87 Kaa Nami! Kwa unyenyekevu 1. Kaa nami! Kwani kumekuchwa; Usiniache gizani, Bwana! Wanaposhindwa wasaidizi, Auni wa kweli, kaa nami! 2. Siku zinayoyoma haraka. Duniani raha hufifia. Naona mabadiliko mengi; Ewe Mwaminifu, kaa nami! 3. Kila saa ninakuhitaji. Nani atamshinda Shetani? Mwimo wangu, mwingine hakuna, Kila hali kaa nami, Bwana! Maandishi: Henry F. Lyte, 1793–1847 Muziki: William H. Monk, 1823–1889 Luka 24:29 Yohana 15:4–12