha wa kiungu ni mojawapo ya matunda matamu zaidi ya injili, ukiondoa hatia na uchungu kutoka kwa mioyo yetu na kuyabadilisha na furaha na amani ya dhamira (“Repent … That I May Heal You,” Ensign ama Liahona, Nov. 2009, 40–41).

Chunguza chochote ambacho huenda unafanya ambacho kinaweza kuwa kina katiza ushawishi wa Roho Mtakatifu katika maisha yako. Zingatia jinsi ungeweza kuvutia nguvu ya Upatanisho wa Yesu Kristo ili kufanya mabadiliko yanayohitajika ambayo yatakusaidia kupokea Roho na kupinga nguvu ya Shetani.

Kutoka Etheri 13–15 tunajifunza kwamba hasira na kulipiza kisasi zinatuongoza kufanya chaguo ambazo zitatuumiza sisi na wengine. Soma na usome tena vifungu vifuatavyo, na ualamishe maneno na vishazi ambavyo vinafundisha ukweli huu: Etheri 13:27; 14:24; 15:6, 22, 28.

Tafakari ni matokeo gani ambayo hasira isiyodhibitiwa inaweza kuwa nayo juu ya familia ama mahusiano mengine. Fikiria kuhusu hali katika maisha yako ambapo huenda ukahitaji kuacha hisia za hasira ama kulipiza kisasi.

Unaposoma kauli ifuatayo ya Mzee David E. Sorensen, mshiriki mstaafu wa Wale Sabini, tafuta jinsi unaweza kushinda hisia za hasira au hamu ya kutafuta kulipiza kisasi: “Wakati mtu ametuumiza ama wale tunaowajali, uchungu huo unaweza kuwashinikiza sana. Inaweza kuhisika ni kama uchungu ama dhuluma ndiyo jambo muhimu sana duniani na kwamba hatuna chaguo lakini kutafuta kulipiza kisasi. Lakini Kristo, Mfalme wa Amani, anatufunza njia bora zaidi. Inaweza kuwa vigumu sana kusamehe mtu madhara wametufanyia, lakini tunapofanya hivyo, tunajifungua kwa maisha bora ya baadaye. Makosa ya mtu mwingine hayadhibiti tena mwendo wetu. Tunaposamehe wengine, inatuweka huru kuchagua jinsi tutakavyoishi maisha yetu wenyewe. Msamaha inamaanisha kwamba shida za siku zilizopita haziamuru hatia zetu, na tunaweza kutazamia siku zijazo na upendo wa Mungu mioyoni mwetu” (“Forgiveness Will Change Bitterness to Love,” Ensign ama Liahona, Mei 2003, 12).

  1. Jibu maswali yafuatayo katika shajara yako ya kujifunza maandiko: Ni wakati gani wewe ama mtu unayemjua amepata uponyaji na uhuru baada ya kuchagua kusamehe?

Unaweza kushinda hisia zozote za hasira na ulipizaji kisasi ikiwa utamgeukia Yesu Kristo na kupokea nguvu ya kusamehe na faraja kupitia Upatanisho Wake. Kumbuka kumgeukia Bwana katika maombi kwa ajili ya usaidizi ambao huenda ukahitaji katika hali hizo.

  1. Andika yafuatayo katika sehemu ya mwisho ya kazi ya leo katika shajara yako ya kujifunza maandiko:

    NimejifunzaEtheri 13–15 na kukamilisha somo hili mnamo (tarehe).

    Maswali ya ziada, mawazo, na umaizi ningetaka kushiriki na mwalimu wangu:

  • Majibu ya shughuli ya kuambatanisha mwanzoni mwa somo: Cairo, Misri (The City of a Thousand Minarets); Manila, Philippines (The Pearl of the Orient); Chicago, USA (The Windy City); Mexico City, Mexico (The City of Palaces); Roma, Italia (The Eternal City).

Chapisha