126
Wapendwa wa Mchungaji
Kwa utulivu
1. Wapendwa wa Mchungaji,
Ni kondoo wapendwa;
Tunu pendo awapalo,
Tunu kuliko fedha.
Wapendwa wa Mchungaji,
Na kondoo “wengine”;
Milimani awasaka,
Hata kina chochote.
[Chorus]
Jangwani watangatanga,
Wasumbuka wapweke;
Aenda kuwakomboa,
Zizini warudishwe.
2. Wapendwa wa Mchungaji,
Ndio wanakondoo;
Kuna wanaopotea,
Wadhoofika huko.
Ona, Mchungaji Mwema,
Asaka wapotevu,
Awarudisha kwa shangwe,
Na kwa gharama kuu.
[Chorus]
Jangwani watangatanga,
Wasumbuka wapweke;
Aenda kuwakomboa,
Zizini warudishwe.
3. Wapendwa wa Mchungaji,
Ni “tisini na tisa.”
Apenda wapoteao,
Tumaini wakosa.
Sikia! Wito wa moyo,
Kwa upole asihi:
“Hutafuti mpotevu,
Aliye mbali nami.”
[Chorus]
Jangwani watangatanga,
Wasumbuka wapweke;
Aenda kuwakomboa,
Zizini warudishwe.
4. Malisho yanavutia;
Maji yenye uhai.
Bwana, kwa ari twajibu,
“Ndiyo, tunakubali!
Tufanye wachunga wako;
Tupe pendo la kina.
Tutume mbali jangwani,
Kondoo kuwasaka.”
[Chorus]
Jangwani watangatanga,
Wasumbuka wapweke;
Twendeni kuwakomboa,
Zizini warudishwe.
Maandishi: Mary B. Wingate, 1845–1933
Muziki: William J. Kirkpatrick, 1838–1921