29
Njoo, Ee Mfalme
Kwa ujasiri
1. Njoo, Ee Mfalme!
Tumekungojea,
Huru utufanye
Kwa wako uweza.
Njoo Ewe Mkombozi,
Ukusanye Israeli.
2. Dhambi ukomeshe,
Takasa dunia,
Haki uilete,
Tuweze kuimba,
Nyimbo nzuri, kwa kinubi,
Mfalme tukikulaki.
3. Hosana waimbe
Waliookoka,
Utukufu uje
Kwa kuimba upya,
Nyimbo nzuri za Sayuni
Zitasikika mbinguni.
4. Karibu, Mfalme!
Mahali pa enzi!
Pale Wateule
Watakapokiri,
Na waasi kuabudu
Ndimi zote zitasifu.
Maandishi: Parley P. Pratt, 1807–1857
Muziki: Hajulikani, mnamo 1889