26 Enyi Wana wa Bwana Kwa kushangilia 1. Enyi wana wa Bwana, Tuimbe kwa umoja. Tupaze wetu wimbo Kwake atawalapo. Tutasafishwa wote, Na makosa yafutwe, Tutapoacha dhambi, Tuishi kwa amani. 2. Tutakavyofurahi Tumwonapo Mwokozi! Aja kwa utukufu, Kukomesha maovu. Nyimbo tutamwimbia Mfalme wetu, Bwana. Tutajaa upendo, Woga kufika mwisho! 3. Tutakuwa wasafi, Tutaishi nuruni. Tutamwimbia sifa; Shangwe tutazipaza. Dunia isafishwe Viumbe vyake vyote, Viishi kwa upendo; Furaha kila moyo. Maandishi: James H. Wallis, 1861–1940 Muziki: Lahani ya Uhispania; umepangiliwa na Benjamin Carr, 1768–1831 Mafundisho na Maagano 133:25, 33, 56 Ufunuo 7:9–17