113
Shangwe Kote
Kwa shangwe
1. Shangwe kote, Bwana aja;
Mfalme, karibu!
Kila moyo, tayarisha,
Na Watakatifu,
Na Watakatifu,
Nanyi malaika sifu.
2. Yesu atapotawala
Na Wema waimbe,
Mbuga, mito, na vilima
Kote warudie,
Kote warudie,
Zao shangwe na zivume.
3. Majonzi yatakomeshwa,
Pia na mateso;
Atakuja kuzifanya
Baraka ziwemo,
Baraka ziwemo,
Kote laana ilipo.
4. Shangwe! Kwa Aliye Juu,
Sayuni yakua
Kama nyota kwenye mbingu,
Milele daima,
Milele daima
Mungu zinamtukuza.
Maandishi: Isaac Watts, 1674–1748; Yamebadilishwa na William W. Phelps, 1792–1872. Yalijumuishwa katika kitabu cha kwanza cha nyimbo za Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, 1835.
Muziki: George F. Handel, 1685–1759; Umepangiliwa na Lowell Mason, 1792–1872